Tuesday, October 20, 2020

Man United imeridhishwa na Herrera kwenye safu ya kiungo?

Must Read

Director Kenny: Harmonize alinipeleka WCB nikafanya video ya Lavalava

MWONGOZAJI bora wa video nchini, Kenned Sanga a.k.a Derector Kenny kutoka Zoom Extra, ametua   hapa Jiachie na...

Rogers mwanamuziki anayevutiwa na Marijani

NA JEREMIA ERNEST BONGO Star Search (BSS), ni shindano lililofanikiwa kuibua vipaji vingi vya...

Ihefu, Azam patachimbika Sokoine, Katwila ndani

NA ASHA KIGUNDULATIMU ya Ihefu inatarajia kushuka uwanjani kucheza na Azam ukiwa ni mchezo wa Ligi Kuu...

MANCHESTER, England

NI baada ya presha aliyoipata katika michezo kadhaa ya Ligi Kuu England na michuano mingine, sasa kocha wa Manchester United, Jose Mourinho ameanza kuelewa thamani ya kiungo Mhispania ​​​​​​​Ander Herrera ndani ya kikosi cha kwanza cha klabu hiyo kongwe ya Jiji la Manchester.

Tangu alipopewa nafasi ya kuonesha alichonacho kwenye safu ya kiungo ambayo ilionekana kupwaya kila kukicha, Herrera amecheza kwa kiwango kizuri huku akishirikiana vyema na mchezaji ghali zaidi duniani, Paul Pogba na anatarajiwa kuanza kwenye mchezo dhidi ya mahasimu wao wakubwa England, Liverpool usiku wa Jumatatu ya wiki ijayo.

Yote hayo yanakuja baada ya Herrera kutumia muda mrefu wa kusubiri nafasi yake ndani ya kikosi hicho tangu alipotua United kwa mara ya kwanza akitokea klabu ya Athletic Bilbao. Ukweli ni kwamba suala la kupata nafasi kikosi cha kwanza halikuwa jambo rahisi kwake na alionekana kama mtu asiye na bahati.

Chini ya kocha wa zamani wa timu hiyo, Louis Van Gaal, Herrera alianzishwa kwenye michezo 36 tu kati ya 76 ya Ligi Kuu England ndani ya misimu yake miwili ya kwanza Old Trafford na hata alipokuja Mourinho bado ilionekana kama hatopata nafasi ya kutosha ya kucheza kabla ya kumwingiza kipindi cha pili cha mchezo wao dhidi ya Manchester City mwezi uliopita na aliona mabadiliko makubwa ya kasi ya mchezo yaliyosababishwa na kuingia kwa Mhispania huyo.

Tangu alipoingia dakika za lala salama za mchezo huo dhidi ya City uliomalizika kwa United kukubali kichapo cha mabao 2-1, Herrera amefanikiwa kuikamata akili ya kocha wake hasa baada ya kuanza kuwashinda wapinzani wake wa namba kikosi cha kwanza.

Marouane Fellaini amerudi benchi na Michael Carrick umri unaanza kumtupa mkono, hivyo hiyo ndio imekuwa nafasi nzuri kwa Herrera kuishikilia nafasi ya kiungo mkabaji (ambayo si nafasi yake halisi uwanjani).

Ni wazi sasa tangu Herrera alipoanza kutumika msimu huu pamoja na kiwango cha hali ya juu alichokionesha Pogba dhidi ya Leicester, kikosi cha Mourinho kilitengeneza nafasi nyingi za wazi katika michezo miwili ya mwisho (nane) zaidi ya tano za michezo ya awali.

Umuhimu wa Herrera haupo tu kwenye suala la kupiga pasi ya mwisho lakini ile kasi yake akiwa na mpira na ikizingatiwa anatokea dimba la chini, imekuwa na manufaa makubwa kwa United. Juan Mata anaweza kuwa na uwezo kama huo lakini hajafikia kasi ya Herrera ambaye pengo lilionekana wazi kwenye mchezo wa pili wa hatua ya makundi Ligi ya Europa dhidi ya Zorya Luhansk, ambapo United ilimaliza mchezo kwa kupiga mashuti mawili tu yaliyolenga lango na kushinda kwa bao 1-0 nyumbani Old Trafford.

United iliikosa kasi timilifu ya Mhispania huyu usiku huo. Fellaini alikuwa na nguvu ya kutosha kumiliki dimba lakini hakuweza kufanya kile anachokifanya Herrera (kuiendesha timu kuanzia chini kwa kasi).

Zaidi ya kuiongezea United kasi kwenye safu ya kiungo hasa pale inaposhambulia, uwezo wake wa kucheza kama kiungo cha kukaba umemfanya Pogba kuwa na uhuru mkubwa wa kushambulia, hilo likisaidiwa na takwimu yake ya kuharibu mipango ya wapinzani kwenye mechi mbili dhidi ya Leicester na Stoke akifanya hivyo mara 11 zaidi ya mchezaji yeyote wa United kwenye michezo hiyo.

Herrera amegeuka kuwa mwokozi wa Pogba hivi sasa, unajua kwanini? Kama ilivyoelezwa juu ni kwamba Mhispania anampa uhuru mkubwa Mfaransa huyo anayeshirikiana naye kwenye safu ya kiungo.

Pogba tangu alipoanza kucheza sambamba na Herrera, amefunga bao moja dhidi ya Leicester, ametengeneza nafasi saba za kufunga na kupiga mashuti matatu yaliyolenga lango ndani ya mechi mbili za mwisho. Hiyo ni takwimu nzuri kwake kuliko ya michezo minne aliyoanza sambamba na Fellaini ambaye kiuchezaji wanafanana kitu kinachomnyima uhuru alionao sasa.

Ushirikiano wa Pogba na Herrera unampa matumaini Mourinho, lakini kuanzia wiki ijayo watakutana na changamoto kubwa dhidi ya timu kubwa za Chelsea, Liverpool na Man City kwenye mechi za Ligi Kuu England na hawana budi kuendeleza makali yao ili wazidishe imani ya mashabiki na kocha wao.

Mtihani wa kwanza unaanza Jumatatu pale Anfield watakapokutana na Liverpool inayoongoza kwa kutengeneza nafasi za  mabao ya kufunga.

Ile ya mnyumbuliko wa Roberto Firmino, Sadio Mane, Daniel Sturridge na Philippe Coutinho vitakuwa ni vitu vigumu kwa Herrera kukabiliana navyo lakini ni nafasi ya pekee ambayo huenda Mhispania huyo alikuwa akiisubiria kwa hamu ili kuendelea kuonesha uwezo alionao.

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

Director Kenny: Harmonize alinipeleka WCB nikafanya video ya Lavalava

MWONGOZAJI bora wa video nchini, Kenned Sanga a.k.a Derector Kenny kutoka Zoom Extra, ametua   hapa Jiachie na...

Rogers mwanamuziki anayevutiwa na Marijani

NA JEREMIA ERNEST BONGO Star Search (BSS), ni shindano lililofanikiwa kuibua vipaji vingi vya wanamuziki wa Tanzania ambao miongoni...

Ihefu, Azam patachimbika Sokoine, Katwila ndani

NA ASHA KIGUNDULATIMU ya Ihefu inatarajia kushuka uwanjani kucheza na Azam ukiwa ni mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara  (VPL), utakaochezwa leo...

Mugalu atema cheche Simba

NA ASHA KIGUNDULA MSHAMBULIAJI wa Simba, Chris Mugalu, amesema wanakwenda mkoani Rukwa kupambana na kupata ushindi katika mchezo wao...

Malale aitisha Yanga

NA ZAINAB IDDY KOCHA Mkuu wa timu ya Polisi Tanzania, Malale Hamsini, amezisikia sifa za kocha mpya wa Yanga,...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -