Thursday, December 3, 2020

MAN UTD VS ST ETIENNE NI POGBA NA FLORENTIN

Must Read

HUJUMA NZITO YANGA

NA WINFRIDA MTOI UONGOZI wa Yanga upo katika harakati za kuhamishia mechi zao zilizobaki...

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika...

ETIENNE, Ufaransa

KAKA yake Paul Pogba, Florentin, anatarajia kukichafua na kuivuruga Manchester United wakati ndugu hao wawili watakapokutana kwa mara ya kwanza leo kama mahasimu kwenye Ligi ya Europa.

Florentin mwenye umri wa miaka 26, beki wa St Etienne, anatarajiwa kuwa kikwazo katika mchezo wa kwanza wa hatua ya 32.

Pamoja na Florentin kusisitiza kwamba Paul ambaye amempita miaka mitatu kutokana na kuwa na umri wa miaka 23, ana uwezo wa kuhimili presha ya kuwa mchezaji ghali baada ya kununuliwa kwa pauni milioni 89, aliongeza kwamba mchezaji huyo wa United hapendi kufungwa.

“Kuhusu suala la kumudu kuwa mchezaji bora, ni bora tukaachana nalo kwa kuwa hilo ni suala la vyombo vya habari zaidi, wala halimsumbui,” alisema Florentin.

“Yeye anaendelea kucheza soka lake, ingawa kila kitu anachofanya kinaangalia mara tatu au nne zaidi, kiwe kibaya au kizuri. Anaweza kumudu yote kwa sababu ya uwezo wake wa kiakili aliokuwa nao tangu akiwa mtoto.

“Ni mwenye hasira, hapendi kufungwa. Kichwa chake kinavurugwa anapofungwa. Nimejifunza kuna kufungwa, lakini yeye akifungwa anachanganyikiwa.

“Mechi hizo mbili zitakuwa kali na nina uhakika tutafanya kweli. Hata kama United ni timu kubwa, kila kitu kinawezekana kwenye soka. Suala la kwenye magazeti kwamba ni wazuri dhidi yetu sisi hatujali.

Florentin alidai kwamba alitabiri St Etienne watapangwa na United wakati wakiwa kwenye mazungumzo na Paul kwenye droo, lakini alikiri kwamba familia yao itashindwa imshabikie nani, akiwamo pacha wake Mathias, mshambuliaji wa Sparta Rotterdam.

“Nitabiri, nilikuwa nazungumza na Paul nikamwambia tutakutana,” aliuambia mtandao uefa.com. “Tulianza kuchaguliwa kisha wakafuata wao. Tulicheka na kumwambia: ‘Mambo yamekuwa mambo, tunakutana uwanjani, si kwenye viwanja vidogo vya jirani zetu’. Maana tulipokuwa tunacheza wakati wa mapumziko mara nyingi tunakuwa timu moja. Sasa nitacheza dhidi yake na nitamkaba.”

“Hakitakuwa kitu cha kawaida lakini hilo ndilo soka. Ni kitu cha kipekee kwa familia nzima kwa kuwa sijui kama itatokea tena. Wazazi wetu watakuwa na hisia mchanganyiko kwa kuwa vyovyote vile lazima mmoja apoteze.

“Pacha wangu Mathias atamshabikia nani? Atashabikia kaka zake,” alisema Florentin akiongeza kwamba Paul alikuwa akifurahia kucheza kama mlinda mlango mjini Roissy-en-Brie nchini Ufaransa kabla ya kutengana mwaka 2007.

“Tulikuwa tukikutana na marafiki zetu na kucheza baada ya kutoka shule, wakati huo tukiwa na umri wa miaka 15 au 16, tulikuwa tukicheza kwenye viwanja vya kawaida mitaani,” alisema.

“Huko ndiko tulipoanza kupiga hatua kwenye soka. Paul alikuwa akipenda kukaa kipa kama sehemu ya kujifurahisha. Lakini mara nyingi tulicheza wote nafasi za ndani na wote tulikuwa tunapenda kufunga, huku tukiwaiga mastaa ambao tulikuwa tunawaangalia kwenye televisheni.

“Tulitengana mwaka 2007, ambapo mimi na pacha wangu tulikwenda Hispania, Celta Vigo na Paul kwenda Le Havre. Kufikia viwango tulivyonavyo leo, nafikiri tumefanya hivyo. Sasa wote watatu tunacheza soka la kulipwa, hivyo hatujutii hilo.”

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

HUJUMA NZITO YANGA

NA WINFRIDA MTOI UONGOZI wa Yanga upo katika harakati za kuhamishia mechi zao zilizobaki...

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul 'Ben Pol' ameshukuru mashabiki kwa...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania...

DEWJI: CHAMA NI SIMBA HADI 2022

Kiungo huyo raia wa Zambia, aliyetoa mchangomkubwakwaSimbakufikisharobo fainaliyaLigiyaMabingwaAfrikamsimuwa 2018/19, ikiwamo kutwaa ubingwa wa LigiKuuTanzaniaBarakwa misimumitatu mfululizo, awali ilidaiwa alikuwa yupo katika hatuayamwishoyakujiunganaYanga.

Sven aruka kihunzi

NA ASHA KIGUNDULA KOCHA Mkuu wa Simba, Sven Vandenbroeck, ameruka kihunzi na kuwaachia msala nyota wake, Clatous Chama na...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -