Wednesday, November 25, 2020

Man Utd yatabiriwa kumaliza nafasi ya tano kisa Pogba

Must Read

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika...

DEWJI: CHAMA NI SIMBA HADI 2022

Kiungo huyo raia wa Zambia, aliyetoa mchangomkubwakwaSimbakufikisharobo fainaliyaLigiyaMabingwaAfrikamsimuwa 2018/19, ikiwamo kutwaa ubingwa wa LigiKuuTanzaniaBarakwa misimumitatu mfululizo, awali...

LONDON, England

MCHEZAJI wa zamani wa klabu ya Arsenal, Charlie Nicholas, amesema klabu ya Manchester United itamaliza msimu huu wa 2016/17 katika nafasi ya tano kwenye msimamo wa Ligi Kuu England huku akimtaja kiungo wao ghali duniani, Paul Pogba, kwamba atakuwa chanzo cha jambo hilo kutokea.

United iliyo chini ya kocha Jose Mourinho ambayo ililazimishwa sare ya bao 1-1 na Stoke City wikiendi iliyopita, ipo kwenye nafasi ya sita katika msimamo ikipishana pointi tano na Manchester City ambao wanaongoza ligi.

Kiungo Pogba amekumbwa na wakati mgumu wa kuonyesha kiwango chake kilichomfanya asajiliwe kwa pauni milioni 89 ambapo Nicholas alisema Mfaransa huyo anaangaliwa kwa ukaribu kutokana na kuvunja rekodi ya uhamisho ghali.

“Man United watamaliza nafasi ya tano msimu huu, Mourinho amekwama kwa sababu ametumia fedha kubwa sana kununua wachezaji, hasa Pogba ambaye bado anajaribu kuizoea Man United.

“Anaonekana kutoelewa na haoneshi dalili, kwamba anatakiwa kufanya kazi yake vema ndani ya kikosi chenye nidhamu. Yeye na (Zlatan) Ibrahimovic, wana nguvu kubwa kikosini, wanaangaliwa mno hasa yale mashuti yake kutoka yadi 30.

“Kama angekuwa ni kijana mdogo kutoka kwenye akademi aliyeingia ndani ya timu watu wangemlaumu sana, lakini kwa sababu ya gharama iliyotumika kwenye uhamisho wake anaruhusiwa kufanya anachojisikia.

“Muda si mrefu United itarudi katika hali yake ya kawaida, lakini nahisi itachukua muda mrefu,” Nicholas aliandika kwenye kolamu yake ya uchambuzi ya Sky Sports.

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania...

DEWJI: CHAMA NI SIMBA HADI 2022

Kiungo huyo raia wa Zambia, aliyetoa mchangomkubwakwaSimbakufikisharobo fainaliyaLigiyaMabingwaAfrikamsimuwa 2018/19, ikiwamo kutwaa ubingwa wa LigiKuuTanzaniaBarakwa misimumitatu mfululizo, awali ilidaiwa alikuwa yupo katika hatuayamwishoyakujiunganaYanga.

Sven aruka kihunzi

NA ASHA KIGUNDULA KOCHA Mkuu wa Simba, Sven Vandenbroeck, ameruka kihunzi na kuwaachia msala nyota wake, Clatous Chama na...

Sarpong ‘aua’ shabiki Simba

Na MWANDISHI WETU, MWANZA BAO la dakika ya 29 lililofungwa na Michael Sarpong wa Yanga juzi, limesababisha kifo cha...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -