Monday, August 10, 2020

MANCHESTER UNITED YA MAUAJI 2017/18

Must Read

Klabu zamiminika kuomba kutumia U/Nelson Mandela

NA ASHA KIGUNDULA UONGOZI wa Chama cha Soka Mkoa wa Rukwa (RUREFA), umesema umeanza...

Kipa mpya Azam atamba kumsaulisha Abarola

NA ZAINAB IDDY KIPA mpya wa Azam, David Kissu, ameuahidi uongozi na mashabiki wa...

Yanga: Hatuna mpango na wasugua benchi Msimbazi

NA ZAINAB IDDY UONGOZI wa Yanga, umesema hauna mpango wa kusajili wachezaji wanasugua benchi...

MANCHESTER, England

KILA unaposikia jina la mchezaji fulani likihusishwa na klabu ya Manchester United, basi usimsahau ‘mchizi’ Ed Woodward. Ni mtu mkubwa sana pale Old Trafford, na ndiye atakayehusika kwa asilimia kubwa kuunda kikosi cha Jose Mourinho kwa ajili ya msimu ujao.

Zile dili za kuwaleta Paul Pogba, Zlatan Ibrahimovic, Henrikh Mkhitaryan na Eric Bailly kwa ajili ya kuunda timu ya kazi kwa ajili ya Mourinho ilikuwa na mkono wa Woodward, na kwa namna yoyote ile wengine watatua OT kwa nguvu yake.

Itambulike wazi, kwa sasa United haina budi kutumia vizuri dirisha la usajili kwa ajili ya kunyakua wachezaji bora kama ni kweli watahitaji kuonesha upinzani wa kweli msimu ujao.

Sehemu ya kwanza ambayo inatakiwa kuongezwa nguvu ni safu ya ulinzi, ambapo mtandao wa Daily Mail ulithibitisha mapema Jumanne ya wiki hii kuwa dili la Michael Keane, mwenye thamani ya pauni milioni 25 linaweza kufanyika.

Keane, ambaye aliuzwa na Louis van Gaal kwa pauni milioni mbili tu, anafanya vizuri Burnley, ambao hadi sasa wameshajihakikishia kubaki Ligi Kuu England. Hadi kufikia sasa, Keane, mwenye umri wa miaka 24, anasifiwa kuwa mmoja wa mabeki walioonesha kazi nzuri msimu huu, ambaye huenda akaifanya safu ya ulinzi ya United kuwa na nguvu mpya msimu ujao.

Ili kuhakikisha safu ya ulinzi inatimia, United inaweza kujikuta ikilazimika kufanya uhamisho wa mlinda mlango mwingine kutokana na tetesi zinazodai David de Gea huenda akatimka, ambapo klabu ya Real Madrid imeendelea kutajwa kuwa katikati ya tetesi hizo. Kumbuka walimkosa ‘kiduchu’ tu miaka miwili iliyopita.

Sasa basi, kutokana na tetesi hizo za De Gea, kipa wa Atletico Madrid, Jan Oblak, atafaa kurithi glovu zake, lakini United italazimika kumgharamia zaidi ambapo ili kuuvunja mkataba wake na Atletico, itabidi pauni milioni 85 zitolewe, na kama hiyo haitoshi, wakala wa kipa huyo aliripotiwa kukwea pipa hadi England kwa ajili ya mazungumzo na United mwishoni mwa mwezi uliopita.

Pia imeripotiwa kuwa, De Gea hana furaha kutokana na maamuzi ya kocha wake, Jose Mourinho, kutomwanzisha katika mechi za Ligi ya Europa na kama United itashindwa kunyakua taji la michuano hiyo, ni wazi kipa huyo hatakuwa na sababu ya kuendelea kubaki OT.

Ni ukweli usiopingika kuwa, United haitakubali haraka kumuuza kipa huyo, ikizingatiwa kila mwaka msimu wa Ligi Kuu England unazidi kuwa mgumu na michuano ni mingi, hivyo kama Madrid itazidi kugonga hodi OT, inatakiwa kuja na fedha za kutosha.

Takribani miezi 18 sasa, ishu ya Antoine Griezmann kutakiwa na miamba hao wa OT imekuwa wazi, ambapo straika huyo hatari wa Atletico anaongoza kwenye orodha ya mastaa wanaotakiwa na Mourinho.

United pia inamtolea jicho kiungo mshambuliaji wa Real Madrid asiye na raha ndani ya ‘pepo’, James Rodriguez. Hembu subiri…kumbe United imeshawashiwa taa ya kijani kumsajili nahodha huyo wa Colombia, lakini kuna ripoti zinazodai kuwa, timu hiyo huenda ‘ikampotezea’ na kufuatilia kwingine.

Mwanzoni mwa makala haya, nafasi ya beki wa kati iligusiwa, lakini safu ya kiungo pia inahitaji nguvu mpya. Na kiungo mrefu na mwenye nguvu wa Monaco, Tiemoue Bakayoko, ndilo chaguo sahihi la Mourinho, hata hivyo, mabingwa wa Ligi Kuu England, Chelsea, wanatajwa kumfukuzia Mfaransa huyo.

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

Klabu zamiminika kuomba kutumia U/Nelson Mandela

NA ASHA KIGUNDULA UONGOZI wa Chama cha Soka Mkoa wa Rukwa (RUREFA), umesema umeanza...

Kipa mpya Azam atamba kumsaulisha Abarola

NA ZAINAB IDDY KIPA mpya wa Azam, David Kissu, ameuahidi uongozi na mashabiki wa timu hiyo kuwa atajituma na...

Yanga: Hatuna mpango na wasugua benchi Msimbazi

NA ZAINAB IDDY UONGOZI wa Yanga, umesema hauna mpango wa kusajili wachezaji wanasugua benchi katika klabu ya Simba kwa...

TSHISHIMBI KUMFUATA MORRISON SIMBA

NA ZAINAB IDDY KIUNGO wa Yanga, raia wa DR Congo, Papy Tshishimbi, anatarajiwa kumfuata winga wa kikosi hicho, Bernard...

TSHISHIMBI KUMFUATA MORRISON SIMBA

NA ZAINAB IDDY KIUNGO wa Yanga, raia wa DR Congo, Papy Tshishimbi, anatarajiwa kumfuata winga wa kikosi hicho, Bernard...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -