Thursday, December 3, 2020

Manchester yaziburuza Madrid, Barca kwa umaarufu duniani

Must Read

HUJUMA NZITO YANGA

NA WINFRIDA MTOI UONGOZI wa Yanga upo katika harakati za kuhamishia mechi zao zilizobaki...

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika...

MANCHESTER, England

HAKUNA Real Madrid, Barcelona wala Bayern Munich, Man United ndiyo klabu maarufu zaidi duniani na takwimu hizo ni kutokana na mauzo ya jezi.

Takwimu zimeonesha kuwa Man United wana wastani wa kuuza jezi milioni 1.75 kwa mwaka na hiyo ni kuanzia mwaka 2011 na mwaka 2016.

Utafiti huo umefanywa na wataalamu wa idara ya masoko ambayo ilikuwa ikiongozwa na Dk. Peter Rohlmann.

Mafanikio hayo yametokana na mkataba ambao Man United walisaini na kampuni ya kutengeneza vifaa vya michezo ya Adidas mwaka jana ambao unatajwa kuwa na thamani ya pauni milioni 75.

Baada ya Man United, Madrid wanaonolewa na kocha Mfaransa Zinedine Zidane wanashika nafasi ya pili wakiwa wameuza takribani jezi milioni 1.65.

Nafasi ya tatu imetua kwa Barc (milioni 1.27), huku nafasi ya nne ikitua kwa wababe wa soka la Ujerumani, Bayern Munich ambao mauzo yao ya jezi yanatajwa kufikia milioni 1.2.

Klabu nyingine zilizoingia kumi bora ni Chelsea iliyouza jezi 899,000, Liverpool (852,000), Arsenal (835,000) na PSG (526,000).

Nyingine ni Juventus (452,000) huku wakali Borussia Dortmund wakikamilisha idadi ya kumi bora kwa mauzo yao ya jezi 393,000.

Kwa mujibu wa utafiti huo, mastaa wa Man United, Paul Pogba na Zlatan Ibrahimovic ndio walioshika nafasi ya kwanza na ya pili kwenye orodha ya wanasoka ambao jezi zao zimenunuliwa kwa wingi.

Lakini pia, chipukizi Marcus Rashford na mlinda mlango wa Old Trafford, David De Gea, nao waliingia kumi bora.

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

HUJUMA NZITO YANGA

NA WINFRIDA MTOI UONGOZI wa Yanga upo katika harakati za kuhamishia mechi zao zilizobaki...

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul 'Ben Pol' ameshukuru mashabiki kwa...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania...

DEWJI: CHAMA NI SIMBA HADI 2022

Kiungo huyo raia wa Zambia, aliyetoa mchangomkubwakwaSimbakufikisharobo fainaliyaLigiyaMabingwaAfrikamsimuwa 2018/19, ikiwamo kutwaa ubingwa wa LigiKuuTanzaniaBarakwa misimumitatu mfululizo, awali ilidaiwa alikuwa yupo katika hatuayamwishoyakujiunganaYanga.

Sven aruka kihunzi

NA ASHA KIGUNDULA KOCHA Mkuu wa Simba, Sven Vandenbroeck, ameruka kihunzi na kuwaachia msala nyota wake, Clatous Chama na...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -