Sunday, November 1, 2020

MANCINI: SINA UCHAWI

Must Read

Hamilton avunja rekodi Ureno

LISBON, Ureno STAA wa mbio za magari Lewis Hamilton, amevunja rekodi ya Valtteri...

Ronaldinho naye ana Corona

RIO, Brazil MKONGWE wa Brazil, Ronaldinho, amethibitishwa ana virusi vya corona. Ronaldinho aliandika...

Sterling amlilia kinda wao Man City

MANCHESTER, England WINGA wa Manchester City, Raheem Sterling, ameandika ujumbe wa majonzi baada ya...

ROMA, Italia

KOCHA Roberto Mancini amewataka mashabiki wa timu ya Taifa ya Italia kuwa na subira kwa kile alichodai kuwa hawezi kufanya miujiza kama mchawi wakati akiimarisha timu.

Italia juzi ilimaliza mkosi wa kutoka uwanjani katika michezo mitano bila ushindi, baada ya kuichapa Poland bao  1-0  katika michuano ya timu za Taifa na hivyo kufufua matumaini ya kusonga mbele.

Alikuwa ni staa Cristiano Biraghi ambaye aliipatia Italia bao la ushindi dakika za mwisho, baada ya kikosi hicho kuonekana kingeondoka na pointi moja licha ya kutawala mchezo huo.

Mancini alionekana kufurahishwa na kiwango cha timu na akasema kwamba walistahili pointi zote tatu, lakini akasema kwamba bado anahitaji kutuliza hasira za mashabiki.

“Tumeutawala mchezo,” Mancini  aliuambia mtandao wa Rai Sport.

“Tungeweza kufunga mabao mapema na tusingekuwa sahihi kama mechi ingemalizika kwa matokeo ya 0-0 kwani kila mchezaji amejituma na tunafahamu itatuchukua muda lakini ushindi huu ni mzuri,” aliongeza kocha huyo.

Alisema kwamba, wanaweza kuimarika zaidi, lakini jambo hilo ni lazima linahitaji subira.

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

Hamilton avunja rekodi Ureno

LISBON, Ureno STAA wa mbio za magari Lewis Hamilton, amevunja rekodi ya Valtteri...

Ronaldinho naye ana Corona

RIO, Brazil MKONGWE wa Brazil, Ronaldinho, amethibitishwa ana virusi vya corona. Ronaldinho aliandika ujumbe kupitia ukurasa wake wa...

Sterling amlilia kinda wao Man City

MANCHESTER, England WINGA wa Manchester City, Raheem Sterling, ameandika ujumbe wa majonzi baada ya kinda wa zamani wa timu...

Afua Suleiman afunguka ‘Utalijua Jiji’ ilivyompa ustaa mjini

NA JEREMIA ERNEST JINA alilopewa na wazazi wake ni Afua Suleiman na hata alipojitupa kwenye ulimwengu wa muziki wa...

Keche: Kundi maarufu Ghana linalowatamani Diamond, Kiba, Harmonize

JIACHIE na Staa Wako, wiki hii tumetua mpaka Accra, Ghana kwa kundi maarufu la muziki nchini humo, Keche linofanya vizuri na ngoma...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -