Friday, November 27, 2020

MANJI KUIREJESHA YANGA KILELENI

Must Read

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika...

DEWJI: CHAMA NI SIMBA HADI 2022

Kiungo huyo raia wa Zambia, aliyetoa mchangomkubwakwaSimbakufikisharobo fainaliyaLigiyaMabingwaAfrikamsimuwa 2018/19, ikiwamo kutwaa ubingwa wa LigiKuuTanzaniaBarakwa misimumitatu mfululizo, awali...

NA KULWA MZEE

WAKATI Yanga inajiandaa kushiriki michuano ya Kombe la Shirikisho, Jamhuri imekana kwa kiapo kwamba hawamshikilii mwenyekiti wa klabu hiyo, Yusuph Manji.

Hayo yalidaiwa jana Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam mbele ya Jaji Ama–Isario Munisi, wakati maombi ya Manji ya kutaka aachiwe kizuizini kwa sababu anashikiliwa isivyo halali yalipotaka kuanza kusikilizwa.

Mahakama Kuu ilipokea maombi kutoka kwa mawakili wa Manji, Hudson Ndusyepo, Alex Mgongolwa na Jeremiah Ntobesya, wakidai mteja wao anashikiliwa kinyume cha sheria katika Hospitali ya Aga Khan ambako amelazwa, hivyo wanaiomba mahakama imwachie huru.

“Mheshimiwa Jaji, Manji analindwa na polisi sita, tunaomba tupewe muda wa kujibu majibu ya kiapo kinzani na iwekwe kwenye kumbukumbu za mahakama kwamba hashikiliwi kama wanavyodai Jamhuri.

“Sisi hatuwezi kuwa wendawazimu tulete maombi mahakamani kuomba aachiwe kizuizini wakati hajashikiliwa,” alidai Mgongolwa.

Wakili wa Serikali Mkuu, Osward Tibabyekomya, jana aliwasilisha majibu ya kiapo kinzani kuhusiana na maombi hayo.

Hii inaweza kuwa habari njema kwa Yanga ambayo inajiandaa kushiriki michuano ya Kombe la Shirikisho Afrika baada ya kuondolewa Ligi ya Mabingwa Afrika na timu ya Zanaco ya Zambia, pia katika jitihada zake ya kutetea ubingwa wa Ligi Kuu msimu huu.

Klabu hiyo kwa sasa inakabiliwa na ukata wa fedha za kujiendesha tangu  Manji ambaye ndiye amekuwa akiisapoti kifedha alipofikishwa katika Mahakama ya Kisutu jijini Dar es Salaam, akikabiliwa na tuhuma za kutumia dawa za kulenya.

Yanga iliondolewa katika michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika kwa faida ya bao ya ugenini kufuatia sare ya bao 1-1 kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salam, kisha suluhu ya 0-0 jijini Lusaka.

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania...

DEWJI: CHAMA NI SIMBA HADI 2022

Kiungo huyo raia wa Zambia, aliyetoa mchangomkubwakwaSimbakufikisharobo fainaliyaLigiyaMabingwaAfrikamsimuwa 2018/19, ikiwamo kutwaa ubingwa wa LigiKuuTanzaniaBarakwa misimumitatu mfululizo, awali ilidaiwa alikuwa yupo katika hatuayamwishoyakujiunganaYanga.

Sven aruka kihunzi

NA ASHA KIGUNDULA KOCHA Mkuu wa Simba, Sven Vandenbroeck, ameruka kihunzi na kuwaachia msala nyota wake, Clatous Chama na...

Sarpong ‘aua’ shabiki Simba

Na MWANDISHI WETU, MWANZA BAO la dakika ya 29 lililofungwa na Michael Sarpong wa Yanga juzi, limesababisha kifo cha...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -