Wednesday, October 21, 2020

MANULA AWAACHIA UBINGWA SIMBA NA YANGA

Must Read

Director Kenny: Harmonize alinipeleka WCB nikafanya video ya Lavalava

MWONGOZAJI bora wa video nchini, Kenned Sanga a.k.a Derector Kenny kutoka Zoom Extra, ametua   hapa Jiachie na...

Rogers mwanamuziki anayevutiwa na Marijani

NA JEREMIA ERNEST BONGO Star Search (BSS), ni shindano lililofanikiwa kuibua vipaji vingi vya...

Ihefu, Azam patachimbika Sokoine, Katwila ndani

NA ASHA KIGUNDULATIMU ya Ihefu inatarajia kushuka uwanjani kucheza na Azam ukiwa ni mchezo wa Ligi Kuu...

NA WINFRIDA MTOI

LICHA ya kuibuka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Simba katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara uliochezwa juzi kwenye Uwanja wa Uhuru, jijini Dar es Salaam, kipa wa Azam, Aishi Manula, amesema kwenye mbio za ubingwa hawamo kutokana na kuanza vibaya msimu huu.

Akizungumza na BINGWA, Manula alisema timu yake kuchukua ubingwa msimu huu, labda itokee miujiza ya Mwenyezi Mungu, kwani wenye nafasi ya kulitwaa taji hilo ni Simba na Yanga.

Manula alisema wamewaachia Simba na Yanga katika harakati za kuwania ubingwa wa msimu kutokana na tofauti ya pointi nyingi dhidi yao.

Alisema mzunguko wa pili wa ligi hiyo ni mgumu kwao kwani mechi zilizosalia  ni chache za kuweza kushinda na kuwa katika hesabu za kuchukua ubingwa.

Manula alisema hawezi kutabiri Yanga na Simba nani atachukua ubingwa,  lakini nafasi ipo kwa timu hizo mbili kutokana na pointi walizofikisha.

“Ni kweli kikosi chetu kiko vizuri kwa sasa  na leo (juzi) tumepata ushindi, lakini kuhusu suala la kuchukua ubingwa  kwa Azam labda itokee miujiza kwa sababu  pointi tulizoachwa na Simba na Yanga ni nyingi.

Manula alisema siri kubwa ya kikosi chao kuamka kwa sasa ni wachezaji kujituma na ushirikiano wa wachezaji tangu walipokuwa katika Kombe la Mapinduzi na wataendelea kupambana hadi mwisho wa ligi.

“Si  kama tumekata tamaa ya ubingwa ila ni kutokana na hali iliyopo ya ushindani, kila timu inapambana kutafuta matokeo mazuri.

Mfano mzuri timu tatu zilizopo juu ni Simba na Yanga na sisi tumeachwa kwa zaidi ya pointi 10,” alisema.

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

Director Kenny: Harmonize alinipeleka WCB nikafanya video ya Lavalava

MWONGOZAJI bora wa video nchini, Kenned Sanga a.k.a Derector Kenny kutoka Zoom Extra, ametua   hapa Jiachie na...

Rogers mwanamuziki anayevutiwa na Marijani

NA JEREMIA ERNEST BONGO Star Search (BSS), ni shindano lililofanikiwa kuibua vipaji vingi vya wanamuziki wa Tanzania ambao miongoni...

Ihefu, Azam patachimbika Sokoine, Katwila ndani

NA ASHA KIGUNDULATIMU ya Ihefu inatarajia kushuka uwanjani kucheza na Azam ukiwa ni mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara  (VPL), utakaochezwa leo...

Mugalu atema cheche Simba

NA ASHA KIGUNDULA MSHAMBULIAJI wa Simba, Chris Mugalu, amesema wanakwenda mkoani Rukwa kupambana na kupata ushindi katika mchezo wao...

Malale aitisha Yanga

NA ZAINAB IDDY KOCHA Mkuu wa timu ya Polisi Tanzania, Malale Hamsini, amezisikia sifa za kocha mpya wa Yanga,...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -