Tuesday, November 24, 2020

MANULA WA KWANZA YANGA

Must Read

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika...

DEWJI: CHAMA NI SIMBA HADI 2022

Kiungo huyo raia wa Zambia, aliyetoa mchangomkubwakwaSimbakufikisharobo fainaliyaLigiyaMabingwaAfrikamsimuwa 2018/19, ikiwamo kutwaa ubingwa wa LigiKuuTanzaniaBarakwa misimumitatu mfululizo, awali...

NA JESSCA NANGAWE

KIPA namba moja wa Azam, Aishi Manula, amesema yeye ni mchezaji na kwamba hana tofauti na mfanyakazi yeyote, hivyo yupo tayari kutua timu yoyote itakayoonyesha nia ya kumtaka, zikiwamo Yanga na Simba.

Manula, ambaye ni tegemeo kubwa kwa Azam, ameweza kuisaidia klabu yake hiyo kwa kiasi kikubwa, baada ya kudaka mfululizo bila kupumzika katika mechi za ligi kuu na za kimataifa.

Akizungumza na BINGWA, kipa huyo alisema licha ya kuendelea kuwa na mkataba na timu hiyo, lakini ifahamike kuwa yeye kama mchezaji ni sawa na mfanyakazi yeyote, kwa hiyo imani yake ni kuwa sehemu yoyote atakayopata ajira atafanya, haijalishi ni timu gani.

“Siwezi kuchagua timu, wakiniita Yanga, Simba au kwingine popote mimi nitakwenda kama tutafikia makubaliano, mpira kwangu ndio maisha yangu, ni lazima niangalie ni vipi nanufaika kwa maslahi yangu, ukiwa mchezaji ni kama mfanyakazi mwingine yeyote ambaye anaangalia zaidi wapi kuna maslahi zaidi,” alisema Manula.

Azam inatarajia kuwasili leo ikitokea Botswana, baada ya kuondolewa na wenyeji wao, Mbabane Swallows kwa jumla ya mabao 3-1.

Manula anatajwa kuwa kipa bora kabisa hapa nchini kwa sasa, akiwa pia ni tegemeo katika kikosi cha timu ya Taifa, Taifa Stars.

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania...

DEWJI: CHAMA NI SIMBA HADI 2022

Kiungo huyo raia wa Zambia, aliyetoa mchangomkubwakwaSimbakufikisharobo fainaliyaLigiyaMabingwaAfrikamsimuwa 2018/19, ikiwamo kutwaa ubingwa wa LigiKuuTanzaniaBarakwa misimumitatu mfululizo, awali ilidaiwa alikuwa yupo katika hatuayamwishoyakujiunganaYanga.

Sven aruka kihunzi

NA ASHA KIGUNDULA KOCHA Mkuu wa Simba, Sven Vandenbroeck, ameruka kihunzi na kuwaachia msala nyota wake, Clatous Chama na...

Sarpong ‘aua’ shabiki Simba

Na MWANDISHI WETU, MWANZA BAO la dakika ya 29 lililofungwa na Michael Sarpong wa Yanga juzi, limesababisha kifo cha...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -