Tuesday, November 24, 2020

MAONGEZI YA SIKU YA KWANZA YA MIADI YAKO

Must Read

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika...

DEWJI: CHAMA NI SIMBA HADI 2022

Kiungo huyo raia wa Zambia, aliyetoa mchangomkubwakwaSimbakufikisharobo fainaliyaLigiyaMabingwaAfrikamsimuwa 2018/19, ikiwamo kutwaa ubingwa wa LigiKuuTanzaniaBarakwa misimumitatu mfululizo, awali...

KWA wengi siku ya kwanza ya miadi ya kukutana na wale waliotaka kuwa wenza wao kulikuwa na hisia mbili zilizochanganyikana.

Hisia za furaha na ile ya woga kiasi

Hisia za furaha kwa ajili ya kukutana na watu wanaowapenda ila pia hisia za woga kiasi kutokana na kila mmoja kutokuwa na mazoea sana na mwenzake.

Ni vizuri kabla ya kutamka ya moyoni kwa yule uliyemkusudia, kukaa naye mahala na kuongea japo kwa saa moja tu.

Ni vizuri kufanya hivyo kwa sababu kila mmoja anapata fursa angalau kidogo ya kumsoma mwenzake. Katika hili unaweza pia kugundua walau tabia chache kutoka kwake na unaweza hata kujua uwezo wake wa kutafakari baadhi ya mambo na hali yake ya kujiamini ilivyo.

Ila kwa bahati mbaya wengi hawajui namna ya kuanza maongezi katika siku yao ya kwanza ya miadi. Wengi huishia kujisifu tu au kuwasifu wahusika kitu ambacho si sahihi sana.

Pia wapo baadhi pindi wakikutana tu, wao hukimbilia katika kuwaambia namna wanavyo wapenda. Kitu kinachowatisha wahusika na kuwaona kama watu wenye papara ya mambo.

Hapa leo nimekuandalia namna unavyotakiwa kufanya katika eneo husika la miadi ukiwa na mlengwa wako. Twende sasa.

ZUNGUMZA KUHUSU KAZI NA MALENGO

Baada ya salamu na maongezi kidogo ya kutia nakshi, anza kumuuliza kuhusu kazi au kitu chochote anachohusika nacho katika kipindi hicho. Wakati anaongea jitahidi kadiri uwezavyo kuyapa thamani mazungumzo yake kwa kusikiliza kwa utulivu na umakini. Hii itamfanya ajione kama anaongea na mtu mwenye kumthamini na kumjali.

Haipendezi na wala si vizuri hata kidogo wakati anaongea na wewe unafanya vitu vingine:- Kama kuchezea simu au kuonekana kama unatazama kitu kingine. Hapana haipaswi kuwa hivyo.

Utulivu na umakini wako utafanya pia azidi pia kuwa na hamu ya kuendelea kuongea na wewe kitu kitakachozidi kukupa wigo mpana wa kuendelea kumjua na kumsoma.

ONGELEA VITU VINAVYOVUMA KWA WAKATI HUO (Current issues)

Hii ni njia nyingine ya kuweza kumsoma na kuweza kuusoma vizuri ubongo wake. Katika hili using’ang’anie sana kuwa mzungumzaji mkuu muda wote, ila pia usimfanye ajihisi kazi yako ni kusikiliza tu, hapana.

Inafaa kuyapa chachu mazungumzo yenu kwa wote kuchangia kwa upana unaostahili. Ila hapa unaweza kuwa mjanja kidogo kwa kumwachia muda mrefu zaidi wa kuongea, lakini hapaswi kujua hivyo. Fanya hivi katika hali ya kimbinu ambayo unahisi hawezi kukushtukia.

Ukiweza kufanya hivi kwa usahihi atafurahia mazungumzo yenu na kila mmoja kupata fursa ya kumsoma mwenzake na kuuondoa ule woga na wasiwasi wa siku ya kwanza kukaa na kuzungumza naye.

KUMBUSHIA MAZUNGUMZO YALIYOPITA

Kwa kuwa unakutana naye katika mazingira ya namna hiyo kwa mara ya kwanza wakati mwingine unaweza kujikuta ghafla stori zinaisha. Likitokea jambo hilo, usihofu sana.

Unachotakiwa kufanya ni kukumbushia mazungumzo yenu mliyofanya katika simu.  Ongea naye bila papara wala hofu. Kumbuka kujiamini ni silaha kubwa unayotakiwa kuitumia ili kuweza kuyapa raha mazungumzo yenu.

Pia epuka kuuliza maswali mengi kama yupo katika mahojiano. Pendelea kutengeneza mazingira ya kimazungumzo si ya kuuliza ulizana tu. Ukiwa una maswali mengi kwake utamfanya kuchoka mapema mazungumzo na wewe. Tengeneza njia za mazungumzo kufanyika baina yenu.

Na ili uweze kupata mazungumzo uliza maswali yanayohitaji maelezo ya kina ambayo yatatoa fursa na kwa wote kuongea katika hali isiyo ya kimahojiano zaidi.

ULIZA KUHUSU FAMILIA YAKE

Ni kitu muhimu kwako kufanya.

Familia yake bila shaka ni lazima itakuwa ni kitu muhimu sana katika maisha yake, usidharau umuhimu huo.

Iulizie ili ajue ni kwa kiwango gani unavyomthamini yeye na nasaba yake. Pia katika kuiulizia utazidi kumjua zaidi ni mtu wa aina gani. Pia kumbuka kuwa makini ila bila kubabaika na kuonekana kama mtu uliyekariri maongezi.

Kuwa makini kwa kila hatua unayofanya kwake pamoja na kuwa mtulivu ili lengo la kumjua vizuri liweze kufikika. Pia unaweza kumuuliza aina ya vitu anayopenda kufanya au aina ya burudani anazopenda. Kama vile aina ya nyimbo anazopenda kusikiliza, aina ya filamu anazopenda kuangalia.

Pia unaweza kuuliza aina ya maeneo anayopenda kutembelea. Epuka kumchosha, wala usikae naye kwa muda mrefu sana kuzungumza naye. Tumia muda wa kawaida tu, kisha mwachane ili umuache akiwa na hamu na shauku kuu ya kutaka kukusikiliza tena.

Katika hili kuwa makini zaidi kwa maana kwa shauku ya wengi kutaka kuzungumza na wenza wao karibu kila siku ya mwanzo walijikuta wakiwachosha wenzao na kupoteza mvuto wa uwepo wao.

Umakini katika maongezi yako katika hii siku  ni muhimu sana maana hapo ndiyo unaweka thamani yako juu au unaiporomosha. Mbali na yote jua kwamba kujihami kwako ndiyo nguzo muhimu zaidi katika siku hii. Katika kujiamini huko ndiyo unaweza kuongea kwa ‘kurelaxy’ na kufanya mazungumzo baina yenu yazidi kupata nakshi na raha zaidi. Kwaleo hapa panatosha wapendwa. Tukutane tena siku nyingine.

ramadhanimasenga@yahoo.com

 

 

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania...

DEWJI: CHAMA NI SIMBA HADI 2022

Kiungo huyo raia wa Zambia, aliyetoa mchangomkubwakwaSimbakufikisharobo fainaliyaLigiyaMabingwaAfrikamsimuwa 2018/19, ikiwamo kutwaa ubingwa wa LigiKuuTanzaniaBarakwa misimumitatu mfululizo, awali ilidaiwa alikuwa yupo katika hatuayamwishoyakujiunganaYanga.

Sven aruka kihunzi

NA ASHA KIGUNDULA KOCHA Mkuu wa Simba, Sven Vandenbroeck, ameruka kihunzi na kuwaachia msala nyota wake, Clatous Chama na...

Sarpong ‘aua’ shabiki Simba

Na MWANDISHI WETU, MWANZA BAO la dakika ya 29 lililofungwa na Michael Sarpong wa Yanga juzi, limesababisha kifo cha...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -