Friday, December 4, 2020

MAPENZI YAPO KWA AJILI YA FURAHA TU, HALI YAKO IKOJE?

Must Read

HUJUMA NZITO YANGA

NA WINFRIDA MTOI UONGOZI wa Yanga upo katika harakati za kuhamishia mechi zao zilizobaki...

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika...

MAPENZI yana mambo ya ajabu na wakati mwingine yanastajaabisha sana. Unakuta mtu yuko tayari kusafiri umbali mrefu, tena wakati mwingine katika mazingira hatarishi ili akamuone mpenzi wake.

Anakubali kuhatarisha maisha yake kwa sababu tu ya kumuona mpenzi wake. Kwake kumuona mpenzi wake ndipo anapata furaha, akimuona tu, anavyocheka, anavyoongea, nafsi yake inaridhika na kujiona ana vingi katika maisha hata kama  bado ana changamoto nyingi katika maisha.

Mapenzi yana uwezo wa kumfanya mtu akacheka kutwa nzima kwa sababu ndogo tu. Mapenzi yana uwezo wa kumnyima mtu furaha na amani kwa sababu inayoonekana ndogo tu.

Kwa mfano, ukihisi mpenzi wako anafanya mawasiliano ya siri na mtu wa jinsia tofauti na yake huwezi kuwa na amani. Hata kama mawasiliano hayo hayapelekei wao kufanya lolote baya, ila kitendo chake cha kuyafanya kuwa siri huleta maswali na viulizo vingi sana.

Utajiuliza; kama hakuna chochote kibaya kinachoendelea ni kwanini afanye siri? Utajiuliza kama hana mpango wowote wa kukufanyia kinyume ni kwanini hataki wewe ujue ni nani anawasiliana naye?

Wapenzi wanapaswa kujua kuwa ujanja ujanja katika mapenzi huua ladha ya mapenzi. Mtu yeyote akimuona mpenzi wake amekuwa mjanja mjanja, ameanza kutoeleweka, ameanza kuwa na visingizio na visababu vingi ajue anayeyusha furaha na amani ya mwenzake.

Furaha ya mapenzi hupatikana pale kunapokuwa na uwazi na ukweli. Kama mambo yako mengi unayafanya kuwa siri basi jua unaidumaza furaha na amani ya mwemzako. Ilipotajwa kuwa wana ndoa ni mwili mmoja ilimaanishwa kuwa ni wajibu wao kuchangia vitu vingi. Bila kuchangia vitu vingi, bila kila mmoja kujua ya siri ya mwenzake dhana ya mwili mmoja hukosa nguvu.

Ili uweze kupata furaha na amani katika mahusiano yako, jua ni wajibu wako kuhakikisha mwenzako ana furaha na amani. Usione anacheka ukaona ana furaha, wengine wanacheka kwa sababu kuna mengi wanayaficha. Mwangalie sura na matendo yake, je, sura yake inatoa tafsiri ya furaha na amani? Matendo yake ni yale yenye kufanywa na mtu mwenye furaha na amani?

Hakuna sababu ya kuwa katika mapenzi kama hamsababishiani raha na amani. Mapenzi yapo kwa ajili ya kumpunguzia mtu mzigo wa mawazo, huzuni na upweke. Kama ukiona badala ya mwenzako kupungukiwa huzuni na upweke, yeye ndiyo anazidi kuwa mnyonge baada ya kuwa na wewe fahamu unashindwa kutimiza majukumu yako ipasavyo.

Jukumu lako la kwanza kama mpenzi wake linapaswa kuwa ni kumpa furaha na amani kwa hali yoyote. Kama upo tu, mwenzako anaumia kwa sababu yako na unaonekana kutokujali, jua wewe ni janga na unashindwa kutambua vema majukumu yako.

Mpenzi wa kweli, yule mwenye kutambua majukumu yake na sababu ya kuwa katika mapenzi ni yule mwenye kuhakikisha mwenzake, hakosi kitu chochote anachoweza kumudu. Kama wewe unashindwa kumudu kumpa amani na furaha mwezako, ni nini basi jukumu unaloweza kumudu kwa mwenzako?

Mapenzi yanatakiwa kutawaliwa na furaha na amani. Mapenzi yanatakiwa kujengwa katika misingi ya raha thamani na kujaliana. Ni ujuha kusema fulani ni mpenzi wako wakati kila siku unasababisha majonzi na huzuni katika maisha yake.

Tambua, hakuna binadamu aliyezoea na mwenye kupenda karaha. Kama wewe unadhani mwenzako hawezi kukuacha hata kama unamfanyia visa na vituko eti kwa sababu anakupenda sana basi pole sana.

Hakuna binadamu mwenye uwezo wa kuvumilia mateso na hila katika kipindi chote cha maisha yake. Leo ataumia kwa sababu yako ila jua kesho na kesho kutwa ataangalia ni nani anaweza kupoza majeraha ya maumivu uliyomsababishia katika maisha yake.

 ramadhanimasenga@yahoo.com

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

HUJUMA NZITO YANGA

NA WINFRIDA MTOI UONGOZI wa Yanga upo katika harakati za kuhamishia mechi zao zilizobaki...

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul 'Ben Pol' ameshukuru mashabiki kwa...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania...

DEWJI: CHAMA NI SIMBA HADI 2022

Kiungo huyo raia wa Zambia, aliyetoa mchangomkubwakwaSimbakufikisharobo fainaliyaLigiyaMabingwaAfrikamsimuwa 2018/19, ikiwamo kutwaa ubingwa wa LigiKuuTanzaniaBarakwa misimumitatu mfululizo, awali ilidaiwa alikuwa yupo katika hatuayamwishoyakujiunganaYanga.

Sven aruka kihunzi

NA ASHA KIGUNDULA KOCHA Mkuu wa Simba, Sven Vandenbroeck, ameruka kihunzi na kuwaachia msala nyota wake, Clatous Chama na...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -