Monday, November 30, 2020

MAPYA YAIBUKA KWA ULIMWENGU

Must Read

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika...

DEWJI: CHAMA NI SIMBA HADI 2022

Kiungo huyo raia wa Zambia, aliyetoa mchangomkubwakwaSimbakufikisharobo fainaliyaLigiyaMabingwaAfrikamsimuwa 2018/19, ikiwamo kutwaa ubingwa wa LigiKuuTanzaniaBarakwa misimumitatu mfululizo, awali...

NA MWANDISHI WETU


BAADA ya kukaa takribani miezi miwili nchini, mapya yameibuka kwa mshambuliaji wa kimataifa, Thomas Ulimwengu, juu ya mkataba wake na TP Mazembe.

Taarifa za uhakika kutoka Congo zinasema kwamba, uongozi wa Mazembe uliamua kuachana na mchezaji huyo kutokana na kushindwa kuonyesha kiwango ambacho kilitarajiwa na mmiliki wa timu hiyo baada ya kuondoka kwa Mbwana Samatta.

Taarifa za awali zilidai kwamba mshambuliaji huyo alivunja mkataba na Mazembe kutokana na ofa nono aliyoipata barani Ulaya.

Tangu kurejea kwa Ulimwengu mengi yamezungumzwa, huku ikiripotiwa kwamba mchezaji huyo amepata ofa sehemu mbalimbali kwenye nchi za Ufaransa, Uholanzi, Sweden na nchi nyingine.

Chanzo chetu cha habari kilisema mara nyingi mmiliki wa Mazembe anakuwa makini sana kumuacha mchezaji akiwa katika kiwango cha hali ya juu, kwani anaamini atasaidia timu yake na kumweka sokoni.

“Bosi wa Mazembe ni mtu ambaye anaangalia zaidi suala la masilahi ya mchezaji pamoja na klabu yake, suala la Ulimwengu kutoongeza mkataba ni kutokana na kutokuwapo katika mipango yao, kwani laiti angekuwa katika kiwango kizuri wasingekubali aondoke,” alisema.

Chanzo hicho kilimtolea mfano Samatta ambaye alimaliza mkataba lakini Mazembe hawakutaka kumwachia na hatimaye walikaa meza moja na kujadili mkataba mpya na kumpa fungu kubwa.

Alisema kwa mfano huo Ulimwengu alishindwa kutumia fursa ya kuonyesha kiwango cha hali ya juu na kuweza kumshawishi mmiliki huyo kumwongeza mkataba mpya.

Wakati huo huo, meneja wa mchezaji huyo, Jamal Kisongo, alisema kwamba  wamepokea ofa nyingi kutoka nchi mbalimbali ambapo ndani ya Januari hii huenda akapata timu na kuondoka nchini.

“Suala la Ulimwengu linaendelea, tumepokea ofa kutoka klabu mbalimbali ikiwamo Al Alhy ya Misri hivyo ndani ya Januari hii kila kitu kitakuwa sawa,” alisema Kasongo.

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania...

DEWJI: CHAMA NI SIMBA HADI 2022

Kiungo huyo raia wa Zambia, aliyetoa mchangomkubwakwaSimbakufikisharobo fainaliyaLigiyaMabingwaAfrikamsimuwa 2018/19, ikiwamo kutwaa ubingwa wa LigiKuuTanzaniaBarakwa misimumitatu mfululizo, awali ilidaiwa alikuwa yupo katika hatuayamwishoyakujiunganaYanga.

Sven aruka kihunzi

NA ASHA KIGUNDULA KOCHA Mkuu wa Simba, Sven Vandenbroeck, ameruka kihunzi na kuwaachia msala nyota wake, Clatous Chama na...

Sarpong ‘aua’ shabiki Simba

Na MWANDISHI WETU, MWANZA BAO la dakika ya 29 lililofungwa na Michael Sarpong wa Yanga juzi, limesababisha kifo cha...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -