Saturday, November 28, 2020

MARA GENK MIKONONI MWA MAN UNITED NUSU FAINALI

Must Read

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika...

DEWJI: CHAMA NI SIMBA HADI 2022

Kiungo huyo raia wa Zambia, aliyetoa mchangomkubwakwaSimbakufikisharobo fainaliyaLigiyaMabingwaAfrikamsimuwa 2018/19, ikiwamo kutwaa ubingwa wa LigiKuuTanzaniaBarakwa misimumitatu mfululizo, awali...

MANCHESTER, England


KAMA klabu anayochezea Mbwana Samatta, Genk itafanikiwa kushinda mechi yao ya Alhamisi hii dhidi ya Celta Vigo na Manchester United wamtoe Anderlecht mechi hizo za robo fainali, kutakuwa na uwezekano wa timu hizo kukutana kwenye hatua ya nusu fainali.

 

Anderlecht vs Man United

Klabu hiyo ya Red Devils imepangwa kukumbana na mabingwa wa Ubelgiji mara 33, Anderlecht. Hii itakuwa ni ratiba nzuri kwa Man United kuanza mechi yao ya kwanza ya robo fainali nchini Ubelgiji, Alhamisi hii na kocha wao, Jose Mourinho, atakuwa na furaha kupangwa na timu hiyo. Lakini Manchester United watakuwa na kazi kubwa ya kuongeza kiwango chao tofauti walivyocheza na Rostov ili kuepuka mechi ya pili kuwa ngumu. Iliwachukua dakika 70 hadi Juan Mata kuweza kutingisha nyavu za klabu hiyo kwenye Uwanja wa Old Trafford na kuitoa timu hiyo hatua ya mtoano kwa mabao 2-1.

Anderlecht waliitoa Apoel kwenye mechi za hatua ya mtoano, wakishinda mabao 1-0 kila mechi. Ambapo walimaliza wakiwa wa pili kwenye kundi lao nyuma ya Saint-Etienne.

 

Lyon vs Besiktas

Lyon wanapewa nafasi ya kunyakua taji hilo la Ligi ya Europa kwa msimu huu wa 2016/17, ambapo wao watacheza na Besiktas kwenye mechi ya robo fainali.  Huenda klabu hiyo ya Ligue 1 ikashinda mechi ya kwanza ya robo fainali, lakini watakuwa na kazi nzito nchini Uturuki. Besiktas wamepoteza mechi moja pekee kwenye uwanja wao wa Vodafone kwa msimu huu katika mechi zao 11 za Ligi ya Europa. Lyon watapaswa kushinda angalau bao moja kama si mawili ambayo yatawasaidia watakapokwenda mjini Istanbul kwa ajili ya mchezo wa marudiano.

 

Celta Vigo vs Genk

Celta Vigo ndio klabu pekee kwenye michuano hiyo na wamepanga kukutana na Genk kwenye mechi za robo fainali, mechi ya kwanza itapigwa nchini Hispania. Celta Vigo itakuwa timu ya sita kubeba taji la michuano hii ndani ya misimu minane na wataingia kwenye mechi hiyo wakiamini wataitoa klabu hiyo ya Ubelgiji. Genk waliwatoa Gent ambayo nayo ni ya Ubelgiji na kutinga robo fainali, wakifunga mabao matano ugenini kwenye mechi ya kwanza ya robo fainali kabla ya kutoka sare ya 1-1 kwenye mechi ya marudiano. Celta Vigo ambao wako nafasi za katikati ya msimamo wa ligi watakuwa na kazi ngumu kuonyesha ubora wao mbele ya Genk.

 

Ajax v Schalke

Robo fainali hii ya nne itaikutanisha miamba ya Uholanzi, Ajax na Ujerumani, Schalke. Ajax wana mechi kadhaa za ligi yao ya Eredivisie ambazo zitawapa picha halisi ya ubingwa wa nchi hiyo. Hivyo, itavutia kuona wapi wataegemea kabla ya mechi yao ya kwanza ya Ligi ya Europa itakayofanyika mjini Amsterdam au watazipigia hesabu zile za ligi hiyo ya Uholanzi na kupumzisha kikosi kwa ajili ya mechi zao kama ile dhidi ya Feyenoord.

Schalke wako katikati ya msimamo wa Bundesliga na njia pekee ya kushiriki ligi ya mabingwa msimu huu ni kunyakua taji hili. Kikosi hicho cha Markus Weinzierl kimefunga mabao mengi kwenye mechi za ugenini, ikiwemo matatu katika Uwanja wa PAOK na mawili dhidi ya Borussia Monchengladbach. Hivyo bila shaka watahakikisha wanatingisha nyavu za wapinzani wao kwenye Uwanja wa Amsterdam na kujiwekea uhakika wa kusonga mbele.

 

RATIBA

Alhamisi, Aprili 13, 2017

Anderlecht v Man Utd, saa 4:05 usiku 

Ajax v Schalke, saa 4:05 usiku

Lyonnais v Besiktas, saa 4:05 usiku  

Celta Vigo v Genk, saa 4:05 usiku    

 

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania...

DEWJI: CHAMA NI SIMBA HADI 2022

Kiungo huyo raia wa Zambia, aliyetoa mchangomkubwakwaSimbakufikisharobo fainaliyaLigiyaMabingwaAfrikamsimuwa 2018/19, ikiwamo kutwaa ubingwa wa LigiKuuTanzaniaBarakwa misimumitatu mfululizo, awali ilidaiwa alikuwa yupo katika hatuayamwishoyakujiunganaYanga.

Sven aruka kihunzi

NA ASHA KIGUNDULA KOCHA Mkuu wa Simba, Sven Vandenbroeck, ameruka kihunzi na kuwaachia msala nyota wake, Clatous Chama na...

Sarpong ‘aua’ shabiki Simba

Na MWANDISHI WETU, MWANZA BAO la dakika ya 29 lililofungwa na Michael Sarpong wa Yanga juzi, limesababisha kifo cha...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -