Monday, August 10, 2020

MARADONA ATAKA TIMU YAKE ISAFIRI KWA NDEGE BINAFSI

Must Read

Klabu zamiminika kuomba kutumia U/Nelson Mandela

NA ASHA KIGUNDULA UONGOZI wa Chama cha Soka Mkoa wa Rukwa (RUREFA), umesema umeanza...

Kipa mpya Azam atamba kumsaulisha Abarola

NA ZAINAB IDDY KIPA mpya wa Azam, David Kissu, ameuahidi uongozi na mashabiki wa...

Yanga: Hatuna mpango na wasugua benchi Msimbazi

NA ZAINAB IDDY UONGOZI wa Yanga, umesema hauna mpango wa kusajili wachezaji wanasugua benchi...

CULIACAN, Mexico


 

KOCHA mpya wa timu ya Dorados inayoshiriki Ligi Daraja la Pili nchini Mexico, Diego Maradona, ameanza mipango ya kuifanya klabu hiyo kuishi kifalme, akitaka usafiri uwe ni wa ndege binafsi katika kila mechi za ugenini.

Gwiji huyo wa soka wa Argentina alikubali kusaini mkataba wa miezi 11 ya kuinoa timu hiyo, ambayo kwa sasa inakamata nafasi ya 13 katika msimamo wa ligi hiyo ya daraja la pili nchini Mexico.

Katika mkataba huo, Maradona atakuwa anakusanya mshahara wa pauni 138,000 kwa mwezi na utaongezwa zaidi kama atafanikiwa kuipandisha daraja timu hiyo ingawa katika michezo sita ya ufunguzi wa ligi, Dorados haijashinda hata mmoja.

Lakini kwa mujibu wa vyanzo vya habari, kabla Maradona hajakubali kuinoa timu hiyo alisisitiza kwamba yeye na wachezaji wake watasafiri kwa kutumia ndege binafsi, badala ya mabasi na ndege za madaraja ya uchumi.

Pia klabu hiyo iliripotiwa kukubali suala la kukodi eneo la kifahari la makazi lililo na bwawa la kuogelea, ambalo lipo nje kidogo ya Jiji la Culiacan, karibu na uwanja wa mazoezi wa Dorados.

Maradona, ambaye aliwahi kuzichezea klabu za Barcelona na Napoli, kwa sasa anaishi katika hoteli ya nyota nne iitwayo Hotel Lucerna, sehemu ambako analindwa na ‘bodigadi’ kwa saa 24.

Ikumbukwe kuwa Maradona alitambulishwa kuwa kocha wa timu hiyo mapema wiki hii na alisema kwamba kazi yake hiyo mpya ni kama ‘amezaliwa upya’ baada ya kukabiliwa na vita ya kuachana na matumizi ya dawa za kulevya, ulevi na unene uliopitiliza

Alisema kwa sasa ana jukumu zito la kuisaidia Dorados na anaona ni sawa na kumbeba tembo kwenye mabega yake.

“Tutaingia uwanjani kujaribu kushinda mechi, maana mimi huwa sivutiwi na mchezo wa kujilinda,” alisema Maradona katika mkutano wake huo wa kwanza na waandishi wa habari.

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

Klabu zamiminika kuomba kutumia U/Nelson Mandela

NA ASHA KIGUNDULA UONGOZI wa Chama cha Soka Mkoa wa Rukwa (RUREFA), umesema umeanza...

Kipa mpya Azam atamba kumsaulisha Abarola

NA ZAINAB IDDY KIPA mpya wa Azam, David Kissu, ameuahidi uongozi na mashabiki wa timu hiyo kuwa atajituma na...

Yanga: Hatuna mpango na wasugua benchi Msimbazi

NA ZAINAB IDDY UONGOZI wa Yanga, umesema hauna mpango wa kusajili wachezaji wanasugua benchi katika klabu ya Simba kwa...

TSHISHIMBI KUMFUATA MORRISON SIMBA

NA ZAINAB IDDY KIUNGO wa Yanga, raia wa DR Congo, Papy Tshishimbi, anatarajiwa kumfuata winga wa kikosi hicho, Bernard...

TSHISHIMBI KUMFUATA MORRISON SIMBA

NA ZAINAB IDDY KIUNGO wa Yanga, raia wa DR Congo, Papy Tshishimbi, anatarajiwa kumfuata winga wa kikosi hicho, Bernard...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -