Tuesday, December 1, 2020

MARAPA WAPYA 5 WA KUTAZAMWA ZAIDI 2017

Must Read

HUJUMA NZITO YANGA

NA WINFRIDA MTOI UONGOZI wa Yanga upo katika harakati za kuhamishia mechi zao zilizobaki...

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika...

NA CHRISTOPHER MSEKENA

HONGERA kwa kuingia mwaka 2017, naamini hii ni nafasi nyingine ambayo Mungu amekupa ili utimize malengo yako uliyoshindwa kuyagusa mwaka uliopita. BINGWA tupo vyema na tayari kwa kukusogezea madini mengine ya burudani kwa mwaka huu.

Mwaka 2016 kuna vichwa vipya vingi vya Bongo Fleva tulivyoviona, uwapo wao umefanya muziki wetu uchangamke huku changamoto ikiwa kwa wasanii wakongwe. BINGWA leo tumeona si mbaya tufungue mwaka kwa kukusogezea marapa watano wapya ambao mwaka 2017 wanatazamwa kufanya vizuri.

Bill Nas

Ni rapa wa kisasa mwenye ladha na floo tamu pale unaposikiliza ngoma zake. Ana uandishi mzuri wa mashairi, anajua kunyumbulika, ana uwezo wa kulitawala jukwaa na kutoa burudani mujarabu kwa hadhira. Kama unamfuatilia Bill Nas basi utakuwa umenielewa.

Alianza kusikika kwenye Raha, wimbo aliyomshirikisha Nazizi, akaachia kazi nyingine inayoitwa Ligi Ndogo, Bill Nas alifunga mwaka 2016 na Chafu Pozi wimbo wenye mzuka wa aina yake huku Dayna Nyange akimtupia kwenye Komela unaofanya vyema kwa sasa.

Grafu ya muziki wake inapanda, endapo ataendelea kukaza basi mwaka 2017 atatusua zaidi kwenye ulimwengu wa rap.

Chemical

Mrembo huyu aliumaliza mwaka 2016 kwa stori ya kupendwa na rapa mwenzake Stereo. Tukirudi kwenye kazi, Claudia Lubao ‘Chemical’ ni miongoni mwa marapa wabunifu wanaojua kubadilika kulingana na mazingira kuanzia mwonekano mpaka kwenye muziki wao.

Ukimsikiliza kwenye ngoma zake kama vile Sielewi, Forever, Am Sorry Mama, Mary Mary na Kama Ipo Ipo Tu aliyomshirikisha Msaga Sugu, utabaini amewekeza zaidi kwenye ubunifu katika tungo hali kadhalika kwenye mwonekano wake, ndiyo rapa bora wa kike kwa sasa, tukimpa muda atakuwa bora zaidi mwaka huu.

Rosa ree

Kutoka kwenye lebo ya The Industry chini ya Navy Kenzo, tunakutana na Rosa Robert ‘Rosa ree’ anayefanya vizuri kwenye ulimwengu wa rap na ngoma yake mpya inayoitwa One Time.

Imezoeleka marapa wengi wa kike huwa wanajiweka kiume ili kujitofautisha na waimbaji ila kwa Rosa ree ni tofauti, ni mrembo anayependa mitindo, anavaa mavazi ya kike kama kawaida lakini hali hubadilika pale anapoanza kuchana kwani ana sauti fulani hivi yenye mamlaka na mistari myeusi isiyoakisi urembo wake.

Mwaka 2017 anapewa nafasi kubwa ya kufanya vizuri kufuatia kuwa chini ya uongozi bora pamoja na uwezo wake binafsi kama rapa.

Pink

Idadi ya marapa wa kike ni ndogo sana kwenye Bongo Fleva hivyo anapotokea binti mwenye umri mdogo na akaonyesha uwezo mkubwa wa kuandika mashairi, mwenye ‘swag’ za kipekee na floo kali ni lazima tumpe nafasi.

Pink alifanya vizuri mwaka jana na nyimbo kadhaa kama vile Ngoma na Sieleweki ambao ameishirikisha sauti ya Rais John Pombe Magufuli katika kiitikio. Ni ubunifu wa hali ya juu unaompa nafasi ya kufanya vyema zaidi mwaka huu.

Nchama The Best

Huyu ni mshindi wa shindano la Super Nyota mwaka 2016 akitokea jijini Mwanza, hivi sasa yupo kwenye mapumziko ya sikukuu na punde atarejea Dar es Salaam tayari kwa kuanza kuachia mikwaju yake.

Nchama ni rapa anayeweza kufanya mitindo huru yaani Free Style. Ana uwezo wa kuandika mistari na akazalisha ngoma kali, nilipata kuzungumza naye wiki iliyopita akanambia kuna kazi kadhaa amefanya na Mr. T Touch ambazo zitaanza kutoka mapema mwezi huu.

Namuona Nchama akiwa juu zaidi ya kina Ruby na Young Killer ambao nao waliibuliwa na shindano la Super Nyota linalofanyika kila mwaka wakati wa tamasha la Fiesta, mwaka huu Nchama atatazamwa kwa jicho la mafanikio zaidi.

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

HUJUMA NZITO YANGA

NA WINFRIDA MTOI UONGOZI wa Yanga upo katika harakati za kuhamishia mechi zao zilizobaki...

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul 'Ben Pol' ameshukuru mashabiki kwa...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania...

DEWJI: CHAMA NI SIMBA HADI 2022

Kiungo huyo raia wa Zambia, aliyetoa mchangomkubwakwaSimbakufikisharobo fainaliyaLigiyaMabingwaAfrikamsimuwa 2018/19, ikiwamo kutwaa ubingwa wa LigiKuuTanzaniaBarakwa misimumitatu mfululizo, awali ilidaiwa alikuwa yupo katika hatuayamwishoyakujiunganaYanga.

Sven aruka kihunzi

NA ASHA KIGUNDULA KOCHA Mkuu wa Simba, Sven Vandenbroeck, ameruka kihunzi na kuwaachia msala nyota wake, Clatous Chama na...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -