Monday, October 26, 2020

MARIANO DIAZ AWAZIA KUITWA KIKOSINI HISPANIA

Must Read

Boni Mwaitege amkalisha Mgogo

NA VALERY KIYUNGU KUPITIA shindano la Nani Zaidi linaloendeshwa na redio Passion Fm ya...

Mzuka warudi tena kwa s2kizzy

NA CHRISTOPHER MSEKENA SIKU chache baada ya kuvamiwa na kufanyiwa uharibifu wa studio zake...

The Yeamen waipiga ‘Shoti’

NA JEREMIA ERNEST MSANII kutoka kundi la The Yeamen, Suma Toto, amewaomba mashabiki wa...

MADRID, Hispania


 

STRAIKA wa Real Madrid, Mariano Diaz, amesema kwamba amepania kuhakikisha anaitwa kwenye kikosi cha timu ya Taifa ya Hispania ili aweze kuachana na ya Jamhuri ya Dominica.

Mariano, ambaye alirejea Real Madrid Agosti mwaka huu baada ya kutumia mwaka mmoja akiichezea Lyon, amewahi kuitumikia Jamhuri ya  Dominica katika mchezo mmoja wa kirafiki kutokana na kuwa mama mzazi wake anatokea katika taifa hilo.

Mchezo huo ni ule ambao waliondoka na ushindi wa mabao 3-1 dhidi ya Haiti  uliopigwa Machi 2013, hivyo ina maana kwamba uraia wake bado uko huru kutokana na kuwa hajaichezea timu hiyo mechi ya mashindano.

Mpaka sasa straika huyo mzaliwa wa Jiji la Barcelona, hajaichezea Real Madrid na hakuweza kufunga bao lolote katika michezo mitatu aliyocheza kwenye michuano ya Ligue 1 jambo ambalo lilimsababishia atoswe na kocha wa Hispania, Luis Enrique, katika michezo ya hivi karibuni dhidi ya England na  Croatia.

Hata hivyo, Mariano juzi alisema kwamba amepania kuhakikisha anaitwa katika kikosi hicho cha Hispania licha ya kupambana na Diego Costa, Iago Aspas  na Rodrigo Moreno.

“Ndio naliwaza hilo na kwa sababu ndoto zangu ni kuitwa na Luis Enrique,” alisema staa huyo alipohojiwa na waandishi wa habari kuhusu mipango yake.

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

Boni Mwaitege amkalisha Mgogo

NA VALERY KIYUNGU KUPITIA shindano la Nani Zaidi linaloendeshwa na redio Passion Fm ya...

Mzuka warudi tena kwa s2kizzy

NA CHRISTOPHER MSEKENA SIKU chache baada ya kuvamiwa na kufanyiwa uharibifu wa studio zake za Pluto Republic, prodyuza nyota...

The Yeamen waipiga ‘Shoti’

NA JEREMIA ERNEST MSANII kutoka kundi la The Yeamen, Suma Toto, amewaomba mashabiki wa Bongo Fleva kuendelea kulipa sapoti...

JB Maeba atimiza ndoto zake na Cannibal

NA CHRISTOPHER MSEKENA MSANII wa Afro Pop na Bongo Fleva anayeishi Kenya, James Tesha a.k.a JB Maeba, amesema anafurahi...

‘Certified Lover Boy’ ya Drake yaiva

TORONTO, CANADA RAPA nyota ulimwenguni, Aubrey Graham maarufu kama Drake, ametangaza habari njema ya ujio wa albamu yake ya...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -