Sunday, November 29, 2020

Mashabiki Mwanza waitabiria tabu Simba

Must Read

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika...

DEWJI: CHAMA NI SIMBA HADI 2022

Kiungo huyo raia wa Zambia, aliyetoa mchangomkubwakwaSimbakufikisharobo fainaliyaLigiyaMabingwaAfrikamsimuwa 2018/19, ikiwamo kutwaa ubingwa wa LigiKuuTanzaniaBarakwa misimumitatu mfululizo, awali...

NA MASYENENE DAMIAN,MWANZA

MASHABIKI wa soka jijini Mwanza, wameitabiria Simba kukwama katika harakati zao za kuzoa pointi zote sita watakapocheza michezo yao miwili na timu kutoka Kanda ya Ziwa.

Simba ambayo ipo Shinyanga, kesho itapambana na Mwadui FC katika mchezo uliopangwa kuchezwa Uwanja wa Kambarage na Jumatano ijayo kwenye uwanja huo huo wataikabili Stand United.

Kanda ya Ziwa imetoa timu tano msimu huu ambapo tayari Simba imeshazifunga Mbao FC, Toto Africans na Kagera Sugar michezo yote ikichezwa jijini Dar es Salaam.

Wakizungumza na BINGWA kwa nyakati tofauti, baadhi ya mashabiki wa soka wa Kanda ya Ziwa walisema uimara wa Simba ikiongozwa na mshambuliaji wao hatari, Shiza Kichuya, inatokana na mechi zao nyingi kuchezwa Dar es Salaam.

Walisema ujio wa Simba inayoongoza Ligi Kuu Bara ikiwa imejikusanyia pointi 29 baada ya kushuka dimbani mara 11, kunaweza kubadili matokeo na ubora wa timu hiyo.

Mmoja wa mashabiki hao, Hussein Kahishi, alisema ubora wa Simba kwasasa unatokana na kucheza mechi nyingi nyumbani hivyo wataanza kuonja joto la jiwe baada ya kuanza kucheza nje ya Dar es Salaam na kusisitiza ubora wa Simba utapimwa baada ya mechi za mikoani.

“Kule Dar es Salaam, Simba ina mashabiki na kila kitu lakini huku hali ni tofauti na mimi siioni Simba kama ni timu yenye ubora maana mchezo wake si kiwango cha juu kivile, Mbao tu alimtoa kamasi Dar es Salaam, sasa anakuja huku na anatarajia kucheza mechi nne na akijitahidi atatoka na pointi mbili tu labda za Mwadui na Toto lakini kwa Mbao na Stand ihesabu maumivu tu,” alisema.

Naye, Said Mohamed, alisema Simba imetangulia tu kwa sasa lakini hawatafika mbali kama watu wanavyofikiria kwa maana katika michezo yake ya nje ya Dar es Salaam, hataambulia alama yoyote huku akisema lazima wataacha pointi kwa Mbao, Toto Africans, Stand United na Mwadui.

Shabiki mwingine wa soka, Michael Ndichae, alisema Simba ni timu nzuri lakini mashabiki wa timu za Kanda ya Ziwa, wana imani timu zao hazitawaangusha na zitatoa upinzani mkali kwa Simba na kufanya mechi zake kuwa ngumu na zenye upinzani mkali.

Amrani Said alikua na mawazo tofauti akisema Kichuya na Muzamiru Yassin, wataipa Simba ushindi katika michezo yake mkoani Shinyanga akiongeza Wekundu hao wa Msimbazi wataendeleza makali yake Kanda ya Ziwa na kuubeba ubingwa wa Ligi Kuu Bara msimu huu.

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania...

DEWJI: CHAMA NI SIMBA HADI 2022

Kiungo huyo raia wa Zambia, aliyetoa mchangomkubwakwaSimbakufikisharobo fainaliyaLigiyaMabingwaAfrikamsimuwa 2018/19, ikiwamo kutwaa ubingwa wa LigiKuuTanzaniaBarakwa misimumitatu mfululizo, awali ilidaiwa alikuwa yupo katika hatuayamwishoyakujiunganaYanga.

Sven aruka kihunzi

NA ASHA KIGUNDULA KOCHA Mkuu wa Simba, Sven Vandenbroeck, ameruka kihunzi na kuwaachia msala nyota wake, Clatous Chama na...

Sarpong ‘aua’ shabiki Simba

Na MWANDISHI WETU, MWANZA BAO la dakika ya 29 lililofungwa na Michael Sarpong wa Yanga juzi, limesababisha kifo cha...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -