Tuesday, December 1, 2020

MASHABIKI WA CHILE WATAKA SANCHEZ AONDOKE ARSENAL

Must Read

HUJUMA NZITO YANGA

NA WINFRIDA MTOI UONGOZI wa Yanga upo katika harakati za kuhamishia mechi zao zilizobaki...

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika...

LONDON, England

MASHABIKI wa soka nchini Chile wamepanga kuandamana ili kulazimisha uhamisho wa nyota wao Alexis Sanchez, hawataki kuona akibaki Arsenal wakiamini inampa mzigo mkubwa.

Mashabiki hao waliwahi kugomea kuingia uwanjani kwa kitendo cha kocha Marcelo Bielsa kuondoshwa kwenye benchi la ufundi la timu yao ya Chile.

Walikataa kuingia uwanjani kuangalia mchezo ambao ulizikutanisha Chile na Uruguay na hata walioingia walivalia mavazi ya rangi nyeusi.

Mashabiki wa soka nchini humo wanataka kuona nyota wao huyo akiihama Arsenal na si kubaki Kaskazini mwa London. Madai ya mashabiki hao ni kwamba, Sanchez hapati sapoti ya wachezaji wenzake katika klabu ya Arsenal.

Kwa maana nyingine, hawataki kuona staa wao huyo akiendelea kutegewa na wachezaji wengine walioko Emirates.

Mashabiki wa Chile wametumia mtandao wa Facebook kuhamasisha maandamano hayo ambayo yamepangwa kufanyika Machi mosi, jijini Santiago, Chile.

Tayari watu 4,000 wameshathibitisha kushiriki maandamano hayo yaliyopachikwa jina la ‘Maandamano ya Taifa kutaka Alexis Sanchez atimke Arsenal’.

Tukio hilo linakuja ikiwa ni siku chache zimepita tangu Arsenal walipopokea kichapo cha mabao 5-1 na Bayern Munich katika mchezo wa kwanza wa hatua ya mtoano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya.

Katika mchezo huo uliochezwa jijini Munich, Ujerumani, bao pekee la Arsenal liliwekwa kimiani na Sanchez.

“Sisi tukiwa kama wananchi wa Chile, tumechoshwa kuona mchezaji wetu pekee akipambana kuisaidia timu,” ilisema taarifa ya mashabiki hao iliyowekwa Facebook.

“Si kwamba tunataka acheze Real Madrid au kurudi Barcelona, ila hatupendi pale anakocheza, tunataka kumuona akipambana sambamba na wachezaji wengine 10 kupata matokeo. Hastahili kucheza pekee yake.”

Mashabiki wa Chile wamejijengea umaarufu mkubwa katika ulimwengu wa soka hasa kwa vitendo vyao vya utovu wa nidhamu.

Itakumbukwa waliwahi kufanya vurugu kwenye Uwanja wa Maracanna wakati wa Fainali za Kombe la Dunia za mwaka 2014 na hiyo ilikuwa ni saa chache kabla ya timu yao kuvaana na Hispania.

Zaidi ya mashabiki 100 waliishia mikononi mwa polisi kwa tukio hilo lililosababisha uharibifu wa ukuta na rasiliamali nyingine za uwanjani hapo.

Mashabiki hao waliokuwa wamevalia nguo za rangi ya bendera ya Chile, walivunja vioo, ukuta na kupasua televisheni tatu zilizokuwa uwanjani, lengo likiwa ni kuingia bure kuitazama timu yao ikicheza na Hispania.

Shirikisho la Soka la Kimatafa (Fifa) lilitoa tamko likisema: “Kundi la watu wasiokuwa na tiketi walilazimisha kuingia uwanjani, walivunja ukuta na kuzidi nguvu ulinzi uliokuwapo.

“Walizuiwa na walinzi na hivyo hawakufanikiwa kukaa kwenye viti. Hali iliweza kuzuiliwa haraka na watu 85 walikamatwa, kwa mujibu wa taarifa ya Polisi wa Rio de Janeiro,” ilisema taarifa ya Fifa.

Mbali na kuifungia bao pekee dhidi ya Bayern, Sanchez ndiye anayeongoza kwa mabao katika mbio za kuwania kiatu cha dhahabu Ligi Kuu England akiwa ameziona nyavu za timu pinzani mara 17.

Wakiwa kwenye uwanja wa nyumbani wa Allianz Arena, vijana wa Carlo Ancelotti waliweza kuimaliza Arsenal kupitia mabao ya Arjen Robben, Thiago Alcantara aliyefunga mara mbili, Robert Lewandowski na Thomas Muller.

Arsenal watakuwa na kibarua kigumu kusonga mbele katika michuano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya, kwani watatakiwa kupata ushindi wa mabao 5-0 au zaidi katika mchezo wa marudiano utakaochezwa London, England.

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

HUJUMA NZITO YANGA

NA WINFRIDA MTOI UONGOZI wa Yanga upo katika harakati za kuhamishia mechi zao zilizobaki...

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul 'Ben Pol' ameshukuru mashabiki kwa...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania...

DEWJI: CHAMA NI SIMBA HADI 2022

Kiungo huyo raia wa Zambia, aliyetoa mchangomkubwakwaSimbakufikisharobo fainaliyaLigiyaMabingwaAfrikamsimuwa 2018/19, ikiwamo kutwaa ubingwa wa LigiKuuTanzaniaBarakwa misimumitatu mfululizo, awali ilidaiwa alikuwa yupo katika hatuayamwishoyakujiunganaYanga.

Sven aruka kihunzi

NA ASHA KIGUNDULA KOCHA Mkuu wa Simba, Sven Vandenbroeck, ameruka kihunzi na kuwaachia msala nyota wake, Clatous Chama na...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -