Tuesday, October 27, 2020

MASHABIKI WAMVAMIA MAVUGO DAR

Must Read

Keche: Kundi maarufu Ghana linalowatamani Diamond, Kiba, Harmonize

JIACHIE na Staa Wako, wiki hii tumetua mpaka Accra, Ghana kwa kundi maarufu la muziki nchini humo,...

Katwila: Sitaidharau Mbeya City

NA VICTORIA GODFREY KOCHA wa timu ya Ihefu, Zuberi Katwila, amesema hawaraidharau  Mbeya City...

Kocha apokea kipigo kwa shingo upande

 NA  VICTORIA GODFREY KOCHA wa timu ya Mwadui, Khalid Adam, amesema amesikitishwa na kipigo...

SALIM MPELI NA WINFRIDA MTOI

KUTOKANA na mashabiki wa Simba kutoridhishwa na kiwango cha mshambuliaji wao, Laudit Mavugo, ikiwa ni pamoja na kukosa mabao mengi hasa kwenye mechi za Ligi Kuu Tanzania Bara, waliamua kumvamia na kumweka kitimoto mshambuliaji huyo wa Burundi.

Mashabiki hao walimvaa mshambuliaji huyo wakati wa mazoezi ya timu hiyo ya Simba yaliyofanyika juzi kwenye Uwanja wa Boko Veterani nje kidogo ya Jiji la Dar es Salaam, wakijiandaa na mchezo wa ligi kuu dhidi ya Azam utakaochezwa kesho kwenye Uwanja wa Uhuru.

Wakati wachezaji wakiwa mazoezi, mashabiki hao waliingilia kazi ya kocha wao, Joseph Omog na kumvuta ‘chemba’ na kuanza kumpa mbinu za kupachika mabao mshambuliaji huyo.

Wengine walionekana kumpa  Mavugo ‘makavu live’ kutokana na kuchoshwa na utendaji wake uwanjani.

Katika mazoezi  hayo, Mavugo  alipiga mashuti makali lakini hayakulenga goli, kitu ambacho kiliwakera zaidi mashabiki wa timu hiyo na kuanza kupiga kelele wakimweleza jinsi ya kufunga.

“Wewe Mavugo angalia goli ukipata mpira si unapiga tu, mtu unapata nafasi nzuri na kupiga mashuti makali lakini hufungi,” walisikika mashabiki hao.

Naye meneja wa timu hiyo, Mussa Hassan ‘Mgosi’, alilazimika kujificha kuwakwepa mashabiki hao ambao siku ya kwanza ya mazoezi walimvaa wakitaka awaeleze sababu ya kasi ya timu hiyo kushuka.

Katika hatua nyingine, Omog ameendelea kuwafua washambuliaji wake ili waweze kufunga  kwa mashuti  ya mbali dhidi ya Azam.

Kocha huyo wa Simba raia wa Cameroon, alikuwa anataka kila mchezaji wake anapopata nafasi, ikiwa nje ya 18 anapiga shuti na si kusubiri kuingia ndani ya eneo la hatari.

Kwenye mazoezi hayo, Omog  aliwapanga wachezaji wake kwenye vikosi viwili waliokuwa wanacheza kama mechi na kuwataka kufanya kama anavyowaelekeza.

Akizungumzia mchezo wao wa keshokutwa, Omog  alisema anakiandaa kikosi kama kawaida na malengo yake ni kupata ushindi.

“Mechi yetu na Azam ni kama mechi nyingine, tunaendelea na mazoezi yetu ya kawaida,” alisema Omog.

Lakini Simba wakiendelea kujiwinda na mchezo huo, uongozi wa Azam umesema  watawafunga kwa staili waliotumia Kombe la Mapinduzi.

Simba ilifungwa na Azam bao 1-0 katika mchezo wa Fainali za Kombe la Mapinduzi uliochezwa Januari 13, mwaka huu kwenye Uwanja wa Amaan.

Mtendaji Mkuu wa Azam, Saad Kawemba, amesema timu yake imejipanga kuhakikisha wanaibuka na ushindi kwa kuwa wanaamini kikosi chao.

 

 

 

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

Keche: Kundi maarufu Ghana linalowatamani Diamond, Kiba, Harmonize

JIACHIE na Staa Wako, wiki hii tumetua mpaka Accra, Ghana kwa kundi maarufu la muziki nchini humo,...

Katwila: Sitaidharau Mbeya City

NA VICTORIA GODFREY KOCHA wa timu ya Ihefu, Zuberi Katwila, amesema hawaraidharau  Mbeya City katika mchezo wa Ligi Kuu...

Kocha apokea kipigo kwa shingo upande

 NA  VICTORIA GODFREY KOCHA wa timu ya Mwadui, Khalid Adam, amesema amesikitishwa na kipigo cha mabao 6-1 kutoka kwa...

KMC kumaliza hasira kwa Gwambina

NA WINFRIDA MTOI BAADA ya kuchezea kichapo cha mabao 2-1 kutoka kwa Yanga, kocha msaidizi wa timu ya Manispaa...

Tshishimbi atambulishwa kuvaa uzi wa AS Vita

NA MWENDISHI WETU KIUNGO wa zamani wa timu ya  Yanga, Papy Tshishimbi, ametambulishwa katika kikosi cha AS Vita ya...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -