Sunday, October 25, 2020

Mashabiki wataka Mourinho afukuzwe

Must Read

Fati aweka rekodi Barcelona

CATALUNYA, Hispania ANSU Fati ameweka rekodi ya mchezaji kinda wa kwanza kufunga mabao...

Lampard amshika mkono Silva

MANCHESTER, England KOCHA wa Chelsea, Frank Lampard, amesema atamtumia, Thiago Silva, katika mechi nyingi msimu huu licha ya...

Tuchel awatolea uvivu Mbappe, Neymar

PARIS, Ufaransa KOCHA wa PSG, Thomas Tuchel, amechukizwa na kiwango kibovu walichoonyesha mastaa wa timu hiyo, Kylian...

LONDON, England

HALI si shwari kwa kocha, Jose Mourinho, hasa baada ya mwenendo unaoonekana kutowaridhisha mashabiki wa klabu ya Manchester United.

Kwa lugha nyepesi na ya kueleweka, kocha huyo ameanza kukumbana na presha ya mashabiki ‘wendawazimu’ wa Old Trafford.

Baada ya Sir Alex Ferguson kutundika daluga, David Moyes, alikumbana na presha hiyo kama ilivyokuwa kwa Louis van Gaal ambaye kuondoka kwake kulimpa nafasi Mourinho.

Tayari mashabiki wa Man United wameanza kukinukisha baada ya kutuma ujumbe katika mitandao ya kijamii wakitaka kocha wao Mourinho atimuliwe kutokana na kipigo walichokipata mwishoni mwa wiki iliyopita kutoka kwa Watford.

Katika mchezo huo uliopigwa katika Uwanja wa Vicarage Road, Man Utd walichezea kichapo cha kushtukiza cha mabao 3-1.

Jahazi la vijana hao wa Old Trafford lilizamishwa na mabao ya Etienne Capoue, Juan Zuniga na Troy Deeney.

Bao pekee la kikosi hicho cha kocha Mreno, Mourinho, liliwekwa kimiani na kinda, Marcus Rashford.

Baada ya mtanange huo mashabiki walianza kutuma jumbe kupitia mtandao wa Twitter wakisema kuwa ni lazima Mourinho aondoke klabuni hapo kutokana na kipigo hicho ambacho ni cha tatu mfululizo.

Licha ya kuanza ligi vizuri, Mourinho alianza kupotea baada ya kuchapwa mabao 2-1 na Manchester City, akaambulia kipigo cha bao 1-0 kutoka kwa Feyenoord kabla ya kusambaratishwa tena katika mchezo wa wiki iliyopita.

Hata hivyo, kwa mujibu wa mtandao wa Daily Mail, taarifa za mashabiki kutaka Mourinho akimbizwe zilianza katikati ya wiki iliyopita baada ya timu hiyo kufungwa na  Feyenoord katika mchezo wa Ligi ya Europa.

Baadhi ya mashabiki waliuambia mtandao wa TalkSport kuwa wamechoshwa na mfululizo wa vipigo.

“Ni jambo la kusononesha kuona tunapoteza tena mechi ya pili muhimu, hatuwezi kuvumilia,” alisema mmoja wa mashabiki wa Old Trafford baada ya mchezo dhidi ya Feyennord.

Baada ya kipigo hicho, Jumamosi ya wiki iliyopita Mourinho alikuwa akitarajia kurejesha imani ya mashabiki wake lakini alijikuta akigonga mwamba mbele ya Watford waliokuwa kwenye uwanja wao wa nyumbani.

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

Fati aweka rekodi Barcelona

CATALUNYA, Hispania ANSU Fati ameweka rekodi ya mchezaji kinda wa kwanza kufunga mabao...

Lampard amshika mkono Silva

MANCHESTER, England KOCHA wa Chelsea, Frank Lampard, amesema atamtumia, Thiago Silva, katika mechi nyingi msimu huu licha ya kuwa na umri wa miaka...

Tuchel awatolea uvivu Mbappe, Neymar

PARIS, Ufaransa KOCHA wa PSG, Thomas Tuchel, amechukizwa na kiwango kibovu walichoonyesha mastaa wa timu hiyo, Kylian Mbappe na Neymar, kwenye mechi...

IBRA:Kifaa kipya Konde Gang aliyetembea kwa mguu kumwinda Harmonize

NA BRIGHITER MASAKI UKITAJA vijana wanaofanya vizuri katika mziki wa bongo fleva, huwezi kukosa kumtaja msanii chipukizi anayefahamika zaidi...

Jay-Z: Mama aliingilia bifu langu na Nas

-Z: Mama aliingilia bifu langu na Nas New York, Marekani HAKUNA shabiki wa Hip hop asiyelifahamu...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -