Monday, January 18, 2021

MASHINDANO YA U20, YABORESHWE ZAIDI MSIMU UJAO

Must Read

Usiyoyajua sare ya Leicester, United

NI katika mechi ya Ligi Kuu ya England iliyomalizika kwa sare ya mabaon 2-2.-Man United wamemiliki mpira...

Eti Zidane anapangiwa kikosi!

IMEFICHUKA kuwa wachezaji waandamizi wa Real Madrid walikaa kikao na Zinedine Zidane kumwambia wachezaji anaopaswa kuwapanga na...

DIDA ASAINI IHEFU FC

Golikipa wa zamani wa Yanga na Simba, Deogratius Munishi ‘Dida’ amejiunga na Timu ya Ihefu inayoshiliki Ligi...

NA LEONARD MANG’OHA

KATIKA jitihada za kuhakikisha mchezo wa soka nchini unapiga hatua, Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) lilianzisha mashindano ya ligi ya vijana chini ya miaka 20 chini ya klabu za Ligi Kuu Tanzania Bara.

Ni jambo linalostahili pongezi kwa TFF walau kwa kuweza kuandaa mashindano hayo yaliyofikia tamati hivi karibuni kwa timu ya vijana ya Simba kunyakua ubingwa wa mashindano hayo baada ya kuwafunga vijana wenzao wa Azam kwa mikwaju ya penalti.

Si mara ya kwanza kuwapo kwa mashindano ya namna hii, kwani hapo kabla yalikuwa yakifanyika katika mfumo wa ligi ambapo klabu za vijana zilikuwa zikicheza mechi ya utangulizi kabla ya mechi ya klabu zao vya ligi kuu kushuka dimbani.

Kwa wale waliobahatika kushuhudia vikosi B vya klabu za ligi kuu wakati ule, watakubaliana nami kuwa wachezaji wale hawakuwa wa klabu B za ligi kuu kutokana na kubadilika kwa kikosi kizima cha timu kila inapocheza na timu fulani hasa pale timu husika inapokuwa ikicheza mechi za ugenini.

Kutokana na klabu nyingi za ligi kuu kutokuwa na uchumi mzuri, zililazimika kutafuta wachezaji mikoani kila wanaposafiri nje ya viwanja vyao vya nyumbani wawatumie kama kikosi chao cha pili ili kuepuka gharama za kusafiri na vijana wao.

Ni wazi kuwa katika mfumo huo isingekuwa rahisi kwa timu kama Majimaji ambayo msimu huu imekuwa ikutembeza bakuli ili kupata fedha za kujiendesha kutokana na kuondokewa na wadhamini wao kabla ya kumpata mwingine aliyeokoa jahazi la wanalizombe lisizame, je, mfumo huu ungewezekana kwa Toto Africans? Si rahisi.

Matokeo yake sikumbuki mfumo huo uliisha kwa mtindo gani bali tulichoshuhudia ni kutoendelea kuchezwa kwa mechi za utangulizi za vijana kabla ya kaka zao kuingia uwanjani kulisakata kabumbu.

Baada ya kuona hilo limeshindikana na kwa kuzingatia maagizo ya Shirikisho la Soka la Kimataifa (FIFA), kuhusu kuendeleza soka la vijana mwaka huu baada ya ligi kuu kuwa katika mapumziko ya katikati ya msimu, TFF wakaanzisha ligi hiyo ya vijana iliyochezwa katika mfumo mashindano.

Timu zilipangwa katika hatua ya makundi kila timu ilicheza mechi saba kutokana na kuwapo kwa makundi mawili tu na kila moja likiwa na timu nane, ambapo timu mbili zilifuzu kwa hatua ya nusu fainali.

Ni wazi kuwa mashindano hayo yaliyodumu kwa muda usiozidi wiki tatu ni muda mfupi sana, ambao hauwezi kumjenga mchezaji na kumfanya kuwa mshindani kutokana na kucheza kwa muda mfupi.

Pamoja na kuendeshwa kwa muda mfupi mashindano hayo pia yaligubikwa na changamoto ya wachezaji kulalamikiwa kuwa na umri mkubwa kinyume cha kanuni za mashindano.

Kalimangonga Ongala ni Kocha Mkuu wa Majimaji ya Songea anasema tatizo ni kwamba, Watanzania tunapenda mambo ya mkato (haraka) ndiyo maana wachezaji hawaandaliwi kuanzia umri wa mdogo badala yake yanapoandaliwa mashindano ya vijana wachezaji wenye umri mkubwa hulazimika kudanganya umri ili wapate nafasi ya kushiriki.

Hivyo basi, naamini TFF imejifunza kitu katika michuano hii, ni bora imeanza na mapungufu yaliyoonekana ni vyema yakafanyiwa kazi katika michuano ijayo ili angalau mashindano haya yawe chachu ya kupata wachezaji kwenye timu za taifa za vijana zinazoendelea kuimarishwa hivi sasa.

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

Usiyoyajua sare ya Leicester, United

NI katika mechi ya Ligi Kuu ya England iliyomalizika kwa sare ya mabaon 2-2.-Man United wamemiliki mpira...

Eti Zidane anapangiwa kikosi!

IMEFICHUKA kuwa wachezaji waandamizi wa Real Madrid walikaa kikao na Zinedine Zidane kumwambia wachezaji anaopaswa kuwapanga na ndiyo maana timu hiyo imeshinda...

DIDA ASAINI IHEFU FC

Golikipa wa zamani wa Yanga na Simba, Deogratius Munishi ‘Dida’ amejiunga na Timu ya Ihefu inayoshiliki Ligi Kuu Tanzania Bara katika kipindi...

JDart Nation wapanga kutawala Africa

CHRISTOPHER MSEKENA MWANAMUZIKI na bosi wa JDart Nation, JDart, amesema miongoni mwa mipango yake kwa mwaka 2021 ni kuhakikisha...

HUJUMA NZITO YANGA

NA WINFRIDA MTOI UONGOZI wa Yanga upo katika harakati za kuhamishia mechi zao zilizobaki za Ligi Kuu Tanzania Bara...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -