Tuesday, October 20, 2020

MASHINE HIZI MSIMU HUU ZITASUMBUA SANA TU

Must Read

Director Kenny: Harmonize alinipeleka WCB nikafanya video ya Lavalava

MWONGOZAJI bora wa video nchini, Kenned Sanga a.k.a Derector Kenny kutoka Zoom Extra, ametua   hapa Jiachie na...

Rogers mwanamuziki anayevutiwa na Marijani

NA JEREMIA ERNEST BONGO Star Search (BSS), ni shindano lililofanikiwa kuibua vipaji vingi vya...

Ihefu, Azam patachimbika Sokoine, Katwila ndani

NA ASHA KIGUNDULATIMU ya Ihefu inatarajia kushuka uwanjani kucheza na Azam ukiwa ni mchezo wa Ligi Kuu...

LONDON, England


 

BAADA ya kumalizika fainali za Kombe la Dunia zilizofanyika mwaka huu nchini Urusi, ilishuhudiwa siku chache mashabiki wa soka kote duniani wakiendelea kupata burudani nyingine kwa kuanza ligi kubwa tano kubwa Ulaya.

Tangu ligi hizo zianze, tayari imeshashuhudiwa baadhi ya wachezaji nyota ambao wamerejea katika vikosi vyao wakiwa na viwango vya hali ya juu ambavyo vimeshazisaidia timu zao kujiweka katika mazingira mazuri ya kutwaa ubingwa.

Licha ya ukweli ni kwamba mwaka huu ulikuwa wa hekaheka kwa wachezaji ndani ya klabu na timu za taifa, lakini baadhi ya wachezaji wameendelea kukaa kwenye ubora wao na huku wengine waking’ara zaidi tofauti na misimu michache iliyopita.

Ifuatayo ni orodha ya wachezaji watano ambao wanaonekana msimu huu wanaweza wasikamatike kutokana na kasi yao ya upachikaji mabao katika mechi za kwanza msimu huu.

1 Lionel Messi

Licha ya kushindwa kufanya vizuri katika fainali za Kombe la Dunia zilizomalizika miezi michache nchini Urusi, hajamzuia nyota huyu wa  Lionel Messi  kuuanza vizuri msimu huu akiwa katika ubora wake.

Mpaka sasa staa huyo ameshafunga mabao manne na kutoa pasi zilizozaa mengine mawili katika mechi tatu alizokwishacheza katika michuano ya LaLiga msimu huu.

Mabao hayo ndiyo yameifanya Barcelona kuanza kuonekana kuwa tishio na kuiwezesha kujiweka katika hatua nzuri ya kutetea taji lake  la ligi hiyo ya Hispania.

2 Kylian Mbappe

Baada ya kufanya vizuri katika fainali za Kombe la Dunia na kuiwezesha nchi yake kutwaa ubingwa na huku akinyakua tuzo ya mchezaji bora mwenye umri mdogo, Mbappe amerejea katika michuano ya Ligi Kuu ya Ufaransa akiwa na makali yaleyale.

Kwa sasa straika huyo wa timu ya Paris Saint Germain, anaonekana kuwa tishio kwa mabeki wa timu pinzani katika ligi ya Ufaransa kutokana na umahiri wake wa kukokota mipira na kucheka na nyavu.

Kama ilivyo kwa Messi, staa huyo ameshaziona nyavu mara nne na kutoa pasi zilizozaa mengine mawili katika michezo mitatu aliyokwishacheza katika ligi hiyo ya Ufaransa na anavyoonekana ataendelea kuuwasha moto msimu wote mzima kama hatakumbwa na majeraha.

3 Sadio Mane

 Raia huyo wa  Senegal naye kama walivyo wenzake, Mohamed Salah  na Roberto Firmino, msimu huu anaonekana ataendelea kujijengea jina kwenye klabu hiyo ya Anfield kutokana na kiwango ambacho anakionesha katika mechi za kwanza akiwa na kikosi hicho cha   Jurgen Klopp.

Kwa sasa Reds ndio wapo kileleni mwa msimamo wa Ligi Kuu ya England ikiwa na pointi 12 na mabao  9  iliyoyapata katika michezo minne.

Kati ya mabao hayo, Sadio Mane ndiye aliyetoa mchango mkubwa kwa asilimia  44 baada ya kufunga manne katika michezo hiyo yote minne aliyokwishacheza.

4 Neymar Jr

Nyota huyo wa timu ya Taifa ya Brazil, alijikuta akiandamwa na mashabiki kutokana na uchezaji wake aliouonesha katika fainali za Kombe la Dunia zilizofanyika mwaka huu nchini Urusi.

Hata hivyo, kwa sasa straika huyo anaonekana kutotaka jambo hilo limtokee msimu huu, baada ya kuanza kwa kasi ya hali ya juu katika michuano ya Ligi Kuu ya Ufaransa akiwa na timu yake ya Paris Saint Germain na ameshaifungia mabao manne na kutoa pasi iliyozaa jingine moja katika michezo minne aliyokwishacheza.

Mabao hayo ndiyo yameisaidia PSG kukaa kileleni mwa msimamo wa Ligue 1.

5 Karim Benzema

Kwa jinsi inavyoonekana msimu huu, staa huyo wa Real Madrid ameamua kufuta makosa baada ya kushindwa kufanya vizuri kipindi cha miaka michache iliyopita.

Kama ilivyotarajiwa na wengi kuwa nyota huyo ndiye anayetakiwa kuibeba timu hiyo ya  Santiago Bernabeu baada ya kuondoka Cristiano Ronaldo, Mfaransa huyo anaonekana kulibeba vilivyo jukumu hilo.

Msimu huu tayari Benzema ameshafunga mabao  manne katika  michezo mitatu aliyokwishaichezea Los Blancos na kuifanya nayo iuanze vyema msimu huu wa  mpya wa  LaLiga.

Endapo ataendelea na kiwango hicho, inaweza kuwafanya mashabiki wa timu hiyo kumsahau  kwa haraka Ronaldo.

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

Director Kenny: Harmonize alinipeleka WCB nikafanya video ya Lavalava

MWONGOZAJI bora wa video nchini, Kenned Sanga a.k.a Derector Kenny kutoka Zoom Extra, ametua   hapa Jiachie na...

Rogers mwanamuziki anayevutiwa na Marijani

NA JEREMIA ERNEST BONGO Star Search (BSS), ni shindano lililofanikiwa kuibua vipaji vingi vya wanamuziki wa Tanzania ambao miongoni...

Ihefu, Azam patachimbika Sokoine, Katwila ndani

NA ASHA KIGUNDULATIMU ya Ihefu inatarajia kushuka uwanjani kucheza na Azam ukiwa ni mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara  (VPL), utakaochezwa leo...

Mugalu atema cheche Simba

NA ASHA KIGUNDULA MSHAMBULIAJI wa Simba, Chris Mugalu, amesema wanakwenda mkoani Rukwa kupambana na kupata ushindi katika mchezo wao...

Malale aitisha Yanga

NA ZAINAB IDDY KOCHA Mkuu wa timu ya Polisi Tanzania, Malale Hamsini, amezisikia sifa za kocha mpya wa Yanga,...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -