Wednesday, November 25, 2020

MASOGANGE APELEKWA KWA MKEMIA MKUU

Must Read

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika...

DEWJI: CHAMA NI SIMBA HADI 2022

Kiungo huyo raia wa Zambia, aliyetoa mchangomkubwakwaSimbakufikisharobo fainaliyaLigiyaMabingwaAfrikamsimuwa 2018/19, ikiwamo kutwaa ubingwa wa LigiKuuTanzaniaBarakwa misimumitatu mfululizo, awali...

Na HERIETH FAUSTINE

STAA wa kupamba video za muziki wa Bongo Fleva, Agnes  Gerald ‘Masogange’, amepelekwa kwa Mkemia Mkuu wa Serikali ili kupimwa damu kuweza kubaini kama ni mtumiaji wa dawa za kulevya.

Masogange mwenye umri wa miaka 25, alikamatwa na Jeshi la Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam kwa tuhuma za kujihusisha na kuuza, kusafirisha na kutumia dawa za kulevya.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana, Kamanda wa Kanda Maalumu, Kamishna Simon Sirro, alisema Masogange alipelekwa kwa Mkemia Mkuu jana ili kuchukuliwa vipimo vya damu kubaini kama anatumia mihadarati ili apelekwe mahakamani.

“Agness Masogange na wenzake 17, leo wamepelekwa kwa Mkemia Mkuu wa Serikali kuchukua damu ili kupimwa na kujua kama wanatumia dawa za kulevya ikiwa wanatumia kesho (leo) watapelekwa mahakamani.

“Upelelezi bado unaendelea, kumekua na kelele nyingi katika mitandao ya kijamii kuwa Masogange hakamatwi sasa amekamatwa na kupekuliwa na kuhojiwa pamoja na wengine 17, hivyo tukipata majibu ndio tutajua tuwapeleke mahakamani au kuwaachia kwa masharti ya kuwa chini ya uangalizi wa Jeshi la Polisi Kanda Maalumu wa Dar es Salaam,” alisema Kamishna Sirro.

Alisema habari ya kusema kwamba alikuwa karibu na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda, ni uvumi na uzushi ambao hauna maana.

 

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania...

DEWJI: CHAMA NI SIMBA HADI 2022

Kiungo huyo raia wa Zambia, aliyetoa mchangomkubwakwaSimbakufikisharobo fainaliyaLigiyaMabingwaAfrikamsimuwa 2018/19, ikiwamo kutwaa ubingwa wa LigiKuuTanzaniaBarakwa misimumitatu mfululizo, awali ilidaiwa alikuwa yupo katika hatuayamwishoyakujiunganaYanga.

Sven aruka kihunzi

NA ASHA KIGUNDULA KOCHA Mkuu wa Simba, Sven Vandenbroeck, ameruka kihunzi na kuwaachia msala nyota wake, Clatous Chama na...

Sarpong ‘aua’ shabiki Simba

Na MWANDISHI WETU, MWANZA BAO la dakika ya 29 lililofungwa na Michael Sarpong wa Yanga juzi, limesababisha kifo cha...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -