Saturday, November 28, 2020

MASOGANGE, WEMA WAKUTANA KISUTU

Must Read

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika...

DEWJI: CHAMA NI SIMBA HADI 2022

Kiungo huyo raia wa Zambia, aliyetoa mchangomkubwakwaSimbakufikisharobo fainaliyaLigiyaMabingwaAfrikamsimuwa 2018/19, ikiwamo kutwaa ubingwa wa LigiKuuTanzaniaBarakwa misimumitatu mfululizo, awali...

NA KULWA MZEE

MNYANGE wa Tanzania 2006 na msanii wa filamu, Wema Sepetu na video queen maarufu hapa nchini, Agnes Gerald maarufu Masogange, jana walikutana kwenye Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu katika kesi zinazowakabili.

Masogange (28), alifikishwa jana katika Mahakama hiyo akikabiliwa na mashtaka mawili ya kutumia dawa za kulevya aina ya heroin na oxazepam.

Wakati Masogange akikabiliwa na shtaka hilo, Wema alifika mahakamani hapo ambapo kesi yake na wenzake wawili ya kukutwa na kete moja ya bangi ilikuwa ikitajwa tena.

Akisoma mashtaka, mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Wilbroad Mashauri Wakili wa Serikali, Constantine Kakula, alidai Masogange alifanya makosa hayo chini ya kifungu cha 18 (a) cha sheria ya kupambana na dawa za kulevya namba 5 ya mwaka 2015.

Katika kesi hiyo namba 77 ya mwaka 2017, Masogange anadaiwa kati ya Februari 7 na 14, 2017 maeneo yasiyojulikana ndani ya Jiji la Dar es Salaam, alitumia dawa za kulevya aina ya heroin.

Inadaiwa kati ya Februari 7 na 14, 2017 alitumia dawa za kulevya aina ya Oxazepam.

Baada ya kusomewa mashtaka hayo, Masogange alikana na upande wa mashtaka ulidai kuwa upelelezi wa kesi hiyo haujakamilika.

Hakimu Mashauri alimtaka mshtakiwa huyo kuwa na wadhamini wawili wanaoaminika, kila mmoja asaini dhamana ya maandishi ya Sh milioni 10 na asitoke nje ya Dar es Salaam bila ya kuwa na kibali cha Mahakama.

Mshtakiwa alikamilisha masharti ya dhamana, kesi iliahirishwa hadi Machi 21, mwaka huu kwa ajili ya kutajwa.

Kwa upande wa Wema ambaye alifikishwa mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Thomas Simba, wakili Kakula alidai upelelezi wa kesi hiyo bado haujakamilika.

Kakula aliomba kesi iahirishwe na Hakimu Simba alikubali huahirisha kesi hiyo hadi Machi 15, mwaka huu kwa ajili ya kutajwa.

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania...

DEWJI: CHAMA NI SIMBA HADI 2022

Kiungo huyo raia wa Zambia, aliyetoa mchangomkubwakwaSimbakufikisharobo fainaliyaLigiyaMabingwaAfrikamsimuwa 2018/19, ikiwamo kutwaa ubingwa wa LigiKuuTanzaniaBarakwa misimumitatu mfululizo, awali ilidaiwa alikuwa yupo katika hatuayamwishoyakujiunganaYanga.

Sven aruka kihunzi

NA ASHA KIGUNDULA KOCHA Mkuu wa Simba, Sven Vandenbroeck, ameruka kihunzi na kuwaachia msala nyota wake, Clatous Chama na...

Sarpong ‘aua’ shabiki Simba

Na MWANDISHI WETU, MWANZA BAO la dakika ya 29 lililofungwa na Michael Sarpong wa Yanga juzi, limesababisha kifo cha...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -