Monday, October 26, 2020

MASTAA AMBAO MIZIMU YAO BADO INAZITESA KLABU ZAO

Must Read

Fati aweka rekodi Barcelona

CATALUNYA, Hispania ANSU Fati ameweka rekodi ya mchezaji kinda wa kwanza kufunga mabao...

Lampard amshika mkono Silva

MANCHESTER, England KOCHA wa Chelsea, Frank Lampard, amesema atamtumia, Thiago Silva, katika mechi nyingi msimu huu licha ya...

Tuchel awatolea uvivu Mbappe, Neymar

PARIS, Ufaransa KOCHA wa PSG, Thomas Tuchel, amechukizwa na kiwango kibovu walichoonyesha mastaa wa timu hiyo, Kylian...

LONDON, England


MICHUANO ya Ligi Kuu England inaendelea kushika kasi huku baadhi ya timu zikionekana kufanya vizuri kutokana na vikosi vyao kuwa imara.

Hata hivyo, pamoja na timu nyingine kufanya vizuri, zipo ambazo zinateswa na mizimu ya wachezaji wao ambao ziliwauza wakati wa usajili wa majira haya ya joto.

Ifuatayo ni orodha  ya wachezaji ambao hadi sasa mapengo yao yameshindwa kuzibika tangu walipouzwa wakati wa usajili huo.

N’Golo Kante (Leicester City)

Kuna sababu nyingi ambazo zinawafanya mabingwa wa Ligi Kuu England, Leicester City kufanya vibaya katika michuano hiyo.

Lakini moja ya sababu kubwa inayotajwa na baadhi ya wachambuzi wa masuala ya soka, ni kuondokewa na staa wao  ‘N’Golo Kante.

Licha ya Kante kutokabiliana na wapinzani ama kutibua mipira ya wapinzani kuliko mchezaji yeyote kwenye kikosi hicho cha Leicester City, lakini aliweza kufanya hivyo kuliko mchezaji yeyote wa ligi kuu baada ya kuzuia pasi za timu pinzani mara 31 na huku akiziingilia mara 15.

Huo unatajwa kuwa ulikuwa ni mchango mkubwa kwa Leicester City ambao kwa sasa wanaukosa.

 

Sadio Mane (Southampton)

Hapo chini ni orodha ya takwimu za  Sadio Mane kwa mujibu wa rekodi za Southampton kutoka katika mechi za ligi kuu alizocheza msimu uliopita, ikiwa ni baada ya miezi mitano tangu aondoke kwenye klabu hiyo.

Mabao ya kufunga: Alikuwa ni wa kwanza

Mashuti yaliyolenga lango- Alikuwa ni wa kwanza
Nafasi alizotengeneza-Alikuwa ni wa tatu
Pasi zilizozaa mabao –Alikuwa ni wa pili
Ukokotaji vizuri mpira –Alikuwa ni wa kwanza

Kutokana na  takwimu hizo, licha ya staa Nathan Redmond kuonekana anaweza kuvaa viatu vya Mane, lakini kwa jinsi hali ilivyo peke yake haviwezi  kutokana na kwamba hana uwezo kama alionao staa huyo hususan kucheka nyavu.

John Stones (Everton)

Kocha Ronald Koeman, alijaribu kuimarisha safu ya ulinzi ya Everton tangu siku ya kwanza aliyekuwa mtangulizi wake, Roberto Martinez aondoke.

Baada ya kuimarisha safu hiyo ilishuhudiwa kikosi hicho cha Koeman kikiruhusu bao moja ama chini ya hapo katika mechi 12 za ligi kuu sawa na asilimia  83 rekodi ambayo iliwahi kuwekwa na timu za Tottenham na  Manchester City pekee na msimu uliopita ikifanikiwa kufanya hivyo kwa asilimia  58.

Hata hivyo, mafanikio hayo yanaonekana yangeendelea kuwa mazuri zaidi kwa  Koeman kama staa wake, John Stones asingehamia  Manchester City.

Akiwa na wachezaji wengine kama Jose Fonte, Toby Alderweireld  na Virgil van Dijk, ambao wanajitahidi kuimarisha safu ya mabeki wa kati, lakini Mholanzi huyo anaonekana angefanya zaidi ya hapo akiwa na Stones.

Lakini kwa bahati mbaya fedha ndio kila kitu na ndio maana Stones na mapenzi yake aliyokuwa nayo kwa timu akaamua kuondoka.

 

Ashley Williams (Swansea City)
  Ashley Williams ni kati ya wachezaji waliocheza dakika nyingi katika timu hiyo ya Swansea City.

Katika matokeo ya takwimu zilizotolewa Machi 8 mwaka jana, Williams alicheza dakika 28, 252  za mechi za Swansea kati ya 28,980 tangu timu hiyo ilipopanda daraja mwaka 2008.

Wakiwa na beki huyo kisiki mabao waliyofungwa Swansea City katika ligi tangu walipopanda  daraja mpaka msimu wa 2013/14 ni 54, lakini msimu huu wanavyoonekana wapo njiani kupachikwa  69.

 

James Tomkins (West Ham)

Ukiangalia idadi ya wachezaji tofauti ambao West Ham imekuwa ikijaribu kuwatumia kwenye safu ya ulinzi wa kati, utabaini kwa kumuuza Tomkins  walifanya makosa makubwa.

Kwa sasa timu hiyo inawategemea wachezaji kama Winston Reid, Angelo Ogbonna, James Collins, Cheikhou Kouyate, Havard Nordveit, Reece Burke na  Reece Oxford lakini kikosi hicho cha  Slaven Bilic bado kinaonekana kupwaya katika eneo hilo.

Akiwa na timu hiyo, Tomkins aliweza kuanza kikosi cha kwanza katika mechi  20 ama zaidi kwa muda wa misimu mitatu.

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

Fati aweka rekodi Barcelona

CATALUNYA, Hispania ANSU Fati ameweka rekodi ya mchezaji kinda wa kwanza kufunga mabao...

Lampard amshika mkono Silva

MANCHESTER, England KOCHA wa Chelsea, Frank Lampard, amesema atamtumia, Thiago Silva, katika mechi nyingi msimu huu licha ya kuwa na umri wa miaka...

Tuchel awatolea uvivu Mbappe, Neymar

PARIS, Ufaransa KOCHA wa PSG, Thomas Tuchel, amechukizwa na kiwango kibovu walichoonyesha mastaa wa timu hiyo, Kylian Mbappe na Neymar, kwenye mechi...

IBRA:Kifaa kipya Konde Gang aliyetembea kwa mguu kumwinda Harmonize

NA BRIGHITER MASAKI UKITAJA vijana wanaofanya vizuri katika mziki wa bongo fleva, huwezi kukosa kumtaja msanii chipukizi anayefahamika zaidi...

Jay-Z: Mama aliingilia bifu langu na Nas

-Z: Mama aliingilia bifu langu na Nas New York, Marekani HAKUNA shabiki wa Hip hop asiyelifahamu...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -