Sunday, November 29, 2020

MASTAA DUNIANI WAIPA ‘BIG UP’ BARCA KWA MUUJIZA WAO

Must Read

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika...

DEWJI: CHAMA NI SIMBA HADI 2022

Kiungo huyo raia wa Zambia, aliyetoa mchangomkubwakwaSimbakufikisharobo fainaliyaLigiyaMabingwaAfrikamsimuwa 2018/19, ikiwamo kutwaa ubingwa wa LigiKuuTanzaniaBarakwa misimumitatu mfululizo, awali...

MANCHESTER, England

MAKOCHA na wachambuzi mbalimbali wa soka wamejitokeza kuimwagia sifa Barcelona kwa ushindi wao wa kushangaza wa mabao 6-1 walioupata juzi dhidi ya PSG.

Barca waliingia katika mchezo huo uliochezwa Camp Nou wakiwa na kumbukumbu ya kichapo cha mabao 4-0 katika mchezo wa kwanza, lakini juzi walishinda mabao 6-1 na kutinga hatua ya robo fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya kwa ushindi wa jumla ya mabao 6-5.

Kocha wa Manchester City, Pep Guardiola, alishindwa kuzuia hisia zake kwa muujiza huo ambapo alisema ulikuwa ni mchezo wa kushangaza katika ulimwengu wa soka.

“Ningependa kuwapongeza Barca, ni matokeo ya ajabu waliyopata usiku wa leo (juzi),” alisema Guardiola.

Naye Philip Neville aliyewahi kutamba Old Trafford ambaye sasa ni mchambuzi wa soka wa Sky Sports, alishangazwa na matokeo hayo ambapo alitumia ukurasa wake wa mtandao wa kijamii wa Twitter kuandika hivi: “Oh! Mungu wangu. Barcelona mmefanya nini?  Kesho (jana) kutakuwa na kazi ya ukocha pale PSG.”

Kupitia Twitter, Ilkay Guendogan aliandika hivi: “Ushindi wa Barca umenikumbusha mechi ya mwaka 2013 kati ya BVB (Borussia Dortmund) na Malaga! Ni ngumu kuamini! Hongera Barca @FC Barcelona.

Kocha wa West Ham, Slaven Bilic, amesema kilichofanywa na Barca ni somo kuwa hakuna kukata tamaa katika mchezo wa soka.

“Ni mchezo mkali ambao unaweza kuutumia kuzungumza na wachezaji wako. Si Barca pekee bali hata PSG. Ulikuwa ni mchezo wa ajabu.”

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania...

DEWJI: CHAMA NI SIMBA HADI 2022

Kiungo huyo raia wa Zambia, aliyetoa mchangomkubwakwaSimbakufikisharobo fainaliyaLigiyaMabingwaAfrikamsimuwa 2018/19, ikiwamo kutwaa ubingwa wa LigiKuuTanzaniaBarakwa misimumitatu mfululizo, awali ilidaiwa alikuwa yupo katika hatuayamwishoyakujiunganaYanga.

Sven aruka kihunzi

NA ASHA KIGUNDULA KOCHA Mkuu wa Simba, Sven Vandenbroeck, ameruka kihunzi na kuwaachia msala nyota wake, Clatous Chama na...

Sarpong ‘aua’ shabiki Simba

Na MWANDISHI WETU, MWANZA BAO la dakika ya 29 lililofungwa na Michael Sarpong wa Yanga juzi, limesababisha kifo cha...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -