Saturday, October 31, 2020

MASTAA HAWA HATUTAWAONA BOXING DAY LIGI KUU ENGLAND

Must Read

Hamilton avunja rekodi Ureno

LISBON, Ureno STAA wa mbio za magari Lewis Hamilton, amevunja rekodi ya Valtteri...

Ronaldinho naye ana Corona

RIO, Brazil MKONGWE wa Brazil, Ronaldinho, amethibitishwa ana virusi vya corona. Ronaldinho aliandika...

Sterling amlilia kinda wao Man City

MANCHESTER, England WINGA wa Manchester City, Raheem Sterling, ameandika ujumbe wa majonzi baada ya...

LONDON, England

KRISMASI ndio hiyo inatugongea hodi na kama historia ya soka la Ligi Kuu England isemavyo, ifikapo Desemba 26 burudani ya mechi za Ligi Kuu huendelea kwa mara nyingine.

Siku hiyo itakuwa maalumu kwa wale wachezaji ambao walipata nafasi ya kupumzika na familia zao wakisherehekea sikukuu hiyo maalumu duniani. Kiufupi watakuwa kwenye wakati mzuri.

Lakini kwa baadhi yao hawataweza kuonekana siku hiyo baada ya kuoneshwa kadi nyingine za njano wiki iliyopita ambazo zitawazuia kucheza ‘Boxing Day’.

Mchezaji muhimu zaidi atakayekosekana ni mshambuliaji hatari wa Chelsea, Diego Costa, ambaye amekuwa na wakati mzuri hadi sasa.

Costa alioneshwa kadi ya tano ya njano dhidi ya Crystal Palace na atakaa nje ya dimba dhidi ya Bournemouth pamoja na mchezaji mwenzake, N’Golo Kante.

Straika wa Leicester, Jamie Vardy, huenda akaukosa mchezo wa ligi dhidi ya Everton.

Vardy alioneshwa kadi nyekundu dhidi ya Stoke City lakini klabu yake imekata rufaa dhidi ya adhabu hiyo.

Manchester City itaendelea bila ya staa wao, Sergio Aguero, ambaye atakosekana katika mchezo wa mwisho katika adhabu ya kukaa nje ya uwanja kwa michezo minne.

Hii hapa orodha kamili ya wachezaji wa Ligi Kuu England ambao hawatacheza ‘Boxing Day’ kutokana na adhabu.

Burnley – Matthew Lowton

Chelsea – Diego Costa, N’Golo Kante

Leicester – Jamie Vardy, Christian Fuchs, Robert Huth.

Manchester City – Sergio Aguero

Stoke – Marko Arnautovic

West Ham – Pedro Obiang

 (Nathan Ake (Bournemouth) na Adnan Januzaj (Sunderland) wote hawataruhusiwa kucheza dhidi ya timu zao za zamani.)

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

Hamilton avunja rekodi Ureno

LISBON, Ureno STAA wa mbio za magari Lewis Hamilton, amevunja rekodi ya Valtteri...

Ronaldinho naye ana Corona

RIO, Brazil MKONGWE wa Brazil, Ronaldinho, amethibitishwa ana virusi vya corona. Ronaldinho aliandika ujumbe kupitia ukurasa wake wa...

Sterling amlilia kinda wao Man City

MANCHESTER, England WINGA wa Manchester City, Raheem Sterling, ameandika ujumbe wa majonzi baada ya kinda wa zamani wa timu...

Afua Suleiman afunguka ‘Utalijua Jiji’ ilivyompa ustaa mjini

NA JEREMIA ERNEST JINA alilopewa na wazazi wake ni Afua Suleiman na hata alipojitupa kwenye ulimwengu wa muziki wa...

Keche: Kundi maarufu Ghana linalowatamani Diamond, Kiba, Harmonize

JIACHIE na Staa Wako, wiki hii tumetua mpaka Accra, Ghana kwa kundi maarufu la muziki nchini humo, Keche linofanya vizuri na ngoma...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -