Tuesday, December 1, 2020

MASTAA HAWA KWA KUPIGA MIGUU YOTE UTAWAPENDA

Must Read

HUJUMA NZITO YANGA

NA WINFRIDA MTOI UONGOZI wa Yanga upo katika harakati za kuhamishia mechi zao zilizobaki...

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika...

LONDON, England

HAKUNA kitu kitamu kwenye soka kama mchezaji kuwa na uwezo wa kutumia miguu yote miwili kwa ufasaha.

Wapo wachezaji wa aina hiyo, tunaishi nao, kiufupi uwezo huo ni kama baraka tosha kwa mchezaji.

Kwanza, ifahamike kwamba hapa hazungumziwi mchezaji mwenye uwezo wa kupiga shuti kali na mguu wake wa kushoto kuliko mwingine, bali ni yule mwenye uwezo wa kufanya maajabu na miguu yote!

Miaka ya nyuma, Zinedine Zidane, Alessandro Del Piero na Pavel Nedved, waliweza kuzunguka pande za uwanja na usingeweza kuwaona wakishindwa kumiliki mpira na miguu yote hata katika ufungaji pia, kumbuka bao la Zidane kwenye fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya 2002 dhidi ya Bayer Leverkusen.

Hata hiyvo, si viungo na washambuliaji pekee wenye uwezo wa kutumia miguu yote kwa ufasaha bali wapo pia na mabeki waliobarikiwa ‘ufundi’ huo kama kitasa wa Juventus, Leonardo Bonucci ambaye kwa miaka ya hivi karibuni amedhihirisha uwezo wake huo hasa katika mfumo wa mabeki watatu.

Kwa maelezo hayo machache tu, hebu fikiria tu faida ya kuwa na mchezaji mwenye kutumia miguu miwili kwa ufasaha? Faida ya kwanza kubwa timu yako itakuwa na uwezo wa kuwania mataji kwani licha ya kwamba itakusanya wachezaji mahiri, kwa namna moja au nyingine uwezo wao huo hautokuwa sawa na mchezaji mwenye uwezo wa kupiga miguu yote kama mastaa hawa.

Santi Cazorla

Kiungo huyo Mhispania, anakubalika sana na wadau wa soka tangu alipotua kwenye Ligi Kuu England akitokea Villareal 2012.

Cazorla amedhihirisha kuwa yeye si bora tu ndani ya klabu ya Arsenal, bali ndani ya ligi kwa ujumla anatambulika vema kwa umahiri wake wa kuichezesha timu akiwa katikati ya dimba, ni rahisi kutambua mienendo yake uwanjani kutokana na ufupi wake huku akiwa na uwezo wa hali ya juu wa kukokota, kutoa pasi na krosi za uhakika, kupiga mashuti kwa kutumia miguu yote.

Cristiano Ronaldo

Hivi tungeanzaje kumsahau Ronaldo kwenye orodha hii? Isingekuwa rahisi kwa sababu mshindi huyo mara nne wa tuzo ya Ballon d’Or inayotolewa na jarida la France Football, ni sumu kwa safu yoyote ya ulinzi hasa linapokuja suala la kufumua mashuti ya mbali kwa kutumia mguu wowote.

Mguu wenye nguvu zaidi kwa Ronaldo ni ule wa kulia, lakini pia alifunga mabao tisa kwa mguu wake wa kushoto msimu uliopita wa La Liga.

Franck Ribery

Huyu jamaa anaweza kuwa hakubarikiwa kuwa na sura ya kuvutia, lakini ana zawadi ya kipekee ya kupiga miguu yote kwa ufasaha.

Hata hivyo, majeraha ya mara kwa mara yamekuwa ni ‘mchawi’ wa Ribery lakini pindi anaporudi dimbani, mabeki wa timu pinzani pale Bundesliga huingiwa na woga wakijua Mfaransa mwenye mbio, chenga za maudhi, mashuti makali kutoka mguu wowote amerudi kuwaadhibu.

Luka Modric

Tottenham Hotspur walitambua kabisa ni aina gani ya mchezaji waliyekuwa wakimpoteza pale ambapo kiungo wao wa zamani, Modric aliposaini Real Madrid mwaka 2012.

Alitabiriwa kuwa bora La Liga lakini hakuna aliyewahi kusema atakuwa bora kwa kiasi gani kama anavyoonekana hivi sasa dimbani.

Modric anaweza kuwa si mchezaji wa kuvutia sana ndani ya dimba la Bernabeu, kutokana na uwapo wa wachezaji ghali kama Ronaldo na Gareth Bale, lakini ukweli utabaki pale pale kuwa uwezo wa miguu miwili ya fundi huyu wa Croatia unaibeba mno Madrid.

Sergio Aguero

Staa huyu wa klabu ya Man City alifunga mabao 32 ndani ya michezo 40 msimu wa 2014/15, 26 kati ya mabao hayo aliyafunga katika Ligi Kuu England, 18 kwa mguu wa kulia na saba kwa mguu wa kushoto.

Mwaka uliofuatia, Muargentina huyo alipiga mabao 24 ya ligi lakini bado hapewi sifa anayostahili huku watu kama Harry Kane na Diego Costa ambao wanastahili sifa, wakisifiwa sana na Aguero akisahaulika. Tutajifunza lini?

Eden Hazard

Mshindi huyo wa tuzo ya PFA msimu wa 2014/15, ni bora mno hasa kwenye suala la ukokotaji wa mpira na kama ulikuwa hujui ana uwezo wa kukokota mpira bila hata kuuangalia mara mbili.

Ni wachezaji wachache wenye uwezo wa kutumia miguu miwili, lakini kukokota mpira bila kuutazama ni jambo moja gumu sana kwa wachezaji wengi.

Hazard hakuwa na wakati mzuri msimu uliopita hadi alipokuja kocha mpya ndani ya klabu ya Chelsea, Antonio Conte, mambo yanamwendea vizuri mno.

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

HUJUMA NZITO YANGA

NA WINFRIDA MTOI UONGOZI wa Yanga upo katika harakati za kuhamishia mechi zao zilizobaki...

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul 'Ben Pol' ameshukuru mashabiki kwa...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania...

DEWJI: CHAMA NI SIMBA HADI 2022

Kiungo huyo raia wa Zambia, aliyetoa mchangomkubwakwaSimbakufikisharobo fainaliyaLigiyaMabingwaAfrikamsimuwa 2018/19, ikiwamo kutwaa ubingwa wa LigiKuuTanzaniaBarakwa misimumitatu mfululizo, awali ilidaiwa alikuwa yupo katika hatuayamwishoyakujiunganaYanga.

Sven aruka kihunzi

NA ASHA KIGUNDULA KOCHA Mkuu wa Simba, Sven Vandenbroeck, ameruka kihunzi na kuwaachia msala nyota wake, Clatous Chama na...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -