Wednesday, October 28, 2020

MASTAA HAWA NA SIRI YA MAJINA YAO

Must Read

Hamilton avunja rekodi Ureno

LISBON, Ureno STAA wa mbio za magari Lewis Hamilton, amevunja rekodi ya Valtteri...

Ronaldinho naye ana Corona

RIO, Brazil MKONGWE wa Brazil, Ronaldinho, amethibitishwa ana virusi vya corona. Ronaldinho aliandika...

Sterling amlilia kinda wao Man City

MANCHESTER, England WINGA wa Manchester City, Raheem Sterling, ameandika ujumbe wa majonzi baada ya...

LOS ANGELES, Marekani

WASANII wengi wamekuwa wakiumiza vichwa kutafuta majina yenye swaga, yatakayokuwa nembo yao katika kazi zao za muziki.

Cha kufurahisha zaidi ni kwamba, imekuwa ikitokea mara kadhaa kwa jina la kisanii kuwa maarufu kuliko hata lile mwanamuziki alilopewa na familia yake.

Wafuatao ni wanamuziki ambao unaweza kushangazwa na jinsi walivyoyapata majina yao ambayo hivi sasa yanafahamika duniani kote.

50 Cent

Alipozaliwa miaka 41 iliyopita, wazazi wake walimuita Curtis Jackson.

Kabla ya kutoka kimuziki ambapo mapaka sasa umempa utajiri wa Dola milioni 15, alikuwa akimkubali sana mshikaji mmoja aliyekuwa staa wa hip hop, Kelven Darnell Martin.

Katika kazi zake, Kelven alikuwa akijiita ‘50 Cent’ na kwa kuwa huyu wa sasa alikuwa shabiki wake mkubwa, ndipo alipoamua kujipachika jina hilo.

Rick Ross

Jamaa anaitwa William Leonard Roberts II, lakini alijiita Rick Rose baada ya kuiba jina la aliyekuwa mfanyabiashara maarufu wa dawa za kulevya, Freeway Rick Ross.

Inadaiwa kuwa muuza ‘unga’ huyo alimfungulia mashitaka Rick Rose wa sasa, lakini hakufanikiwa kumfunga wala kulipwa fidia.

Wiz Khalifa

Kwa wanaomfahamu vizuri, wanamuita Cameron Jibril Thomaz. Kabla ya kuwa maarufu, alijiita Wisdom, akimaanisha ‘busara’.

Babu yake ambaye ni Muislamu ndiye aliyemuita Khalifa, jina la Kiarabu linalomaanisha ‘mwenye mafanikio’.

Akiwa na umri wa miaka 15, ndipo alipofupisha jina Wisdom na kupata ‘Wiz’ na kisha kuunganisha na Khalifa.

The Game

Sio jina analotumia kwenye nyaraka zake muhimu, ikiwamo hati ya kusafiria. Jina lake kamili ni Jayceon Terrell Taylor na alizaliwa Novemba 29, 1979.

Jina la The Game liliibuliwa na bibi yake. Kama ilivyo tafsiri ya Kiswahili ya neno ‘Game’ (mchezo), bibi huyo alimpachika mjukuu wake jina hilo kutokana na uwezo wake wa kucheza michezo mingi.

Akiwa ‘chalii’, mbali na soka, nyota huyo alikuwa moto wa kuotea mbali kwenye mchezo wa mpira wa kikapu.

Snoop Dogg

Ukiweka kando usanii wake, unaweza kumuita Calvin Cordozar Broadus. Akiwa mdogo, ndugu zake wlikuwa wakimfanananisha na muigizaji aitwaye Snoopy.

Jina hilo lilikua na hata alipoanza kuimba hakuona sababu ya kuliacha.

Jay Z

Jina la Jay Z lilitokana na aliyekuwa swahiba na mshauri wake ambaye alikuwa akiitwa Jay O.

Alichokifanya yeye ni kuondoa ‘O’ na kuweka ‘Z’.

Shuleni na hata kwenye shughuli nyingine rasmi, anaitwa Shawn Carter na alizaliwa mwaka 1969.

Tupac

Kama ilivyo kwa Rick Rose na 50 Cent ambao walichukua majina ya watu, hata Tupac alifanya hivyo.

Jina hilo la Tupac ni la kiongozi wa zamani wa Peru, Jose Gabriel Tupac Amaru.

Kiongozi huyo anakumbukwa nchini humo kutokana na juhudi zake za ukombozi.

Ushujaa huo ndio uliomfanya Tupac tunayemfahamu sisi kuchukua jina hilo, lakini yeye anaitwa Lesane Parish Crooks.

Drake

Mmoja kati ya wanamuziki ambao hawakupata tabu hata kidogo walipokuwa wakifikiria jina la kisanii, ni Drake.

Kwanza jamaa anaitwa Aubrey Drake Graham, alichokifanya ni kuchukua jina la kati, yaani la baba yake.

Wengi wanafikiri mshikaji ni raia wa Marekani, lakini ukweli ni kwamba ni Mcanada.

Eminem

Mmoja kati ya majina ya kibunifu ni hili la Eminem. Alianza kwa kuchukua ‘M’ mbili kutoka kwenye jina lake la Marshall Bruce Mathers na ndipo alipopata ‘M & M’.

Kama utachunguza kwa makini, utagundua kuwa ukitaja jina hilo, litasikika ‘Eminem’ na ndicho alichokifanya mshikaji huyo ambaye amekuwa mstari wa mbele kupinga ubaguzi wa rangi.

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

Hamilton avunja rekodi Ureno

LISBON, Ureno STAA wa mbio za magari Lewis Hamilton, amevunja rekodi ya Valtteri...

Ronaldinho naye ana Corona

RIO, Brazil MKONGWE wa Brazil, Ronaldinho, amethibitishwa ana virusi vya corona. Ronaldinho aliandika ujumbe kupitia ukurasa wake wa...

Sterling amlilia kinda wao Man City

MANCHESTER, England WINGA wa Manchester City, Raheem Sterling, ameandika ujumbe wa majonzi baada ya kinda wa zamani wa timu...

Afua Suleiman afunguka ‘Utalijua Jiji’ ilivyompa ustaa mjini

NA JEREMIA ERNEST JINA alilopewa na wazazi wake ni Afua Suleiman na hata alipojitupa kwenye ulimwengu wa muziki wa...

Keche: Kundi maarufu Ghana linalowatamani Diamond, Kiba, Harmonize

JIACHIE na Staa Wako, wiki hii tumetua mpaka Accra, Ghana kwa kundi maarufu la muziki nchini humo, Keche linofanya vizuri na ngoma...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -