Sunday, January 17, 2021

Mastaa hawa waliuza bangi, ‘unga’ kabla hawajatoka

Must Read

Usiyoyajua sare ya Leicester, United

NI katika mechi ya Ligi Kuu ya England iliyomalizika kwa sare ya mabaon 2-2.-Man United wamemiliki mpira...

Eti Zidane anapangiwa kikosi!

IMEFICHUKA kuwa wachezaji waandamizi wa Real Madrid walikaa kikao na Zinedine Zidane kumwambia wachezaji anaopaswa kuwapanga na...

DIDA ASAINI IHEFU FC

Golikipa wa zamani wa Yanga na Simba, Deogratius Munishi ‘Dida’ amejiunga na Timu ya Ihefu inayoshiliki Ligi...

LOS ANGELES, Marekani

NI watu wachache sana wanaoweza kutojiingiza kwenye njia haramu za kupata fedha wanapokuwa hoi kiuchumi.

Kwa kulitambua hilo, wapo wanaoamini kuwa umasikini ni chanzo cha maovu yote. Mtu ‘anapopigika’ ni rahisi kushawishika kujitosa katika uhalifu ili kuingiza kitu mfukoni.

Makala haya yanakuletea baadhi ya mastaa ambao kutokana na hali ngumu ya kimaisha kabla ‘hawajatusua’ walijitosa katika biashara ya uuzaji wa dawa za kulevya ‘unga’ ili kujikimu.

Snoop Dogg

Nyota huyo aliwahi kutajwa kuwa miongoni mwa wasanii wanaotumia kwa kiasi kikubwa kilevi aina ya bangi.

Rapa huyo alikiri kutumia kete 81 za bangi kwa siku.

Kwa mujibu wa Cameron Diaz ambaye alisoma na Snoop, nyota huyo aliuza bangi wakati wakiwa ‘skonga’.

Mwanadada Diaz alisema alikuwa mteja mkubwa wa Snoop.

“Alikuwa mrefu na mwembamba. Nina uhakika nilikuwa nikinunua bangi zake,” alisema Diaz.

Jay-Z

Kwa sasa mume huyo wa mwanadada, Beyonce Knowles, ana mpunga wa kufa mtu.

Miaka 25 iliyopita, alikuwa kwenye mitaa ya jijini Brooklyn akihangaika kuuza dawa za kulevya.

Alianza kuuza bangi na baadaye alipodunduliza kipato alijitosa katika ‘cocaine’.

Jay-Z amewahi kusema kuwa hata mama yake alilijua hilo lakini hakuwa na jinsi kutokana na hali ngumu ya kimaisha.

Hata hivyo, Jay-Z alisema licha ya kuuza ‘mizigo’ hiyo, hakuwahi kutumia.

Aliongeza kuwa kujiingiza katika uuzaji wa dawa hizo za kulevya kulimfanya kuwa na uwezo mkubwa wa kusimamia biashara ikiwemo kuweka na kusimamia bajeti.

T.I

Jina lake ni Clifford Joseph Harris Jr, lakini mashabiki wake wanamfahamu kwa jina la T.I.

Alikuwa muuzaji wa dawa za kulevya katika mitaa ya Jiji la Atlanta na kipindi hicho alikuwa na umri wa miaka 14.

Licha ya umri wake mdogo, alijitosa katika biashara hiyo na mara kadhaa alijikuta mikononi mwa polisi.

Alidai kuwa uuzaji wa dawa za kulevya ulimwezesha kujiingizia kipato ikiwemo kumlea mama yake.

Kwa sasa kutokana na shughuli zake za muziki, rapa huyo anatajwa kuwa na utajiri wa Dola za Marekani milioni 50.

50-Cent

Ngoma iliyomtoa staa huyu ni “Wanksta” ya mwaka 2002.

Mwaka mmoja baadaye alitoa albamu yake ya kwanza iliyoitwa ‘Get Rich or Die Tryin’ ambayo ilitikisa vilivyo na kuvunja rekodi ya mauzo.

Anamiliki lebo yake ya muziki inayotajwa kuigharimu Dola za Marekani milioni 150.

Alikulia Kusini mwa Jamaica na mara kadhaa alijichanganya na makundi ya wahuni.

Wakati anazaliwa, mama yake aitwaye Sabrina Jackson, alikuwa na umri wa miaka 15.

Ili kujikimu, Sabrina hakusita kuingia katika biashara ya dawa za kulevya.

Sabrina alikuwa miongoni mwa wauzaji unga waliojijengea umaarufu mkubwa nchini Jamaica.

Mwanamama huyo aliuawa wakati 50 Cent akiwa na umri wa miaka nane.

Alipokuwa na umri wa miaka 12, ndipo 50 Cent alipofuata nyayo za mama yake na kujitosa rsmi katika biashara hiyo ya dawa za kulevya.

Frank Ocean

Anatajwa kuwa miongoni mwa wanamuziki wakali nchini Marekani.

Alizaliwa California lakini alikulia New Orleans.

Alianza kuandika na kurekodi ‘singo’ akiwa sekondari.

Akiwa ‘A-Level’ hali ya kiuchumi ya familia yake ilikuwa mbaya na ndipo alipoanza kujiingizia katika biashara hiyo haramu.

Alitumia sehemu kubwa ya kipato chake kuingia studio na kurekodi ‘ngoma’.

Meek Mill

Mzaliwa huyo wa Philadelphia, alianza kupata umaarufu mwaka 2012 baada ya albamu yake ya kwanza iliyoitwa ‘Dreams and Nightmares’.

Albamu hiyo ilishika nafasi ya pili kwenye chati za Billboard na ilichukua muda mrefu kuporomoka.

Mwaka 2008, kabla hajatoboa, staa huyo alinaswa na mkono wa sheria kwa kosa la kufanya biashara ya dawa za kulevya na kumiliki silaha kinyume cha sheria.

Kutokana na kosa hilo, alitupwa rumande kwa miezi kadhaa.

Baadaye alihukumiwa tena kifungo cha miezi sita gerezani kwa kosa hilo.

 

Fat Joe

Jina lake halisi ni Joseph Cartagena.

Rapa huyo alijfunza mambo mengi kutoka kwa kaka yake aitwaye Angel, ikiwemo maisha ya mtaani.

Licha ya kuanza kuimba, lakini pia Fat Joe alikuwa akijiingizia kipato kutokana na biashara ya dawa za kulevya.

Inadaiwa kuwa kilichomfanya Fat Joe, kujiingizia kwenye biashara hiyo ni dhana aliyokuwa nayo kuwa ndio utamaduni wa hip-hop kwani wasanii wengi wa muziki huo walikuwa wakifanya hivyo.

Hata hivyo, kabla hajanogewa na biashara hiyo, ndipo alipoanza kuelekeza nguvu kubwa kwenye muziki na hatimaye akafanikiwa.

The Game

Wengi tulianza kumfahamu The Game mwaka 2003, baada ya kusainishwa na ‘prodyuza’ Dr. Dre katika lebo ya Aftermath Records.

Kabla ya hapo, aliwahi kufukuzwa shule baada ya kukutwa akiwa na dawa za kulevya.

Baada ya hapo alirejea ‘uswazi’ na kuanza kuuza dawa hizo huku akizunguka na wahuni.

 

Lil’ Kim

Si rahisi kuamini lakini ukweli ndio huo, Kim naye alikuwa katika maisha hayo ya kukimbizana na polisi kila siku.

Alifanya biashara ya dawa za kulevya kabla ya kipaji chake kuibuliwa na Notorious B.I.G.

Mmoja kati ya waliowahi kutoka naye kimapenzi ni Damion “World” Hardy ambaye alikuwa mfanyabiashara mkubwa wa dawa za kulevya.

Ingawa haijawahi kuangukia mikononi mwa polisi, Kim aliwahi kusema kuwa aliingia kwenye biashara hiyo ili kujiingizia kipato.

Busta-Rhymes

Jina alilopewa na wazazi wake ni Trevor George Smith, Jr ingawa Busta Rhymes ndilo lililojizolea umaarufu mkubwa.

Kabla ya ustaa alionao hivi sasa, Rhymes alikuwa akiishi na mama yake ambaye hata hivyo hakuwa na kipato kikubwa.

Katika kumsaidia ‘bi mkubwa’ wake huyo, mkali huyo alijitosa katika mishe za kuuza dawa za kulevya mtaani.

Lakini pia, Busta alikiri kuwa aliwahi ‘kukaba’ ili kujiingizia kipato.

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

Usiyoyajua sare ya Leicester, United

NI katika mechi ya Ligi Kuu ya England iliyomalizika kwa sare ya mabaon 2-2.-Man United wamemiliki mpira...

Eti Zidane anapangiwa kikosi!

IMEFICHUKA kuwa wachezaji waandamizi wa Real Madrid walikaa kikao na Zinedine Zidane kumwambia wachezaji anaopaswa kuwapanga na ndiyo maana timu hiyo imeshinda...

DIDA ASAINI IHEFU FC

Golikipa wa zamani wa Yanga na Simba, Deogratius Munishi ‘Dida’ amejiunga na Timu ya Ihefu inayoshiliki Ligi Kuu Tanzania Bara katika kipindi...

JDart Nation wapanga kutawala Africa

CHRISTOPHER MSEKENA MWANAMUZIKI na bosi wa JDart Nation, JDart, amesema miongoni mwa mipango yake kwa mwaka 2021 ni kuhakikisha...

HUJUMA NZITO YANGA

NA WINFRIDA MTOI UONGOZI wa Yanga upo katika harakati za kuhamishia mechi zao zilizobaki za Ligi Kuu Tanzania Bara...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -