Sunday, October 25, 2020

Mastaa hawa wanachukua mpunga mrefu pale Etihad

Must Read

Fati aweka rekodi Barcelona

CATALUNYA, Hispania ANSU Fati ameweka rekodi ya mchezaji kinda wa kwanza kufunga mabao...

Lampard amshika mkono Silva

MANCHESTER, England KOCHA wa Chelsea, Frank Lampard, amesema atamtumia, Thiago Silva, katika mechi nyingi msimu huu licha ya...

Tuchel awatolea uvivu Mbappe, Neymar

PARIS, Ufaransa KOCHA wa PSG, Thomas Tuchel, amechukizwa na kiwango kibovu walichoonyesha mastaa wa timu hiyo, Kylian...

MANCHESTER, England

WANASOKA ni miongoni mwa wanamichezo wanaoingiza fedha nyingi kutokana na kazi zao ndani na nje ya uwanja.

Mara nyingi vipato vyao nje ya uwanja hutegemea zaidi biashara ya matangazo.

Ndani ya uwanja chanzo kikubwa cha mapato ya wachezaji hutegemea zaidi mishahara yao ambayo hupokea kila wiki.

Katika msimu wa 2013-14, mabosi wa Man City walitumia kitita cha pauni milioni 216. Msimu uliopita matajiri hao wa Etihad walimwaga pauni milioni 193 kuwalipa mshahara wachezaji wake.

Hilo la usajili, Man City walitumia kitita cha pauni milioni 174 na kuwa timu yenye matanuzi makubwa kwenye soko la usajili kuliko zote za Ligi Kuu England.

Man City walijikuta wakitumbua kitita hicho kwa kuwasajili John Stones (pauni milioni 47.5), Leroy Sane (pauni milioni 36), Gabriel Jesus (pauni milioni 26), Ilkay Gundogan (pauni milioni 20), Nolito (pauni milioni 13), Claudio Bravo (pauni milioni 15), Marco Moreno (pauni milioni 4.6) na Geronimo Rulli (pauni milioni 4).

Baada ya kushika nafasi ya kwanza kwenye orodha ya timu zilizotumia fedha nyingi kwenye dirisha la usajili la majira haya ya kiangazi, ni wazi Man City watalazimika kuumia zaidi katika mshahara wa mastaa wa kikosi hicho.

Sergio Aguero/Yaya Toure

Bila shaka wanastahili kuwa vinara wa orodha ya wachezaji wanaolipwa vizuri na mabosi wa Etihad. Mastaa hao wanaweka mfukoni pauni 220,000 kwa wiki na hiyo ni kutokana na mikataba yao ya sasa klabuni hapo.

Mkataba wa Aguero na Man City utafikia tamati mwaka 2019 huku ule wa Yaya ukitajwa kuwa utakwisha mwakani. Aguero alitua Etihad mwaka 2011 akitokea Atletico Madrid na hata hivyo ada yake ya uhamisho haikutajwa na tangu hapo amekuwa silaha muhimu katika safu ya ushambuliaji.

Kwa upande wake, Yaya amekuwa katika wakati mgumu hasa baada ya ujio wa kocha Pe Guardiola ambaye ameonekana kutomkubali kivile.

Rahim Sterling

Staa huyo wa timu ya Taifa ya England alijiunga na Man City akitokea Liverpool na ada yake ya uhamisho ilikuwa ni pauni milioni 47.

Sterling anashika nafasi ya pili kwenye idadi ya mastaa wanaopokea mshahara mzuri pale Etihad.

Akaunti yake ya benki ina uhakika wa kuwekewa pauni 18,000 kila baada ya wiki moja.

Mkataba wake wa sasa wa miaka minne na wababe hao wa jijini Manchester utamalizika mwaka 2020.

David Silva

Kiungo huyo wa kimataifa wa Hispania anaweka mfukoni pauni 160,000 kwa wiki kutokana na mkataba wake wa sasa na Man City.

Silva ambaye alisajiliwa na Man City akitokea Valencia, amekuwa na msaada mkubwa kwa kiasi kikubwa kwa kikosi hicho. Man City ililazimika kutoa pauni milioni 24 kuipata huduma ya mkali huyo na ataendelea kuvuna mshahara huo wa pauni 160,000 mpaka mwaka 2019.

Kevin De Bruyne

Katika siku za hivi karibuni, Mjerumani huyo mwenye umri wa miaka 24 amekuwa kwenye kiwango cha hali ya juu hasa baada ya ujio wa kocha Pep Guardiola.

Kutokana na ubora wake uwanjani, De Bruyne anakinga pauni 150,000 kwa wiki na ataendelea kukunja kiasi hicho cha fedha mpaka pale mkataba wake wa miaka mitano utakapomalizika mwaka 2021.

Mshahara huo ni sawa na ule wanaopokea Samir Nasri aliyepelekwa  kwa mkopo Valencia na Ilkay Gundogan. Lakini pia, Vincent Kompany na Nicolas Otamendi wanachukua kiasi hicho cha fedha kila wiki.

Joe Hart

Mlinda mlango huyo mwenye umri wa miaka 27, amepelekwa mkopo katika klabu ya Torino ya Italia lakini bado Man City wanaendelea kumlipa pauni 110,000.

Hart bado ana mkataba na Man City ambao utafikia tamati mwaka 2019, hivyo mshahara huo mnono utaendelea kuingia kwenye akaunti yake.

Claudio Bravo

Mlinda mlango huyo ambaye amesajiliwa na Guardiola kuchukua nafasi ya Joe Hart, ana mkataba wa miaka minne utakaomalizika mwaka 2020 na anaweka mfukoni pauni 100,000 kwa wiki.

Lakini pia, ni kiasi hicho cha fedha ndicho anachopokea beki mpya aliyetokea Everton, John Stones na Mnigeria Kelechi Iheanacho mwenye mkataba wa miaka mitano.

Gael Clichy

Beki huyo wa zamani wa Arsenal ambaye hivi sasa ana umri wa miaka 29, anapokea kiasi cha pauni 90,000 na mkataba wake utafikia tamati mwaka 2017. Kwa mashahara huo, Clichy analingana na Pablo Zabaleta   mwenye umri wa miaka 30.

Mbali na hao, wachezaji wengine wanaopokea mshahara huo ni Fabian Delph, Fernandinho na Jesus Navas.

Aleksandar Kolarov

Mlinzi huyo wa pembeni raia wa Serbia ana uhakika wa kujiwekea mfukoni pauni 85,000 kila inapofika mwishoni mwa wiki.

Mkataba unaomfanya kuingiza kitita hicho kikubwa cha fedha utamalizika mwaka 2018 na huenda akapewa mwingine.

Bacary Sagna

Kama ilivyo kwa Clichy, Sagna naye ni raia wa Ufaransa na alitokea Arsenal kabla ya kujiunga na Man City.

Sagna mwenye umri wa miaka 32, anaingiza pauni 80,000 kwa wiki na ana mkataba wa mwaka mmoja wa kuendelea kuvuna kiasi hicho cha fedha.

Leroy Sane

Huyu ni kinda mwenye umri wa miaka 20 tu lakini kila wiki ana uhakika wa kuingiziwa pauni 55,000 kwenye akaunti yake.

Sane ataendelea kuweka mfukoni kitita hicho mpaka pale mkataba wake wa miaka mitano utakapomalizika na hiyo itakuwa ni mwaka 2021.

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

Fati aweka rekodi Barcelona

CATALUNYA, Hispania ANSU Fati ameweka rekodi ya mchezaji kinda wa kwanza kufunga mabao...

Lampard amshika mkono Silva

MANCHESTER, England KOCHA wa Chelsea, Frank Lampard, amesema atamtumia, Thiago Silva, katika mechi nyingi msimu huu licha ya kuwa na umri wa miaka...

Tuchel awatolea uvivu Mbappe, Neymar

PARIS, Ufaransa KOCHA wa PSG, Thomas Tuchel, amechukizwa na kiwango kibovu walichoonyesha mastaa wa timu hiyo, Kylian Mbappe na Neymar, kwenye mechi...

IBRA:Kifaa kipya Konde Gang aliyetembea kwa mguu kumwinda Harmonize

NA BRIGHITER MASAKI UKITAJA vijana wanaofanya vizuri katika mziki wa bongo fleva, huwezi kukosa kumtaja msanii chipukizi anayefahamika zaidi...

Jay-Z: Mama aliingilia bifu langu na Nas

-Z: Mama aliingilia bifu langu na Nas New York, Marekani HAKUNA shabiki wa Hip hop asiyelifahamu...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -