Tuesday, October 27, 2020

MASTAA HAWA WATAENDELEA KUKUMBUKWA ZAIDI MAN UTD

Must Read

Hamilton avunja rekodi Ureno

LISBON, Ureno STAA wa mbio za magari Lewis Hamilton, amevunja rekodi ya Valtteri...

Ronaldinho naye ana Corona

RIO, Brazil MKONGWE wa Brazil, Ronaldinho, amethibitishwa ana virusi vya corona. Ronaldinho aliandika...

Sterling amlilia kinda wao Man City

MANCHESTER, England WINGA wa Manchester City, Raheem Sterling, ameandika ujumbe wa majonzi baada ya...

MANCHESTER, ENGLAND

MIAMBA ya England, Manchester United ni kati ya timu zenye mafanikio makubwa katika  Ligi Kuu nchini humo kutokana na kwamba ndiyo pekee ambayo imeweza kutwaa taji hilo mara 20 ikifuatiwa na mahasimu wao, Liverpool ambao wamewahi kufanya hivyo mara 18.

Katika mafanikio hayo yakiwamo pia na mataji kadhaa ya michuano mbalimbali, kuna wachezaji ambao wanatajwa kama mastaa bora wa muda wote mahali hapo ikichagizwa na utendaji kazi wao mkubwa wa kung’arisha kikosi cha Mashetani hao Wekundu kufanya vizuri zaidi.

Katika makala haya BINGWA litajaribu kuchambua baadhi ya wachezaji ambao wamechangia mafanikio hayo.

Rio Ferdinand

Ferdinand licha ya kujiunga na United 2002 akitokea Leeds United na kuwakuta wakali wengine katika safu hiyo ya ulinzi kama kina Laurent Blanc, John O’Shea, Wes Brown, Ronny Johnsen, Mikael Silvestre na Gary Neville, lakini aling’ara kweli kweli na kudumu kwenye kikosi cha kwanza.

Katika msimu wake huo wa kwanza akicheza jumla ya michezo 28, alifanikiwa kutengeneza ukuta mgumu na kuifanya United kuwa miongoni mwa timu chache zilizoruhusu nyavu zao kuguswa mara chache zaidi.

Aina ya utulivu wake akicheza nafasi hiyo ya beki wa kati asilia ikiashiria kabisa tamaduni za  soka la England, staili yake hiyo ni kivutio kwa  kizazi cha wachezaji wengi wa ligi hiyo na baadhi ya ligi kadhaa barani Ulaya.

 Denis Irwin

Irwin kwa misimu 12 aliyodumu Old Trafffod, akicheza kwa fomu ya juu upande wa beki wa kushoto tungu alipowasili mahali hapo 1990 hadi 2002 katika mafanikio lukiki ya kocha Alex Ferguson, nyota huyo alichangia kwa kiasi kikubwa.

Nyota huyo alikuwa na uwezo wa kucheza beki wa pembeni pande zote mbili kushoto na kulia kwa nyakati tofauti kulingana na mahitaji ya kocha. Hadi anaondoka viunga hivyo alikuwa ameshuka dimbani mara 529 na kumfanya kuwa miongoni mwa machaguo nane ya Ferguson ya muda mrefu kwenye kikosi chake.

Cristiano Ronaldo

Akiwa katika ubora wake, Ronaldo alitumia misimu mitatu na alifanikiwa kunyakuwa mataji kadhaa ya Ligu Kuu, FA, Kombe la Ligi na Ligi ya Mabingwa Ulaya na katika muda huo alitajwa kama mchezaji aliyetoa mchango mkubwa ndani ya timu.

 Gary Neville

Neville beki wa kulia wa zamani wa Mashetani Wekundu, anatajwa kama miongoni mwa alama ya United iliyofanya vyema. Hadi anatundika daluga 2011, alikuwa ameichezea timu yake hiyo pekee kwenye maisha yake ya soka la ushindani jumla ya michezo 600.

Mwingereza huyo alianza kung’ara akiwa na  umri wa miaka 19 akicheza eneo hilo la beki wa kulia ingawa kuna wakati wachambuzi wa soka walimhukumu kwa makosa madogomadogo ya kupoteza mipira mara kadhaa. Lakini bado anabaki kuwa mchezaji aliyekuwa na kipaji kikubwa kilichoibeba United.

 Wayne Rooney

Hivi sasa umri unaonekana kumpa mkono wa kwa kheri nahodha Rooney na kufikia hatua ya kukosa nafasi kwenye kikosi cha kwanza kutokana na kushuka kiwango kwa misimu ya hivi karibuni, lakini rekodi za nyuma zinaonyesha raia huyo wa England yuko kwenye orodha ya mafundi waliofanya vyema kwa mafanikio zaidi mahali hapo.

Mchango wa Rooney katika timu hiyo ni kwamba, ameiwezesha Man Utd ikiwa chini ya  Sir Alex Ferguson, kutwaa mataji matano na huku akiwa ameifungia timu hiyo mabao 179.

 Peter Schmeichel

Schmeichel ni mlinda mlango anayezungumzwa zaidi midomoni mwa wachambuzi wengi wa soka kulingana na umahiri wake langoni na  uhodari wa kupangua penalti jambo ambalo lilimfanya kupachikwa jina la mikono mia moja.

Mkongwe huyo alikuwa miongoni mwa nyota tegemeo aliyeshinda mataji kadhaa ikiwamo kombe la ligi mara tano na ‘European Cup’, alidumu United kwa miaka tisa kutimkia klabu za Spoting CP, Aston Villa na Manchester City.

Paul Scholes

Ni mmoja kati ya viungo ambao mjadala wao ni  mkubwa duniani kote kutokana na ubora aliokuwa nao katika kipindi cha miaka kumi iliyopita

Kwa mujibu wa aliyekuwa kocha wake, Furguson, aliwahi kukaririwa akisema staa  huyo hakuwa tu kiungo bora duniani isipokuwa ni mchezaji wa daraja la juu sana.

Roy Keane

Keane alikuwa mchezaji mwingine aliyekuwa akiongeza nguvu katika safu ya kiungo katika kikosi cha Man United, licha ya matukio kadhaa ndani ya uwanja ukiwamo utovu wa nidhamu, lakini ujasiri wake wa kupambana ulimfanya kuwa uti wa mgongo wa United, asilimia kubwa kupata matokeo chanya katika misimu yote aliyodumu Old Trafford, ikiwamo mchezo wa fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya dhidi ya Juventus msimu wa 1998/99, ambapo Mashetani hao wekundu waliibuka na ushindi wa mabao 3-2.

Ryan Giggs

Giggs pia ni miongoni mwa mastaa walioweka rekodi ya aina yake klabuni kwake hapo kutokana na kucheza jumla ya michezo 963 kwa mafanikio makubwa zaidi akicheza upande wa winga ambapo alijivunia heshima kubwa hadi kwa mashabaki wa timu pinzani kwa kupigiwa makofi.

 Eric Cantona

Cantona ni kizazi cha dhahabu 1992, aliyefanya  vizuri zaidi mahali hapo akichagizwa zaidi na kipaji alichokuwa nacho Mfaransa huyo sambamba na kina Ryan Giggs na Paul Scholes. Akidumu viunga hivyo kwa miaka mitano pekee 1992-1997, aliingia kimiani mara 64 ikiwa ni jumla ya michezo 143, inaelezwa vile vile ni fowadi aliyekuwa kivutio Ligi Kuu England.

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

Hamilton avunja rekodi Ureno

LISBON, Ureno STAA wa mbio za magari Lewis Hamilton, amevunja rekodi ya Valtteri...

Ronaldinho naye ana Corona

RIO, Brazil MKONGWE wa Brazil, Ronaldinho, amethibitishwa ana virusi vya corona. Ronaldinho aliandika ujumbe kupitia ukurasa wake wa...

Sterling amlilia kinda wao Man City

MANCHESTER, England WINGA wa Manchester City, Raheem Sterling, ameandika ujumbe wa majonzi baada ya kinda wa zamani wa timu...

Afua Suleiman afunguka ‘Utalijua Jiji’ ilivyompa ustaa mjini

NA JEREMIA ERNEST JINA alilopewa na wazazi wake ni Afua Suleiman na hata alipojitupa kwenye ulimwengu wa muziki wa...

Keche: Kundi maarufu Ghana linalowatamani Diamond, Kiba, Harmonize

JIACHIE na Staa Wako, wiki hii tumetua mpaka Accra, Ghana kwa kundi maarufu la muziki nchini humo, Keche linofanya vizuri na ngoma...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -