Thursday, October 22, 2020

MASTAA HAWA WATATUA AFRIKA KUKINUKISHA

Must Read

Director Kenny: Harmonize alinipeleka WCB nikafanya video ya Lavalava

MWONGOZAJI bora wa video nchini, Kenned Sanga a.k.a Derector Kenny kutoka Zoom Extra, ametua   hapa Jiachie na...

Rogers mwanamuziki anayevutiwa na Marijani

NA JEREMIA ERNEST BONGO Star Search (BSS), ni shindano lililofanikiwa kuibua vipaji vingi vya...

Ihefu, Azam patachimbika Sokoine, Katwila ndani

NA ASHA KIGUNDULATIMU ya Ihefu inatarajia kushuka uwanjani kucheza na Azam ukiwa ni mchezo wa Ligi Kuu...

London, England

FAINALI za Mataifa ya Afrika (Afcon) zinatarajiwa kuanza kutimua vumbi mwakani.

Michuano hiyo itakayofanyika nchini Gabon inashirikisha mataifa 16 na itaanza Januari 14 na kufikia tamati Februari 5.

Habari mbaya kwa baadhi ya timu za Ligi Kuu England ni kwamba zitalazimika kuwakosa wachezaji wao wa Kiafrika kwa kipindi chote hicho.

Wafuatao ni baadhi ya mastaa wa Ligi Kuu England ambao watatua barani Afrika kuziwakilisha timu za taifa kwenye michuano hiyo ya Afcon.

  1. Eric Bailly (Ivory Coast)

BEKI huyo wa kati wa Manchester United atakuwa na uzi wa Ivory Coast katika mashindano ya Afcon.

Staa huyo alitua Man United akitokea Villarreal, huku dau lake likitajwa kuwa ni pauni milioni 30.

Tangu alipotua klabuni hapo akiwa ni mchezaji wa kwanza kusajiliwa na Jose Mourinho, Bailly amejihakikishia nafasi kwenye kikosi cha kwanza.

Amesaini mkataba wa miaka minne kuichezea Man United na si rahisi kuachwa kwenye kikosi cha Ivory Coast kitakachokwenda Gabon.

 

  1. Saido Mane (Senegal)

Mane alisajiliwa na Liverpool akitokea Southampton na uhamisho wake uliigharimu klabu hiyo pauni milioni 30.

Tangu hapo, Mane amekuwa sehemu muhimu ya kikosi cha Liver kinachonolewa na Mjerumani, Jurgen Klopp.

Hakuna shaka kuwa ana nafasi kubwa ya kwenda Gabon na timu yake ya taifa ya Senegal.

  1. Mohamed Elneny (Misri)

Kiungo huyo anakipiga katika klabu ya Arsenal ya Mfaransa, Arsene Wenger.

Kuna uwezekano mkubwa wa Arsenal kuikosa huduma yake kwa takribani mwezi mmoja wakati mashindano ya Afcon yatakapoanza.

Hakuna shaka kuwa atakuwa na kikosi cha Misri kwenye mashindano hayo makubwa barani Ulaya.

  1. Andre Ayew (Ghana)

Mchezaji huyo kwa sasa anaichezea West Ham na ana uhakika wa kupata namba kwenye kikosi cha Ghana kitakachoshiriki Afcon 2017.

Kwenye kikosi cha Ghana, Ayew atakutana na mastaa wenzake wa Ligi Kuu England ambao wanakipiga katika klabu za Jeffrey Schlupp na Daniel Amartey.

  1. Bakary Sako (Mali)

Sako amekuwa nguzo imara ya safu ya kiungo wa Crystal Palace msimu huu. Kiungo mshambuliaji huyo atatua Afrika kuiwakilisha Mali katika fainali za Afcon.

Klabu yake ya kwanza ilikuwa ni Chateauroux kabla ya kuhamia Saint-Etienne na Wolverhampton Wanderers.

  1. Riyad Mahrez (Algeria)

Leicester City watalazimika kuchezwa mwezi mmoja bila staa wao, Mahrez ambaye hakuna ubishi kuwa atakuwa na Algeria nchini Gabon.

Atakuwa na jukumu la kushirikiana na mchezaji mwenzake katika kikosi cha Leicesre, Islam Slimani, kuhakikisha Algeria inafanya vyema kwenye fainali hizo.

  1. Sofiane Boufal (Morocco)

Boufal ndiyo kwanza ana umri wa miaka 23, lakini amekuwa moto wa kuotea mbali.

Akiwa na umri huo, tayari Boufal amekuwa mchezaji aliyenunuliwa kwa fedha nyingi pale Southampton.

Hivi karibuni, amejihakikishia namba kwenye kikosi cha timu yake ya Taifa ya Morocco na ana uhakika mkubwa wa kucheza fainali za Gabon hapo mwakani.

  1. Didier Ndong (Gabon)

Kuna uwezekano mkubwa wa Ndong kurejea Afrika kulibeba taifa lake la Gabon kwenye fainali za Afcon.

Kwa sasa yuko na Sunderland pale Ligi Kuu England.

Itakumbukwa kuwa, alitua Sunderland akitokea Lorient ya Ufaransa.

Ndong alianzia maisha yake ya soka katika klabu ya CS Sfaxien ya Tunisia ambako alicheza mechi 40 kabla ya kuhamia Lorient mwaka jana.

 

  1. Allan Nyom (Cameroon)

Ni beki wa pembeni wa Bromwich Albion. Alitumia sehemu kubwa ya maisha yake ya soka akiwa na Granada, ambayo aliichezea mechi 220 mpaka anaondoka.

Mwaka jana alijiunga na Watford akitokea Italia alikokuwa akiichezea Udinese, lakini baadaye alihamia Albion.

  1. Wahbi Khazri (Tunisia)

Winga huyo wa kulia alitua Sunderland akitokea Bordeaux kwa dau la pauni milioni 8.

Kabla ya kujiunga na Black Cats, nyota huyo mwenye umri wa miaka 24 alikuwa akiwaniwa na klabu za Swansea, Aston Villa na Everton.

Mkataba wa sasa wa Khazri na Sunderland utafikia tamati mwaka 2020.

Ni miongoni mwa mastaa wa Ligi Kuu England watakaokuwa Afrika mwakani kucheza fainali za Afcon.

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

Director Kenny: Harmonize alinipeleka WCB nikafanya video ya Lavalava

MWONGOZAJI bora wa video nchini, Kenned Sanga a.k.a Derector Kenny kutoka Zoom Extra, ametua   hapa Jiachie na...

Rogers mwanamuziki anayevutiwa na Marijani

NA JEREMIA ERNEST BONGO Star Search (BSS), ni shindano lililofanikiwa kuibua vipaji vingi vya wanamuziki wa Tanzania ambao miongoni...

Ihefu, Azam patachimbika Sokoine, Katwila ndani

NA ASHA KIGUNDULATIMU ya Ihefu inatarajia kushuka uwanjani kucheza na Azam ukiwa ni mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara  (VPL), utakaochezwa leo...

Mugalu atema cheche Simba

NA ASHA KIGUNDULA MSHAMBULIAJI wa Simba, Chris Mugalu, amesema wanakwenda mkoani Rukwa kupambana na kupata ushindi katika mchezo wao...

Malale aitisha Yanga

NA ZAINAB IDDY KOCHA Mkuu wa timu ya Polisi Tanzania, Malale Hamsini, amezisikia sifa za kocha mpya wa Yanga,...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -