Tuesday, November 24, 2020

MASTAA LIGI KUU ENGLAND ‘WALIVYOKICHAFUA’ WAKIWA NA MATAIFA YAO

Must Read

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika...

DEWJI: CHAMA NI SIMBA HADI 2022

Kiungo huyo raia wa Zambia, aliyetoa mchangomkubwakwaSimbakufikisharobo fainaliyaLigiyaMabingwaAfrikamsimuwa 2018/19, ikiwamo kutwaa ubingwa wa LigiKuuTanzaniaBarakwa misimumitatu mfululizo, awali...

LONDON, England

WIKI iliyopita kulikuwa na mapumziko ya kimataifa ambapo ligi mbalimbali duniani zilisimama kupisha mechi za timu za taifa.

Mastaa mbalimbali wa Ligi Kuu England waliziacha klabu zao na kujiunga na timu zao za taifa katika mechi za kuwania tiketi ya kucheza fainali za Kombe la Dunia za mwaka 2018.

Lakini pia, wengine walikuwa na mataifa yao katika mechi za kirafiki.

Mabao mengi yalifungwa na hata wachezaji wa klabu mbalimbali vigogo kupata majeraha wakati wakipambana kuyaokoa mataifa yao.

Arsenal

Alex Oxlade-Chamberlain, hakupata nafasi ya kuichezea England katika mchezo wa Jumatano iliyopita ambapo kikosi hicho kilichapwa bao 1-0 na Ujerumani.

Lakini alicheza kwa dakika zote 90 katika mchezo dhidi ya Lithuania uliochezwa juzi.

Kipa David Ospina hakuruhusu nyavu za Colombia kutikiswa kwani timu yake hiyo iliichapa Bolivia bao 1-0.

Alexis Sanchez alikuwa uwanjani kwa dakika 90 wakati taifa lake la Chile likichapwa bao 1-0 na Argentina katika mchezo wa kuwania kufuzu Fainali za Kombe la Dunia za Urusi zitakazofanyika mwaka ujao.

Nyota Alex Iwobi alicheza dakika 61 katika kikosi chake cha Nigeria katika mchezo wa kirafiki waliotoa sare ya bao 1-1 na Senegal.

Aaron Ramsey alikuwa uwanjani wakati Wales ikitoka bila kufungana na Jamhuri ya Ireland, mchezo uliochezwa Ijumaa ya wiki iliyopita.

Jumamosi ya wiki iliyopita, Granit Xhaka, alikuwa akiiwakilisha Uswisi katika mchezo ambao waliwafunga Latvia bao 1-0.

Olivier Giroud aliifungia Ufaransa mabao mawili katika ushindi wa mabao 3-1 dhidi ya Luxembourg, mtanange wa Kundi A uliopigwa Jumamosi ya wiki iliyopita.

Katika mchezo huo, Laurent Koscielny alikuwa nguzo imara kwenye safu ya ulinzi ya Ufaransa.

Mesut Ozil alitokea benchi na kucheza kwa dakika 29 wakati taifa lake la Ujerumani liliposhinda mabao 4-1 dhidi ya Azerbaijan.

Hata hivyo, Shkodran Mustafi, aliishia benchi kwenye kikosi hicho cha Ujerumani.

Chelsea

Gary Cahill alicheza kwa muda wote wa mchezo wakati England ilipochapwa bao 1-0 na Ujerumani.

Willian alicheza dakika tano wakati taifa lake la Brazil liliposhinda mabao 4-0 dhidi ya Uruguay. Mchezo huo ulikuwa wa kuwania tiketi ya kucheza Fainali za Kombe la Dunia za Urusi.

Diego Costa alicheza kwa dakika zote za mchezo wakati Hispania ilipoichapa Israel mabao 4-1. Pedro hakuingia kabisa katika mchezo huo kuiwakilisha Hispania.

Huenda Costa akaukosa mchezo dhidi ya Ufaransa kutokana na majeruhi.

Nemanja Matic alikuwa na Serbia kwa dakika zote 90 za mchezo dhidi ya Georgia.

Thibaut Courtois alikuwa langoni wakati Ubelgiji ilipoambulia sare ya 1-1 dhidi ya Ugiriki. Mbelgiji mwenzake katika kiklosi cha Chelsea, Michy Batshuayi, hakucheza kabisa.

Liverpool

Adam Lallana aliingia kwenye kikosi cha kwanza wakati kikosi chake cha England kilipochapwa bao 1-0 na Ujerumani.

Katika mchezo huo, Emre Can, alitokea benchi kuipa nguvu Ujerumani ingawa aliukosa mchezo dhidi ya Azerbaijan.

Lallana alicheza vizuri dhidi ya Lithuania ambapo pasi yake ilizaa bao.

Philippe Coutinho na Roberto Firmino walianza kwenye kikosi cha Brazil kilichoiua Uruguay mabao 4-1 katika mchezo wa kuwania kufuzu Kombe la Dunia.

Sadio Mane aliiwakilisha Senegal kwa dakika 25 katika mchezo ambao timu yake iliambulia sare ya bao 1-1 mbele ya Nigeria.

Georginio Wijnaldum, aliitwa benchi kipindi cha pili wakati timu yake ya Uholanzi ilipochapwa mabao 2-0.

Simon Mignolet na Divock Origi, walibaki benchi wakati taifa lao la Ubelgiji lilipotoa sare ya bao 1-1 na Ugiriki.

Man City

Leroy Sane aliichezea Ujerumani iliyoshinda bao 1-0 dhidi ya England na alikuwa uwanjani walipoitandika Azerbaijan mabao 4-1.

Fernandinho aliichezea Brazil dakika tisa lakini timu yake iliifunga Uruguay mabao 4-1.

Sergio Aguero na Nicolas Otamendi, walikuwa uwanjani kuiwezesha Argentina kushinda bao 1-0 dhidi ya Chile ambayo langoni ilikuwa na staa mwenzao kwenye kikosi cha Man City, Claudio Bravo.

Kelechi Iheanacho aliifungia Nigeria bao la penalti na kuipa sare ya bao 1-1 mbele ya Senegal.

David Silva aliifungia Hispania bao la kwanza katika ushindi wa mabao 4-1 dhidi ya Israel.

Aleksandar Kolarov, alikuwa uwanjani kwa muda wote wa mchezo wakati Serbia yake ilipoifunga Georgia.

John Stones wa England alicheza dhidi ya Ujerumani kabla ya kuiwakilisha tena katika mchezo dhidi ya Lithuania.

Raheem Sterling alitoa pasi ya bao la Jermain Defoe, wakati England iliposhinda mabao 2-0 dhidi ya Lithuania.

Man Utd

Chris Smalling alianza wakati Jesse Lingard, Luke Shaw na Marcus Rashford walitokea benchi katika kikosi cha England kilichochapwa bao 1-0 na Ujerumani.

Rashford alitokea benchi tena dhidi ya Lithuania huku Shaw na Lingard wakiishia kuutazama mchezo huo wakiwa benchi.

Antonio Valencia alicheza kwa dakika 90 wakati timu yake ya Ecuador ilipochapwa mabao 2-1 na Paraguay.

Sergio Romero na Marcos Rojo waliiwezesha Argentina kupata ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Chile.

David De Gea alikuwa langoni mwa Hispania wakati timu hiyo ilipoibuka na ushindi wa mabao 4-1 dhidi ya Israel.

Italia haikumtumia Matteo Darmian iliposhinda mabao 2-0 dhidi ya Albania.

Daley Blind alikuwa uwanjani wakati Uholanzi yake ilipochapwa mabao 2-0 na Bulgaria.

Marouane Fellaini alikosa nafasi nyingi za mabao na hatimaye kutolewa katika mchezo ambao timu yake ya Ubelgiji ilipata sare ya bao 1-1 dhidi ya Ugiriki.

Henrikh Mkhitaryan alifunga mara moja katika ushindi wa Armenia wa mabao 2-0 dhid ya Kazakhstan.

Tottenham

Dele Alli, Eric Dier na Kyle Walker, walikuwa kwenye kikosi cha kwanza cha England kilichochapwa bao 1-0 na Ujerumani.

Walker, Alli na Dier walirudi tena uwanjani dhidi ya Lithuania.

Hugo Lloris alikuwa langoni mwa Ufaransa na kukisaidia kikosi hicho kushinda mabao 3-1 dhidi ya Luxembourg.

Jan Vertonghen alikuwa na Ubelgiji, Moussa Dembele, walikuwa kwenye kikosi cha Ubelgiji.

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania...

DEWJI: CHAMA NI SIMBA HADI 2022

Kiungo huyo raia wa Zambia, aliyetoa mchangomkubwakwaSimbakufikisharobo fainaliyaLigiyaMabingwaAfrikamsimuwa 2018/19, ikiwamo kutwaa ubingwa wa LigiKuuTanzaniaBarakwa misimumitatu mfululizo, awali ilidaiwa alikuwa yupo katika hatuayamwishoyakujiunganaYanga.

Sven aruka kihunzi

NA ASHA KIGUNDULA KOCHA Mkuu wa Simba, Sven Vandenbroeck, ameruka kihunzi na kuwaachia msala nyota wake, Clatous Chama na...

Sarpong ‘aua’ shabiki Simba

Na MWANDISHI WETU, MWANZA BAO la dakika ya 29 lililofungwa na Michael Sarpong wa Yanga juzi, limesababisha kifo cha...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -