Friday, December 4, 2020

MASTAA WA DRC WALIVYOUKARIBISHA MWAKA 2017

Must Read

HUJUMA NZITO YANGA

NA WINFRIDA MTOI UONGOZI wa Yanga upo katika harakati za kuhamishia mechi zao zilizobaki...

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika...

NA NOAH YONGOLO


WAPENZI wa Kona ya Bolingo nawapongeza sana kwa kuweza kuuona mwaka mpya wa 2017.

Wapo wenzetu wengi wameshindwa kuuona, hivyo ni jambo la kumshukuru Mwenyezi Mungu, kwani sisi tuliobahatika kuvuka salama na kuuona mwaka hizo ni neema tu wala si ujanja wetu.

Kona ya Bolingo bado ingali ndani ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo DRC, ambapo kuna mengi yalijiri na yanaendelea kujiri katika kipindi hiki  cha kusherehekea mwaka mpya wa  2017.

Kama nilivyosema hapo juu, baadhi ya wakali wa muziki katika DRC  wameendelea kunogesha sherehe hizo kwa kufanya shoo kali na za kufa mtu ndani na nje  mipaka ya Kongo DR.

Miongoni mwao  ni JB Mpiana’ Mokonzi ya Ba Wenge’ yeye baada ya ziara ya nchini Malawi kupata mafanikio makubwa kuitangaza albamu yake mpya ijayo ‘Balle De Match’, alirejea jijini Kinshasa kwa muda na sasa tayari ameshawasili nchini Equatorial Guinea kuendelea na ziara hiyo akiuwasha  moto mkali wa shoo kali.

Katika ziara hiyo Mpiana ameambatana na silaha zake hatari wakiwamo Nono Fuji ‘NF’, Atchuda, Zagoko, Rio De Janein, Segun Mignon ‘Maniata’, Tramendo, Julles Kibens, Tolbee Solo, Sunda Bass, Ficarre Muamba ‘Fi Fi Maitre’, Fusee De Guerre, Lisimo Gentamicine na wengine wengi.

Mtu mzima Koffi Olomide ‘DJ Mopao Mokonzi’ yeye yuko jijini Kigali nchini Rwanda ambapo alipiga shoo ya nguvu siku ya mkesha wa mwaka mpya na vijana wake wa Quarter Latin kwenye ukumbi wa Convention Center.

Kisha akaangusha shoo nyingine kali ndani ya Serena Hoteli ambapo watu walijipapasa mifukoni na kutoa dola 700 za Kimarekani kwa ajili ya kiingilio.

Naye mfalme wa msitu ‘Le Roi De La Foret’ Noel Ngiama Makanda Werrason, mara  baada ya kusherehekea siku yake ya kuzaliwa Desemba  25, ameendelea kusalia jijini Luandai Angola akiwa na  bendi yake ya Wenge Musica Maison Mere ‘WMMM’ akifanya mavitu.

Mbali ya shoo aliyopiga wakati wa sikukuu ya Krismasi pamoja na mwaka mpya, Werrason amepewa shavu zaidi la kuendelea kuwapo nchini humo kwa kuongezewa shoo nyingine zaidi.

Kwa mujibu wa ratiba iliyotolewa na waandaaji wake, kesho atawasili katika  mji wa Lucapa ambapo Januari 6 atakuwa kwenye mji wa Dundo katika Mkoa wa  Lunda Notre ambako atashusha shoo ya maana.

Januari atakuwa hapo hapo mjini Dundo kwenye ukumbi maarufu wa Nzaji.

Jumamosi ya Januario 14 atasafiri mpaka kwenye mji wa Lucapa mkoani Lunda Norte na kupiga shoo ya nyingine kabla ya kurudi tena jijini Luanda Januari 17 na  kuwapagawisha mashabiki wake.

Jumamosi Januari 21 atapiga tena shoo kwenye bwawa la kuogelea la Alvalade jijini Luanda kabla ya kuhitimisha ziara hiyo, ambapo Januari  23 ataagana na wenyeji wake kisha kurejea jijini Kinshasa.

‘Wakuu wa Nchi’, Zaiko Langa Langa chini ya uongozi shupavu wa mkongwe Nyoka Longo Jossart, wao hawakwenda mbali walibakia jijini Kinshasa na kupiga shoo ya nguvu siku ya  Krismasi na mwaka mpya.

Mpendwa msomaji, kwa uchache hayo ndiyo yaliyojiri katika kipindi hiki cha shamrashamra za kuuaga mwaka 2016 na kuukaribisha mwaka mpya wa 2017, kwa leo naomba nihitimishie hapa tukutane tena wiki ijayo.

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

HUJUMA NZITO YANGA

NA WINFRIDA MTOI UONGOZI wa Yanga upo katika harakati za kuhamishia mechi zao zilizobaki...

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul 'Ben Pol' ameshukuru mashabiki kwa...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania...

DEWJI: CHAMA NI SIMBA HADI 2022

Kiungo huyo raia wa Zambia, aliyetoa mchangomkubwakwaSimbakufikisharobo fainaliyaLigiyaMabingwaAfrikamsimuwa 2018/19, ikiwamo kutwaa ubingwa wa LigiKuuTanzaniaBarakwa misimumitatu mfululizo, awali ilidaiwa alikuwa yupo katika hatuayamwishoyakujiunganaYanga.

Sven aruka kihunzi

NA ASHA KIGUNDULA KOCHA Mkuu wa Simba, Sven Vandenbroeck, ameruka kihunzi na kuwaachia msala nyota wake, Clatous Chama na...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -