Tuesday, October 20, 2020

Mastaa wa kike ambao ni mfano wa kuigwa ‘Bongo’

Must Read

Director Kenny: Harmonize alinipeleka WCB nikafanya video ya Lavalava

MWONGOZAJI bora wa video nchini, Kenned Sanga a.k.a Derector Kenny kutoka Zoom Extra, ametua   hapa Jiachie na...

Rogers mwanamuziki anayevutiwa na Marijani

NA JEREMIA ERNEST BONGO Star Search (BSS), ni shindano lililofanikiwa kuibua vipaji vingi vya...

Ihefu, Azam patachimbika Sokoine, Katwila ndani

NA ASHA KIGUNDULATIMU ya Ihefu inatarajia kushuka uwanjani kucheza na Azam ukiwa ni mchezo wa Ligi Kuu...

Na Happyglory Urassa

WANAPOZUNGUMZIWA mastaa wa kike hapa Bongo wanaojihusisha na mambo mbalimbali wapo wengi sana ingawa wengine wamesahaulika kwa sasa, lakini bado wakitokea kwenye jamii wanaheshimika kutokana na vitu au kazi walizowahi kufanya hapo awali.

Baadhi ya mastaa hao wamejaribu kuhakikisha kuwa ‘status’ yao haishuki na wanatumia majina yao ipasavyo kujiendeleza kiuchumi, lakini pia kuisaidia jamii na si kuwa na ustaa wa kwenye mitandao kama baadhi yao walivyo.

Kwa jina jingine ambalo linawafaa mastaa hawa ni ‘wanawake wa shoka’ kwani wanajitambua wao ni nani pia wanakipigania kile wanachoamini kwamba wanastahili.

Nje ya kujulikana kwao, pia wana maisha yao ambayo hatuyaoni kwenye mitandao ya kijamii, wakiwa makini zaidi kwenye kazi na kutengeneza fedha kuliko ‘kiki’ zisizo na maana.

Vannesa Mdee

Vannesa maarufu ‘V-Money’, ni mwanadada anayefanya vizuri kwenye tasnia ya muziki wa kizazi kipya, ambapo alianza harakati zake za kuimba huku wadau wachache ndio waliokuwa wakielewa kile alichokuwa akikifanya.

Lakini kadiri siku zilivyozidi kwenda na bidii aliyojiwekea mwenyewe, taratibu alianza kujizolea umaarufu na mashabiki lukuki.

Tunapomzungumzia Vanessa kwa sasa ni moja kati ya wanamuziki wa kike wanaofanya vizuri Afrika, kwani amekuwa akitajwa kwenye tuzo kubwa barani humu na alifanikiwa kutwaa tuzo za MTV Africa Music na zile za Kora.

Ni juhudi za kipekee zilizomfanya Vanessa afanikiwe kwenye kazi zake, hana mambo ya kujikweza na kutafuta ‘kiki’ zisizo na maana, huwezi kumsikia akiyaongelea maisha yake binafsi kwenye mitandao au kwenye vyombo vya habari.

Maisha yake yameegemea kwenye harakati za kweli za kujitengenezea maisha mazuri, ni wazi kuwa mafanikio yake makubwa ameyapata kupitia sanaa yake ukiacha miradi yake mingine mingi aliyonayo.

Elizabeth Michael (Lulu)

Lulu ni msichana mwenye umri mdogo mwenye umaarufu mkubwa kwenye tasnia ya uigizaji na mmoja wa waigizaji ghali ambao bila milioni 20 hawezi kufanya kazi na wewe.

Ni mwanamke mwenye kipaji cha hali ya juu kwenye filamu za Kibongo, hata waandaaji wa tuzo za Afica Magic Viewers Choise huko Nigeria wakauona uwezo wake na kumpambanisha na waigizaji maarufu kama Omotola Jalade, Ritha Dominic na wakali wengine kutoka Bollywood.

Wengi watakumbuka matokeo ya Lulu baada ya kuchaguliwa kwenye tuzo hizo, kwani alifanikiwa kurudisha heshima nyumbani baada ya kupigiwa kura nyingi zaidi na ni hakika kwamba kura hizo hazikuwa za Watanzania pekee bali hata Afrika Mashariki.

Miaka kadhaa iliyopita Lulu alikuwa akipondwa kwa tabia zake zilizolinganishwa na umri wake mdogo lakini hivi sasa amekuwa na si mtu wa kuanika maisha yake binafsi kwenye mitandao.

Hivi sasa Lulu ni mwanamke makini aliyejikita zaidi kufanya kazi na si ‘drama’ za kwenye mitandao, anajua yeye ni nani na kipi hasa anatakiwa kukifanya.

Lady Jaydee

Mafanikio ya nguli huyu wa muziki yanaufafanua vizuri ule msemo wa ‘Let success make noise’. Ndio, huyu ni mwanamke jasiri na mpambanaji hasa. Kwenye orodha ya wanamuziki wa kike wenye mafanikio Tanzania huyu ndiye anayewakimbiza.

Ameweza kudumu kwenye tasnia ya Bongo Fleva kwa muda mrefu zaidi ya miaka 12 na amekuwa imara wakati wote na kila akiachia wimbo lazima uwe wa taifa kwa kuimbwa na asilimia kubwa ya mashabiki wake.

Kuwa mmiliki wa sehemu ya burudani, kumiliki bendi ya muziki na miradi mingine mingi anayomiliki Jaydee ni vitu vinavyoweza kukuonyesha ni jinsi gani mwanadada alivyo mfano halisi wa upambanaji.

Kitu usichokijua kuhusu Binti Machozi ni kwamba huwezi kumwona anaweka mambo yake ya ndani kwenye mitandao, ni msiri sana na hicho ndicho kinachomsaidia zaidi kwani watu wanajua zaidi kazi zake na mafanikio yake.

Miriam Odemba

Miss Temeke wa mwaka 1997, Odemba naye ni kati ya ‘wanawake wa shoka’. Aliwahi kupeperusha bendera ya taifa kwa kuiwakilisha katika mashindano ya ulimbwende ya dunia mwaka 2008 na kuishia kwenye hatua ya 16 bora.

Hakukata tamaa, akaendelea na harakati zake za kusaka mafanikio akikitumia kipaji chake. Kabla ya kuhamisha nguvu zake kwenye masuala ya mitindo na anaendelea kufanya vizuri.

Kwa sasa Odemba ni mwanamitindo anayeangaliwa sana na wasichana wadogo Tanzania wenye ndoto za kuwa wanamitindo wenye mafanikio.

Wema Sepetu

Mama wa vigoma kwa sasa, Miss Tanzania 2006, Wema ni msanii pekee wa Bongo Movie anayependwa na kuzungumziwa zaidi na watu kuliko msanii yeyote yule.

Licha ya changamoto nyingi anazokutana nazo, Wema anaweza kuzikabili na kunyanyuka tena, hakuna anachokifanya mrembo huyu kisifanikiwe licha ya mapungufu aliyonayo lakini ni mwanamke anayefanya kazi sana na ni mbunifu.

Shoo aliyoianzisha ‘Madame’ ijulikanayo kama Vigoma imememtengenezea fedha nyingi sana ukiacha biashara ya ‘lipstick’, viatu na miradi mingine mbalimbali.

Aidha, amekuwa akiingiza fedha kutokana na mialiko maalumu anayokaribishwa kwenye shughuli mbalimbali (special appearance).

Tofauti na wanawake wengine wa shoka, Wema amekuwa si mtu wa maisha ya siri kwani kila kitu chake kinajulikana katika mitandao ya kijamii.

Jacquline Mengi (K-Lyin)

Miss Tanzania mwaka 2000 na mwakilishi wa Tanzania, Miss World mwaka 2004. Hakufanya vizuri kwenye mashindano hayo ya dunia ambapo aliamua kuingia kwenye tasnia ya muziki wa Bongo Fleva mwaka 1997 na kudumu kwa muda wa miaka kumi mpaka alipoamua kubadilisha fani na kujihusisha zaidi na ubunifu wa masuala ya urembo wa samani na nyumba.

K-lyin ameweza kusimamia jina lake na kuhakikisha linadumu kwa zaidi ya miaka 20 sasa. Huyu si mtu wa ‘drama’ kwenye mitandao, mtulivu na anajitambua.

Wasichana wengi Afrika Mashariki wanavutiwa sana na mafanikio yake, kujitoa kwake kwenye jamii na uchapakazi wake ndicho hasa kinachomfanya awe wa kipekee.

Hawa ndiyo baadhi ya mastaa wa kike wenye hadhi ya kuitwa ‘wanawake wa shoka’, wanaojua wanachokifanya. Wasichana wengi wadogo wanawatazama kama mfano kutokana na mafanikio yao, wanatoa hamasa kubwa kwa kizazi cha sasa kwa bidii zao.

 

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

Director Kenny: Harmonize alinipeleka WCB nikafanya video ya Lavalava

MWONGOZAJI bora wa video nchini, Kenned Sanga a.k.a Derector Kenny kutoka Zoom Extra, ametua   hapa Jiachie na...

Rogers mwanamuziki anayevutiwa na Marijani

NA JEREMIA ERNEST BONGO Star Search (BSS), ni shindano lililofanikiwa kuibua vipaji vingi vya wanamuziki wa Tanzania ambao miongoni...

Ihefu, Azam patachimbika Sokoine, Katwila ndani

NA ASHA KIGUNDULATIMU ya Ihefu inatarajia kushuka uwanjani kucheza na Azam ukiwa ni mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara  (VPL), utakaochezwa leo...

Mugalu atema cheche Simba

NA ASHA KIGUNDULA MSHAMBULIAJI wa Simba, Chris Mugalu, amesema wanakwenda mkoani Rukwa kupambana na kupata ushindi katika mchezo wao...

Malale aitisha Yanga

NA ZAINAB IDDY KOCHA Mkuu wa timu ya Polisi Tanzania, Malale Hamsini, amezisikia sifa za kocha mpya wa Yanga,...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -