Saturday, October 31, 2020

MASTAA ‘WALIOWAROGA’ WABONGO

Must Read

Hamilton avunja rekodi Ureno

LISBON, Ureno STAA wa mbio za magari Lewis Hamilton, amevunja rekodi ya Valtteri...

Ronaldinho naye ana Corona

RIO, Brazil MKONGWE wa Brazil, Ronaldinho, amethibitishwa ana virusi vya corona. Ronaldinho aliandika...

Sterling amlilia kinda wao Man City

MANCHESTER, England WINGA wa Manchester City, Raheem Sterling, ameandika ujumbe wa majonzi baada ya...

NA WINFRIDA MTOI,

WAKATI zikiwa zimebaki siku chache kuufunga mwaka huu 2016 na kuukaribisha 2017, tumeona ni vema kukuletea majina ya mastaa ambao wameendelea kubaki kuwa vipenzi vya Watanzania kutokana na sababu mbalimbali.

Kati yao, wapo ambao majina yao yamekuwa hayakosekani kwenye vichwa vya habari vya magazeti yakihusishwa na matukio yasiyopendeza mbele ya jamii, lakini kutokana na mvuto wao binafsi, bado wamekuwa wakitetemekewa kila wanapopita.

Ukiachana na hao, wapo wale ambao wamekuwa wakipendwa mno na jamii kutokana na umahiri wanaouonyesha katika fani zao, lakini pia mwonekano na mwenendo wao kwa ujumla.

BINGWA linakuletea mastaa 10 ambao wanaelekea kuufunga mwaka wakiwa bado wana mvuto wa aina yake kwa jamii, kiasi cha kutetemekewa kila wanakopita au majina yao kutajwa kila dakika.

Wema Sepetu

Mrembo huyo mwenye mvuto wa aina yake ambaye ni Miss Tanzania 2006, ameendelea kuwa kipenzi cha wengi hapa nchini japo mara kadhaa amekuwa akiandamwa na skendo, zaidi zikiwa ni zile za kiuhusiano wa kimapenzi na wanaume tofauti.

Pamoja na hayo, Wema amebaki kuwa staa anayependwa zaidi hapa nchini kiasi kwamba kila anapopita watu hujikuta wakimgombania kupiga naye picha na ‘kuzitupia’ katika kurasa zao za mitandao ya kijamii.

Nyota ya Wema ilianza kuvuma mara tu alipotwaa taji la Miss Tanzania na baadaye kujiingiza kwenye filamu. Wataalamu wa mambo ya mahusiano ya kimapenzi, wanamtaja Wema kuwa mwanamke mwenye mvuto wa kimapenzi kwa wanaume kuliko mastaa wote hapa nchini.

Irene Uwoya

Tofauti na mvuto wa sura yake inayowavutia watu wengi hasa wanaume, nyota yake inazidi  kung’ara  tangu alipoingia kwenye tasnia ya filamu hadi  kufikia hatua ya kuingia kwenye ulingo wa siasa kulikopanua wigo wa shughuli zake.

Uwoya amekuwa kipenzi cha watu hata alipotangaza kugombea ubunge wa viti maalumu, aliweza kuungwa mkono kwa asilimia kubwa bila kujali skendo zozote zilivowahi kumkumba huko nyuma.

Lulu

Elizabeth Michael maarufu kwa jina la Lulu, licha ya kukumbwa na matukio mbalimbali, bado  mvuto na jina lake limesimama pale pale kwa kujiongezea mashabiki kila kukicha na ameweza kuyashawishi makampuni mengi kumtumia katika matangazo ya bidhaa zao.

Akiwa na umri mdogo tu, tayari alishatengeneza jina kwenye ulimwengu wa sanaa wakati akiigiza michezo ya televisheni. Uhodari wake wa kutumia mitandao ya kijamii, imekuwa moja ya njia inayomfanya azidi kuwa Lulu kama jina lake kutokana na mapozi ya picha zake zinazovutia wengi kutazama.

Ali Kiba

Ni mwanamuziki anayetajwa kuwa na kipaji cha hali ya juu kuliko msanii yeyote wa Bongo Fleva hapa nchini, licha ya kushindwa kukitumia vizuri kipaji hicho kujiingizia fedha nyingi kama wanavyofanya wasanii wengine duniani.

Hata hivyo, Kiba huwezi kumtoa kwenye orodha ya watu wenye mvuto hapa nchini na amekuwa kipenzi kikubwa cha watu hasa dada ambao zaidi wanavutiwa na umbo lake pamoja na nyimbo zake zenye hisia.

Diamond Platnumz

Jina lake halisi ni Naseeb Abdul’ ‘Diamond’, huyu kwenye sauti ya kuimba hayuko vizuri sana na hilo aliweza kukiri mwenyewe lakini amejua kutumia watu vizuri katika kuwashirikisha kile alichonacho.

Diamond anaongoza kwa kuwa na mashabiki wengi hapa nchini na huwezi ukataja jina lake mbele za watu wasishtuke. Pia ameweza kuteka akili za watu wengi na kuwafanya wamfuatilie kila jambo analolifanya.

Jokate

Jokate Mwegelo alianzia kwenye umiss mwaka 2006  na hivi sasa ni kati ya majina makubwa hapa nchini akijipatia umaarufu kupitia shughuli zake anazozifanya ikiwamo sanaa na ujasiriamali. Kujichanganya na jamii imefanya kufunika kabisa skendo zinazoelekezwa kwake.

Kanumba

Licha ya kwamba hayupo duniani, huwezi ukataja jina la Steven Kanumba mahali popote watu wasishtuke na kutaka kuhoji nini kimetokea. Alikuwa msanii mwenye nyota kali katika tasnia ya filamu nchini na bado kazi zake zinaendelea kutamba.

Gabo

Anaitwa Salim Ahmed maarufu kwa jina la Gabo, ni msanii wa filamu nchini anayeelekea kuziba pengo la Kanumba. Baada ya kufariki kwa Kanumba wadau wa tasnia hii wanajiuliza nani anaweza kufuata nyayo zake, lakini Gabo anaweza kuziba pengo hilo kutokana na kuonyesha uwezo mkubwa wa kuigiza unaowavutia mashabiki wengi hivi sasa.

Lady Jaydee

Ni mwanamuziki pekee wa kike aliyeweza kudumu kwenye fani kwa muda mrefu na kujiongezea mashabiki kila kukicha. Kuna wakati anakaa kimya bila kutoa kazi yoyote, lakini anaporudi kishindo anachopokelewa nacho, huwezi kulinganisha na mtu mwingine, hii ni kutokana na anavyopendwa na watu wa kila rika.

Joti

Hata mtoto mdogo ukimwamsha usingizini ukimtajia Joti atakwambia ni nani katika ardhi hii ya Bongo. Jina lake halisi ni Lucas Mhavile, amejizolea umaarufu kupitia sanaa ya vichekesho na sasa amejipenyeza kwenye muziki ambako nako anafanya vizuri.

Je, tuambie wewe mastaa wako 10 wa kufungia mwaka ni akina nani? Tuma orodha yako kupitia namba 0764 617590 ambapo tutaitoa katika toleo la BINGWA Jumanne ijayo.

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

Hamilton avunja rekodi Ureno

LISBON, Ureno STAA wa mbio za magari Lewis Hamilton, amevunja rekodi ya Valtteri...

Ronaldinho naye ana Corona

RIO, Brazil MKONGWE wa Brazil, Ronaldinho, amethibitishwa ana virusi vya corona. Ronaldinho aliandika ujumbe kupitia ukurasa wake wa...

Sterling amlilia kinda wao Man City

MANCHESTER, England WINGA wa Manchester City, Raheem Sterling, ameandika ujumbe wa majonzi baada ya kinda wa zamani wa timu...

Afua Suleiman afunguka ‘Utalijua Jiji’ ilivyompa ustaa mjini

NA JEREMIA ERNEST JINA alilopewa na wazazi wake ni Afua Suleiman na hata alipojitupa kwenye ulimwengu wa muziki wa...

Keche: Kundi maarufu Ghana linalowatamani Diamond, Kiba, Harmonize

JIACHIE na Staa Wako, wiki hii tumetua mpaka Accra, Ghana kwa kundi maarufu la muziki nchini humo, Keche linofanya vizuri na ngoma...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -