Sunday, January 17, 2021

MASTAA WATAKAOYABEBA MATAIFA YALIYOFUZU KOMBE LA DUNIA 2018

Must Read

Usiyoyajua sare ya Leicester, United

NI katika mechi ya Ligi Kuu ya England iliyomalizika kwa sare ya mabaon 2-2.-Man United wamemiliki mpira...

Eti Zidane anapangiwa kikosi!

IMEFICHUKA kuwa wachezaji waandamizi wa Real Madrid walikaa kikao na Zinedine Zidane kumwambia wachezaji anaopaswa kuwapanga na...

DIDA ASAINI IHEFU FC

Golikipa wa zamani wa Yanga na Simba, Deogratius Munishi ‘Dida’ amejiunga na Timu ya Ihefu inayoshiliki Ligi...

LONDON, England

MPAKA sasa mataifa tisa yameshajihakikishia kushiriki fainali za Kombe la Dunia za mwakani zitakazofanyika nchini Urusi.

Mbali na wenyeji ambao hupita moja kwa moja, kuna Brazil, washindi mara tano wa fainali hizo, Ubelgiji, Iran, Mexico, Japan, Saudi Arabia, Hispania na Korea Kusini, ambao hii ni mara yao ya tisa mfululizo.

Lakini je, ni wachezaji gani waliofanya kazi kubwa kuzisaidia timu hizo kufuzu na wanatarajiwa kung’ara kwenye fainali za Urusi?

Igor Akinfeev (Urusi)

Kikosi hicho cha kocha Stanislav

Cherchesov, kilishindwa kuvuka hatua ya makundi kwenye michuano ya Kombe la Mabara na hiyo ilikuwa ni baada ya kupoteza mechi zake dhidi ya Mexico na Ureno licha ya kuwafunga New Zealand katika mchezo wa ufunguzi.

Hata hivyo, bado inapewa nafasi kubwa ya kung’ara kwenye michuano ya Kombe la Dunia. Itategemea zaidi uzoefu wa kipa mkongwe, Igor Akinfeev, ambaye amecheza zaidi ya mechi 100.

Kipa huyo mwenye umri wa miaka 31 ambaye amekuwa na CSKA Moscow kwa kipindi chake chote cha maisha ya soka anapewa nafasi

kubwa ya kuwa nahodha katika  fainali hizo.

Eden Hazard (Ubelgiji)

Ubelgiji ndiyo timu ya kwanza barani  Ulaya kufuzu baada ya Urusi licha ya kuwa na timu ngumu za Bosnia-Herzegovina na Ugiriki katika kundi lake.

Katika fainali za mwaka 2014, Ubelgiji walifika robo fainali, wakichapwa na Argentina walioshika nafasi ya pili.

Nchini Urusi, kikosi hicho kitakuwa na mastaa; Moussa Dembele, Marouane Fellaini, Divock Origi, Michy Batshuayi, Thibaut Courtois, Christian Benteke, Romelu Lukaku, Kevin de Bruyne na Eden Hazard.

Hata hivyo, wachambuzi wa soka wanamtaja Eden Hazard kuwa ndiye atakayeng’ara zaidi, wakiamini kukosekana kwake kutaweza kuiyumbisha timu hiyo.

Neymar (Brazil)

Katika kila fainali za Kombe la Dunia, Brazil wamekuwa wakipewa nafasi ya kutwaa ubingwa. Washindi hao mara tano (1958, 1962, 1970, 1994 na 2002), walichapwa mabao 7-1 na Ujerumani katika hatua ya nusu fainali ya Kombe la Dunia mwaka 2014.

Anayetarajiwa kuing’arisha mwakani nchini Urusi ni Neymar aliyetua PSG akitokea Barcelona kwa ada ya pauni milioni 200.

Tayari mkongwe Pele amesema nyota huyo mwenye umri wa miaka 25 ni moto wa kuotea mbali na anastahili tuzo ya Ballon d’Or.

Mbali na Neymar, kikosi hicho kitakuwa na Ederson, Fernandinho, Gabriel Jesus, Philippe Coutinho, Roberto Firmino na Willian wanaokipiga Ligi Kuu England.

Lozano/Chicharito (Mexico)

Hawakupoteza katika michezo ya

kufuzu, wakishinda bao 1-0 dhidi ya Panama.

Wengi wanatarajia makubwa kutoka kwa Mexico kwani wametinga hatua ya mtoano katika fainali sita zilizopita na walifika robo fainali mwaka 1986.

Nyota wanayemtegemea kuwabeba mwakani nchini Urusi ni Hirving Lozano, ambaye ndiye aliyefunga bao pekee katika ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Panama.

Dogo huyo atakuwa akishirikiana na Javier Hernandez ‘Chicharito’ kuipeperusha bendera ya Argentina.

Rezaeian (Iran)

Ni timu inayowezwa kubezwa katika fainali za mwakani, lakini ikumbukwe

kuwa katika mechi za kufuzu

haikuruhusu nyavu zake kuguswa katika mechi 12 mfululizo.

Iran watakwenda Urusi wakiwa chini ya kocha msaidizi wa zamani wa Manchester United, Carlos Queiroz na hii ni mara yao ya tano kucheza Kombe la Dunia.

Mwakani, wataitegemeza zaidi safu yao ya ulinzi, chini ya beki kisiki, Ramin Rezaeian. Beki huyo wa kulia anayeichezea Oostende ya Ligi Kuu Ubelgiji, amekuwa hatari kwa krosi zake.

Son (Korea Kusini)

Fainali za mwaka 2002 ziliwashuhudia wakitinga nusu fainali. Katika mechi zao

za kufuzu safari ya Urusi, wamecheza mechi 10, wakishinda nne na mabao yao 11.

Mwakani, watamtegemea Son Heung-min ambaye amekuwa hatari kwenye safu ya ushambuliaji ya Tottenham.

Lakini pia, watakuwa na Ki Sung-yueng  wa Swansea na mkongwe, Lee Dong-gook, ambaye atakuwa na umri wa miaka 39 huku akiwa amecheza mechi 105.

Kagawa/ Honda (Japan)

Tangu mwaka 1998, Japan haijakosa fainali za Kombe la Dunia.

Watakwenda Urusi wakitarajia msaada mkubwa kutoka kwa staa wake anayekipiga Borussia Dortmund, Shinji Kagawa, ambaye atasaidiana na Keisuke Honda wa AC Milan na Shinji Okazaki anayekipiga Leicester City.

Pia, watakuwa na Takuma Asano ambaye ameshaifungia Japan mabao matatu huku akiiokoa Stuttgart kutoshuka daraja msimu uliopita wa Bundesliga alikokuwa akicheza kwa mkopo akitokea Arsenal.

Isco (Hispania)

Ushindi wa mabao 8-0 dhidi ya Liechtenstein, uliiwezesha Hispania kukata tiketi ya kwenda Urusi.

Waliopachika mabao ni Sergio Ramos, mshambuliaji wa Chelsea, Morata, Isco, David Silva, Iago Aspas, Alvaro Morata na Max Goppel.

Isco anatajwa kuwa mmoja kati ya mastaa watakaoing’arisha Hispania mwakani, hasa kwa kiwango chake katika mchezo walioichapa Italia mabao 3-0.

Mbali na kuonyesha kiwango kizuri, pia alifunga mabao mawili yaliyoiweka Hispania katika mazingira mazuri ya kufuzu fainali za mwakani.

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

Usiyoyajua sare ya Leicester, United

NI katika mechi ya Ligi Kuu ya England iliyomalizika kwa sare ya mabaon 2-2.-Man United wamemiliki mpira...

Eti Zidane anapangiwa kikosi!

IMEFICHUKA kuwa wachezaji waandamizi wa Real Madrid walikaa kikao na Zinedine Zidane kumwambia wachezaji anaopaswa kuwapanga na ndiyo maana timu hiyo imeshinda...

DIDA ASAINI IHEFU FC

Golikipa wa zamani wa Yanga na Simba, Deogratius Munishi ‘Dida’ amejiunga na Timu ya Ihefu inayoshiliki Ligi Kuu Tanzania Bara katika kipindi...

JDart Nation wapanga kutawala Africa

CHRISTOPHER MSEKENA MWANAMUZIKI na bosi wa JDart Nation, JDart, amesema miongoni mwa mipango yake kwa mwaka 2021 ni kuhakikisha...

HUJUMA NZITO YANGA

NA WINFRIDA MTOI UONGOZI wa Yanga upo katika harakati za kuhamishia mechi zao zilizobaki za Ligi Kuu Tanzania Bara...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -