Sunday, January 17, 2021

MASTER Guardiola anavyotembea na historia mfukoni

Must Read

Usiyoyajua sare ya Leicester, United

NI katika mechi ya Ligi Kuu ya England iliyomalizika kwa sare ya mabaon 2-2.-Man United wamemiliki mpira...

Eti Zidane anapangiwa kikosi!

IMEFICHUKA kuwa wachezaji waandamizi wa Real Madrid walikaa kikao na Zinedine Zidane kumwambia wachezaji anaopaswa kuwapanga na...

DIDA ASAINI IHEFU FC

Golikipa wa zamani wa Yanga na Simba, Deogratius Munishi ‘Dida’ amejiunga na Timu ya Ihefu inayoshiliki Ligi...

MANCHESTER, England

NI wazi kuwa kocha Pep Guardiola ameanza kufurahia maisha pale Etihad.

Alifanya hivyo akiwa na Barcelona, akarudia alipokuwa Bayern Munich na sasa ametua Ligi Kuu England na tayari timu pinzani zimeanza kupata joto ya jiwe.

Ukiachana na mbio za kuwania ubingwa wa Ligi Kuu England, kwa upande mwingine, Guardiola ameanza kuonyesha makali yake kwenye michuano ya kimataifa.

Katika mchezo wake wa kwanza wa Ligi ya Mabingwa Ulaya akiwa na Man City, kocha huyo ameibuka na ushindi wa mabao 4-0 dhidi ya timu ngumu ya Borussia Monchengladbach, inayoshiriki Bundersliga.

Matokeo hayo yalikuja ikiwa ni baada ya kuwachapa Steaua Bucharest katika michezo yote miwili ya kufuzu kucheza hatua ya makundi.

Alipokabidhiwa rasmi mikoba ya kuinoa Barca, katika michezo yake nane ya mwanzo, Guardiola alishinda mara tano, alipoteza miwili na sare moja.

Alianza na ushindi mnono wa mabao 4-0 dhidi ya Wisla Krakow katika mtanange wa kuwania kufuzu Ligi ya Mabingwa Ulaya.

Waliporudiana, Barca walichezea kichapo cha bao 1-0, kabla kukumbana na matokeo kama hayo katika mchezo wa ufunguzi wa La Liga (2008-09) dhidi ya ‘vibonde’  Numancia.

Wengi walimtabiria majanga Guardiola, hasa baada ya kikosi hicho kuambulia sare ya bao 1-1 katika mchezo uliofuata dhidi ya Racing de Santander.

Baada ya hapo, Guardiola alishinda michezo yote minne iliyofuata.

Katika idadi hiyo ya mechi nane, Barca waliweza kupasia nyavu mara 19, huku wakifungwa mabao nane pekee.

Hata hivyo, Guardiola aliendeleza moto wake kwa kushinda michezo 11 na huo ukawa ndio mwanzo wa utawala wa kocha huyo kwenye ulimwengu wa soka.

Akiwa Catalunya alishinda mataji mbalimbali, yakiwemo ya La Liga, Copa del Rey na lile la Ligi ya Mabingwa Ulaya.

Alipotua Ujerumani na kujiunga na Bayern, kiungo huyo wa zamani wa Barca na timu ya Taifa ya Hispania alishinda michezo sita kati ya nane ya mwanzo, alipoteza mmoja na kutoa sare mara moja.

Itakumbukwa kuwa Guardiola alikumbana na kichapo katika mchezo wake wa kwanza akiwa Allianz Arena.

Akiwa kwenye benchi la ufundi, Bayern walipokea kichapo cha mabao 4-2 kutoka kwa Borussia Dortmund, iliyokuwa ikinolewa na Jurgen Klopp.

Pia, kulikuwa na matokeo ya sare ya bao 1-1 katika mchezo wa Bundesliga dhidi ya Freiburg.

Moja kati ya kumbukumbu nzuri alizoziacha Bayern, ni ushindi wa mikwaju ya penalti katika mchezo wa UEFA Super Cup dhidi ya wababe wa Magharibi mwa London, Chelsea, waliokuwa wakinolewa na hasimu wake, Jose Mourinho.

Baada ya kushuka dimbani mara nane, safu yake ya ushambuliaji ilikuwa imeshafunga jumla ya mabao 16, huku walinzi wake wakiruhusu nyavu zao zicheke mara nane pekee.

Inaweza ikawa ni mapema mno kutabiri kuwa Guardiola ataendeleza historia yake ya mafanikio akiwa England.

Ni ngumu, hasa kutokana na tofauti ya aina ya uchezaji ya La liga, Bundersliga na hii aliyoikuta England.

Lakini, kwa kasi aliyoanza nayo, ni rahisi pia kuamini kuwa ana uwezo mkubwa wa kufanya maajabu Ligi Kuu England, hasa ikizingatiwa kuwa na historia inayojitosheleza, hasa linapokuja suala la ushindani.

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

Usiyoyajua sare ya Leicester, United

NI katika mechi ya Ligi Kuu ya England iliyomalizika kwa sare ya mabaon 2-2.-Man United wamemiliki mpira...

Eti Zidane anapangiwa kikosi!

IMEFICHUKA kuwa wachezaji waandamizi wa Real Madrid walikaa kikao na Zinedine Zidane kumwambia wachezaji anaopaswa kuwapanga na ndiyo maana timu hiyo imeshinda...

DIDA ASAINI IHEFU FC

Golikipa wa zamani wa Yanga na Simba, Deogratius Munishi ‘Dida’ amejiunga na Timu ya Ihefu inayoshiliki Ligi Kuu Tanzania Bara katika kipindi...

JDart Nation wapanga kutawala Africa

CHRISTOPHER MSEKENA MWANAMUZIKI na bosi wa JDart Nation, JDart, amesema miongoni mwa mipango yake kwa mwaka 2021 ni kuhakikisha...

HUJUMA NZITO YANGA

NA WINFRIDA MTOI UONGOZI wa Yanga upo katika harakati za kuhamishia mechi zao zilizobaki za Ligi Kuu Tanzania Bara...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -