Tuesday, October 27, 2020

Maswali haya yalimfukuzisha kazi Allardyce

Must Read

Hamilton avunja rekodi Ureno

LISBON, Ureno STAA wa mbio za magari Lewis Hamilton, amevunja rekodi ya Valtteri...

Ronaldinho naye ana Corona

RIO, Brazil MKONGWE wa Brazil, Ronaldinho, amethibitishwa ana virusi vya corona. Ronaldinho aliandika...

Sterling amlilia kinda wao Man City

MANCHESTER, England WINGA wa Manchester City, Raheem Sterling, ameandika ujumbe wa majonzi baada ya...

LONDON, England

HATIMAYE kibarua cha kocha wa timu ya Taifa ya England, Sam Allardyce, kiliota nyasi juzi.

Kocha huyo alitegwa na waandishi wa habari wa mtandao wa Telegraph waliojifanya wafanyabiashara kutoka Singapore.

Katika mazungumzo yake na watu hao, alikubali kupokea kitita cha pauni 400,000 ili kuvunja taratibu za usajili zilizowekwa na Chama cha Soka cha England (FA).

Miaka nane iliyopita, FA walitangaza kupiga marufuku uwepo wa makampuni yanayomsimamia mchezaji katika usajili.

Umiliki huo unaofahamika kama ‘third part’, ulikosolewa vikali na FA ambao waliuita utumwa.

Katika mazungumzo na wachunguzi hao bila kujua, Allardyce alitoa majibu yafuatayo ambayo ndiyo yaliyomfukuzisha kazi.

  1. Swali: Nini kilimwangusha Roy Hodgson Euro 2016?

Allardyce: Wachezaji walimwangusha mwishoni. Nafikiri hakuwa na msimamo. Labda alikuwa ni mpuuzi kwa wachezaji wake. Namaanisha kabla ya mchezo dhidi ya Iceland, alikuwa ameshinda mechi 10 za kuwania kufuzu.

Tulitoa sare na Urusi, tulipaswa kuchomoza na ushindi. Tulitoka sare na Slovakia, hivyo tulihitaji sare tu na Iceland, tungefuzu… alishindwa.

  1. Swali: Unamzungumziaje Gary Neville (aliyekuwa msaidizi wa Hodgson)?

Allardyce: Gary Neville hakuwa mtu sahihi kumshauri Hodgson. Kwanza, ukiwa kocha unafanya kile unachokitaka, si kile unachoambiwa na mwingine.

Hapo, Allardyce alikuwa akizungumzia kitendo cha Garry kubishana na Hodgson juu ya kumwingiza, Marcus Rashford, katika mchezo dhidi ya Iceland wakati wa fainali za Euro.

  1. Swali: Unazungumziaje nafasi ya wachezaji kwenye kikosi chako cha England?

Allardyce: Wanaokaa benchi kwenye klabu zao hawawezi kucheza. Huwezi kuwachezesha wakati hawapati nafasi kwenye timu zao.

Kama hawachezi kwenye klabu zao, hata hapa hawawezi kupata nafasi.

  1. Swali: Inawezekana kuizunguka FA na kuvunja taratibu za usajili?

Allardyce: Hakuna tatizo. Tulimpata Valencia (wakati kocha huyo alipokuwa West Ham). Tulitumia mfumo huo kumsajili alipokuwa Mexico.

  1. Swali: Vitendo hivyo bado vinaendelea?

Allardyce: Mbona mambo hayo yanaendelea! Mara nyingi yamekuwa yakifanyika Amerika ya Kusini, Ureno, Hispania, Ubelgiji na hata Afrika.

  1. Swali: Kuna makocha wenye tabia hii?

Allardyce: Wengi sana. Kuna makocha, maofisa na hata wachezaji wanaojihusisha na vitendo vya rushwa.

  1. Swali: Unazungumziaje uboreshaji wa Uwanja wa Wembley?

Allardyce: (FA) ni wapuuzi. Walitumia pauni milioni 870 kuuboresha Wembley, hivyo watalazimika kuendelea kulipa deni hilo.

Ni kama wameujenga upya. Kama wangeujenga sehemu nyingine, wangetumia kiasi kidogo cha fedha, ni pauni milioni 400 pekee zingetumika.

Ilishangaza kumwaga fedha zote hizo kwa ajili ya uboreshaji wa uwanja na watalipa fedha nyingi. Kiasi kikubwa cha fedha kitakachopatikana sasa kitatumika kulipa deni hilo.”

  1. Swali: Kuna tabia ya wachezaji wa sasa na wa zamani wa England kucheza kamari?

Allardyce: Imewahi tokea mara nyingi. Tulicheza sana kamari kuliko wanavyofanya hivi sasa. Tulicheza kamari ya karata kila tulipokuwa njiani baada ya kucheza mchezo wa ugenini.

  1. Swali: Unaizungumziaje FA?

Allardyce: Wako pale kujiingizia fedha tu. Ni uongo? Unajua kama FA ndicho chama cha soka tajiri kuliko vyote duniani? Ndiyo, wana utajiri wa pauni milioni 325.

  1. Swali: Unamzungumziaje Prince Harry (mtoto wa Malkia Elizabeth wa Uingereza).

Allardyce: Ni kijana mbaya. Mbaya, mbaya sana. Hafichi ubaya wake.

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

Hamilton avunja rekodi Ureno

LISBON, Ureno STAA wa mbio za magari Lewis Hamilton, amevunja rekodi ya Valtteri...

Ronaldinho naye ana Corona

RIO, Brazil MKONGWE wa Brazil, Ronaldinho, amethibitishwa ana virusi vya corona. Ronaldinho aliandika ujumbe kupitia ukurasa wake wa...

Sterling amlilia kinda wao Man City

MANCHESTER, England WINGA wa Manchester City, Raheem Sterling, ameandika ujumbe wa majonzi baada ya kinda wa zamani wa timu...

Afua Suleiman afunguka ‘Utalijua Jiji’ ilivyompa ustaa mjini

NA JEREMIA ERNEST JINA alilopewa na wazazi wake ni Afua Suleiman na hata alipojitupa kwenye ulimwengu wa muziki wa...

Keche: Kundi maarufu Ghana linalowatamani Diamond, Kiba, Harmonize

JIACHIE na Staa Wako, wiki hii tumetua mpaka Accra, Ghana kwa kundi maarufu la muziki nchini humo, Keche linofanya vizuri na ngoma...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -