Monday, January 18, 2021

Maswali magumu Lwandamina vs Pluijm

Must Read

Usiyoyajua sare ya Leicester, United

NI katika mechi ya Ligi Kuu ya England iliyomalizika kwa sare ya mabaon 2-2.-Man United wamemiliki mpira...

Eti Zidane anapangiwa kikosi!

IMEFICHUKA kuwa wachezaji waandamizi wa Real Madrid walikaa kikao na Zinedine Zidane kumwambia wachezaji anaopaswa kuwapanga na...

DIDA ASAINI IHEFU FC

Golikipa wa zamani wa Yanga na Simba, Deogratius Munishi ‘Dida’ amejiunga na Timu ya Ihefu inayoshiliki Ligi...

NA EZEKIEL TENDWA,

LICHA ya kwamba Yanga wapo kwenye spidi kali ya kuhakikisha wanatetea ubingwa wao kwa kutoa vipigo vikali kwa kila timu inayojipendekeza mbele yao, yapo maswali kwa mashabiki ambayo bado hayajapatiwa majibu.

Maswali hayo ambayo yanaumiza vichwa vya mashabiki juu ya hatima ya kocha wa sasa, Hans van der Pluijm pamoja na George Lwandamina wa Zesco ya Zambia ambaye siku chache zilizopita alikuja nchini kukutana na Wanajangwani hao kufanya mazungumzo.

Licha ya kwamba mpaka sasa uongozi wa Yanga unakataa kuweka wazi juu ya juhudi zao za kutaka kumchukua Lwandamina kama kocha wao mkuu, taarifa za uhakika zisizo na shaka ni kwamba, mazungumzo ya pande hizo mbili yamekwenda vizuri.

Taarifa za ndani kabisa kutoka Yanga zinadai kuwa Lwandamina ameingia mkataba wa miaka miwili na sasa anasubiri tu kumaliza mkataba wake na Zesco ili aanze kibarua chake hicho kipya kwa Wanajangwani hao.

Kutokana na taarifa hizo za ujio wa Lwandamina, Pluijm aliamua kuandika barua ya kujiuzulu hadi pale Waziri wa Mambo ya Ndani, Mwigulu Nchemba, alipoingilia kati na kumshawishi atengue uamuzi wake huo na kufanikiwa.

Baada ya kuandika barua ya kujiuzulu, ilibidi Pluijm akose mchezo dhidi ya JKT Ruvu na Juma Mwambusi kuwa kwenye benchi Wanajangwani hao wakiibuka na ushindi wa mabao 4-0 na baada ya kufanya mazungumzo na Waziri Nchemba na kurudi, aliiongoza Yanga kuibamiza Mbao FC mabao 3-0 mwishoni mwa wiki iliyopita.

Kurudi tena kwa Pluijm ndiko kunakozua maswali mengi kwa mashabiki kwamba ni nani hasa atasimama kama kocha kwa mabingwa hao watetezi wa Ligi Kuu Tanzania Bara ikizingatiwa kuwa kila mmoja ana uwezo mkubwa kwenye kazi hiyo.

Taarifa za uhakika kutoka Yanga zinadai kuwa Lwandamina atakuja kuwa kocha mkuu na Pluijm atakuwa kama Mkurugenzi wa Ufundi, nafasi ambayo inadaiwa Mholanzi huyo haitaki akitaka kuendelea kuwa kocha.

Taarifa hizo za kutaka kumwondoa Pluijm zimesababisha uwepo wa makundi mawili moja likitaka kocha huyo kuendelea kubaki kwa madai ya kuifanyia timu hiyo mambo makubwa, huku lingine likitaka aondoke kwa madai ya kuanza kuishiwa na mbinu.

Wanaosema Pluijm abaki wanasimamia hoja ya kuipatia timu hiyo makombe mbalimbali likiwamo la ligi kuu na lile la FA huku akifanikiwa kuifikisha timu hatua ya makundi michuano ya Kombe la Shirikisho Afrika.

Wale ambao wanataka aondoke na aje Lwandamina ili kupata changamoto mpya, wanasimamia hoja ya kwamba timu imeshindwa kufika mbali michuano ya kimataifa na CV ya kocha huyo kutoka Zambia inawafanya kumtaka kwa kila namna.

Swali ambalo linatembea kwenye vichwa vya wengi ni kwamba kama Yanga wameshaingia mkataba na Lwandamina watakubalije kuvunja naye mkataba huo kwani itawalazimu kumlipa fedha nyingi Mzambia huyo ambaye mkataba wake na Zesco unamalizika Januari mwakani.

Viongozi wanaomtaka Lwandamina wanajua kuwa anao uwezo mkubwa ndiyo maana Zesco wanahaha kumbakisha huku kocha huyo akiwa pia na ofa mkononi kutoka Free State Stars ya nchini Afrika Kusini.

Maswali hayo ambayo mashabiki wanajiuliza, siku si nyingi jibu litapatikana kwani lazima mmoja kati yao abakie Yanga na mwingine aondoke. Kama ni Lwandamina au Pluijm itajulikana.

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

Usiyoyajua sare ya Leicester, United

NI katika mechi ya Ligi Kuu ya England iliyomalizika kwa sare ya mabaon 2-2.-Man United wamemiliki mpira...

Eti Zidane anapangiwa kikosi!

IMEFICHUKA kuwa wachezaji waandamizi wa Real Madrid walikaa kikao na Zinedine Zidane kumwambia wachezaji anaopaswa kuwapanga na ndiyo maana timu hiyo imeshinda...

DIDA ASAINI IHEFU FC

Golikipa wa zamani wa Yanga na Simba, Deogratius Munishi ‘Dida’ amejiunga na Timu ya Ihefu inayoshiliki Ligi Kuu Tanzania Bara katika kipindi...

JDart Nation wapanga kutawala Africa

CHRISTOPHER MSEKENA MWANAMUZIKI na bosi wa JDart Nation, JDart, amesema miongoni mwa mipango yake kwa mwaka 2021 ni kuhakikisha...

HUJUMA NZITO YANGA

NA WINFRIDA MTOI UONGOZI wa Yanga upo katika harakati za kuhamishia mechi zao zilizobaki za Ligi Kuu Tanzania Bara...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -