Monday, November 30, 2020

MATAJIRI YANGA WAFANYA KWELI

Must Read

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika...

DEWJI: CHAMA NI SIMBA HADI 2022

Kiungo huyo raia wa Zambia, aliyetoa mchangomkubwakwaSimbakufikisharobo fainaliyaLigiyaMabingwaAfrikamsimuwa 2018/19, ikiwamo kutwaa ubingwa wa LigiKuuTanzaniaBarakwa misimumitatu mfululizo, awali...

NA HUSSEIN OMAR

MABOSI wa Yanga wajanja sana asikuambie mtu kwani wanajua kuwa watani zao wa jadi, Simba, wameungana na Azam FC ili Wanajangwani hao wadondoshe pointi tatu Jumamosi na sasa vibopa wa mabingwa hao watetezi wa Ligi Kuu Tanzania Bara, wameamua kukutana na wachezaji wao ili kuwaweka sawa.

Yanga wanakutana na Azam FC, Jumamosi Uwanja wa Taifa, jijini Dar es Salaam, ambapo mchezo huo unatazamwa kwa jicho la tatu na Wanajangwani hao huku Simba nao wakitajwa nao kutaka kuingiza mkono kutokana na hali ilivyo katika mbio za ubingwa.

Katika safari hiyo ya kusaka ubingwa, Simba wapo kileleni wakiwa na pointi 55, huku Yanga wakifuatia na pointi zao 53 hiyo ikimaanisha kuwa timu itakayoteleza itampa mwenzake mwanya wa kuukaribia ubingwa ndiyo maana vita imezidi kuwa kubwa hasa kwa timu hizo mbili kongwe.

Kwa kuujua ukweli huo, vibopa wa Yanga wameamua kuacha shughuli zao Alhamisi ya wiki hii na kwenda kukutana na wachezaji wao ambapo moja ya mambo yanayotajwa kuwa yatazungumzwa ni pamoja na kupewa ahadi nono endapo watawatoa nishai Azam FC.

Kikao hicho kizito kitakachowakutanisha wachezaji, benchi la ufundi pamoja na vigogo hao, kinaashiria makubwa ambayo Yanga wamepania kuyafanya ikizingatiwa kuwa mwishoni mwa wiki iliyopita, viongozi wa matawi ya Yanga Mkoa wa Dar es Salaam, walikutana na kujadiliana namna ya kuwamaliza Azam FC mchana kweupe.

Kigogo mmoja mwenye ushawishi mkubwa ndani ya Yanga, aliliambia BINGWA kuwa wameamua kukutana na wachezaji wao Alhamisi ili kuwapa hamasa na pia watawaahidi donge nono endapo wataibuka na ushindi.

“Ni kweli baada ya viongozi wa matawi kukutana jana (juzi Jumapili), sisi nasi tunatarajia kukutana na wachezaji Alhamisi kuzungumza nao mambo mbalimbali yanayohusiana na timu.

“Jambo kubwa ni kuhusu maandalizi ya mchezo wetu na Azam FC Jumamosi, tunafahamu kuwa wenzetu Simba nao wanataka sisi tupoteze lakini hawataweza kwani tumejipanga kuanzia ndani hadi nje ya uwanja hivyo niwahakikishie mashabiki wetu kuwa wasiwe na wasiwasi wowote.

“Mpaka sasa kuna ahadi ambayo tumesema tutawapa wachezaji endapo watashinda mchezo huo japo haitakuwa busara kutaja hapa, tutakapokutana nao tutawaambia nini tutawapa na hiyo itakuwa siri yao na sisi,” alisema kigogo huyo.

Kwa upande wake Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Mashindano ya Yanga, Mustafa Ulungo, alisema hakuna sababu ya mashabiki na wanachama wa timu hiyo kuwa na hofu juu ya uwezo wa Kocha George Lwandamina na kuwataka kusubiri mambo mazuri kutoka kwa Mzambia huyo.

“Mwalimu bado hajaanza kazi hata kwa asilimia 50 bado, tuwe na subira muda si mrefu Yanga itatisha, tumejipanga kumpa sapoti kubwa kuelekea kwenye mchezo wetu wa Jumamosi dhidi ya Azam,” alisema Ulungo.

Katika hatua nyingine kikosi cha Wanajangwani hao kimeendelea kujifua vilivyo katika Uwanja wa Chuo cha Polisi kujiwinda na mchezo huo unaotarajiwa kuwa mkali kutokana na timu hizo kupaniana.

Yanga wanajua kuwa wakishinda mchezo huo hiyo Jumamosi wataongoza ligi kwa muda huku wakisubiri nini kitawatokea wapinzani wao Simba dhidi ya Kagera Sugar, mchezo utakaochezwa Uwanja wa Kaitaba, mkoani Kagera Jumapili.

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania...

DEWJI: CHAMA NI SIMBA HADI 2022

Kiungo huyo raia wa Zambia, aliyetoa mchangomkubwakwaSimbakufikisharobo fainaliyaLigiyaMabingwaAfrikamsimuwa 2018/19, ikiwamo kutwaa ubingwa wa LigiKuuTanzaniaBarakwa misimumitatu mfululizo, awali ilidaiwa alikuwa yupo katika hatuayamwishoyakujiunganaYanga.

Sven aruka kihunzi

NA ASHA KIGUNDULA KOCHA Mkuu wa Simba, Sven Vandenbroeck, ameruka kihunzi na kuwaachia msala nyota wake, Clatous Chama na...

Sarpong ‘aua’ shabiki Simba

Na MWANDISHI WETU, MWANZA BAO la dakika ya 29 lililofungwa na Michael Sarpong wa Yanga juzi, limesababisha kifo cha...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -