Thursday, December 3, 2020

MATAJIRI YANGA WAWAKESHEA WAARABU

Must Read

HUJUMA NZITO YANGA

NA WINFRIDA MTOI UONGOZI wa Yanga upo katika harakati za kuhamishia mechi zao zilizobaki...

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika...

NA HUSSEIN OMAR,

YANGA wameonyesha kwamba safari hii hawataki tena kuwa wateja wa Waarabu na wameanza mikakati yao kwa kufanya vikao usiku na mchana ili kuhakikisha wanawatoa MC Alger, kwenye mchezo wa marudiano wa kusaka nafasi ya kushiriki hatua ya makundi ya Kombe la Shirikisho Afrika.

Bao la Thaban Kamusoko lilitosha kuwapa Yanga ushindi wa 1-0 dhidi ya MC Alger kwenye mchezo wa kwanza wa michuano hiyo uliofanyika Jumamosi ya wiki iliyopita katika Uwanja wa Taifa, sasa miamba hiyo ya Ligi Kuu Tanzania Bara itakuwa na kazi nzito mjini Algiers nchini Algeria wakati wa mchezo wa marudiano utakaofanyika Uwanja wa Omar Hamadi Jumamosi.

Hivyo klabu hiyo ya Jangwani itasafiri hadi Algeria kwenda kusaka ushindi au sare ya namna yoyote mbele wa Waarabu hao, huku wakijua kwamba watakumbana na vigingi ikiwamo figisu mbalimbali na ndio maana walianza vikao bab kubwa mara moja baada ya mechi ya kwanza.

Mmoja wa wajumbe wa kamati ya utendaji Yanga, aliliambia BINGWA kuwa wamefanya vikao kadhaa vya kujadili mchezo huo wa marudiano pamoja na kupanga mikakati kabambe ya kuwang’oa Waarabu.

“Safari hii hatutaki kuendelea kuwa wateja wa Waarabu kila mara, kwani uwezo wa kuwatoa upo na ndio maana tumeamua kufanya vikao usiku na mchana ili kuweka mikakati mizito, ingawa siwezi kuanika kila kitu hadharani lakini mipango madhubuti ya kufanikisha lengo letu la kutinga hatua ya makundi ya michuano hiyo ya shirikisho imekamilika,” alisema.

 

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

HUJUMA NZITO YANGA

NA WINFRIDA MTOI UONGOZI wa Yanga upo katika harakati za kuhamishia mechi zao zilizobaki...

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul 'Ben Pol' ameshukuru mashabiki kwa...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania...

DEWJI: CHAMA NI SIMBA HADI 2022

Kiungo huyo raia wa Zambia, aliyetoa mchangomkubwakwaSimbakufikisharobo fainaliyaLigiyaMabingwaAfrikamsimuwa 2018/19, ikiwamo kutwaa ubingwa wa LigiKuuTanzaniaBarakwa misimumitatu mfululizo, awali ilidaiwa alikuwa yupo katika hatuayamwishoyakujiunganaYanga.

Sven aruka kihunzi

NA ASHA KIGUNDULA KOCHA Mkuu wa Simba, Sven Vandenbroeck, ameruka kihunzi na kuwaachia msala nyota wake, Clatous Chama na...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -