Tuesday, October 27, 2020

Matawi yabariki Yanga kukodishwa

Must Read

Hamilton avunja rekodi Ureno

LISBON, Ureno STAA wa mbio za magari Lewis Hamilton, amevunja rekodi ya Valtteri...

Ronaldinho naye ana Corona

RIO, Brazil MKONGWE wa Brazil, Ronaldinho, amethibitishwa ana virusi vya corona. Ronaldinho aliandika...

Sterling amlilia kinda wao Man City

MANCHESTER, England WINGA wa Manchester City, Raheem Sterling, ameandika ujumbe wa majonzi baada ya...

NA MARTIN MAZUGWA,

WAKATI timu ya Yanga ikitarajia kuingia kwenye mfumo mpya wa kukodishwa, viongozi wa matawi jijini Dar es Salaam wamekutana katika kikao cha dharura na kubariki ukodishwaji wa timu yao na kuahidi kumsaka mtu anayevujisha siri za klabu hiyo.

Juzi viongozi hao walikuwa na kikao kilichofanyika  katika makao makuu ya klabu hiyo yaliyopo Mtaa wa Twiga  Kariakoo, kilichokuwa kinajadili mambo mbalimbali ikiwemo mkakati wa kumnasa  mvujisha siri huyo pamoja na kusikia hoja za wale wanaopinga mchakato wa kukodishwa kwa timu hiyo.

Viongozi hao wanahofia  endapo mambo  wanayoyapanga yataendelea  kuvujishwa, kuna uwezekano wa  wenzao wa upande wa pili kuiba mbinu  wanazotaka kutumia kuboresha  klabu  yao.

Kikao hicho  kilihudhuriwa na wenyeviti wa matawi na makatibu, pamoja na wajumbe wengine kama viongozi wa Baraza la Wazee.

Kikao hicho kilifikia tamati  kwa wajumbe wote kukubaliana  na suala la ukodishwaji wa timu.

Mwenyekiti wa tawi la Yanga Ubungo Terminal, Hassan Msigiti (Hans),  alisema mkutano huo ulikwenda vizuri na wamezungumza mambo ya kujenga timu yao pamoja na mwenyekiti wao huyo na kwamba wale ambao hawataki maendeleo ya klabu yao hiyo hawatafanikiwa.

“Kuna baadhi ya watu  ambao hawapendi maendeleo ya timu, hawataki suala hili lifanyike, sisi kama wanachama na mashabiki wa Yanga, tutahakikisha jambo hili linafanikiwa bila wasiwasi wowote,” alisema.

Alisema Yanga ina miaka mingi lakini hakuna maendeleo yoyote na sasa amejitokeza mtu ambaye anataka kuifikisha mbali, hivyo hawawezi kumwachia na badala yake watahakikisha wanashirikiana naye mpaka mwisho.

Alisema kumekuwa na kundi la watu likiwapotosha Wanayanga kuhusu suala hilo ambalo tayari limefikia kikomo kwa ridhaa ya viongozi wa bodi ya udhamini kukubali jambo hili kwa ajili ya maendeleo ya Yanga.

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

Hamilton avunja rekodi Ureno

LISBON, Ureno STAA wa mbio za magari Lewis Hamilton, amevunja rekodi ya Valtteri...

Ronaldinho naye ana Corona

RIO, Brazil MKONGWE wa Brazil, Ronaldinho, amethibitishwa ana virusi vya corona. Ronaldinho aliandika ujumbe kupitia ukurasa wake wa...

Sterling amlilia kinda wao Man City

MANCHESTER, England WINGA wa Manchester City, Raheem Sterling, ameandika ujumbe wa majonzi baada ya kinda wa zamani wa timu...

Afua Suleiman afunguka ‘Utalijua Jiji’ ilivyompa ustaa mjini

NA JEREMIA ERNEST JINA alilopewa na wazazi wake ni Afua Suleiman na hata alipojitupa kwenye ulimwengu wa muziki wa...

Keche: Kundi maarufu Ghana linalowatamani Diamond, Kiba, Harmonize

JIACHIE na Staa Wako, wiki hii tumetua mpaka Accra, Ghana kwa kundi maarufu la muziki nchini humo, Keche linofanya vizuri na ngoma...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -