Wednesday, November 25, 2020

MATOKEO SITA YA KUKUMBUKWA MICHUANO YA MATAIFA YA AFRIKA

Must Read

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika...

DEWJI: CHAMA NI SIMBA HADI 2022

Kiungo huyo raia wa Zambia, aliyetoa mchangomkubwakwaSimbakufikisharobo fainaliyaLigiyaMabingwaAfrikamsimuwa 2018/19, ikiwamo kutwaa ubingwa wa LigiKuuTanzaniaBarakwa misimumitatu mfululizo, awali...

LIBREVILLE, Gabon

MICHUANO ya Mataifa ya Afrika imemalizika Jumapili ya wiki iliyopita na Cameroon kufanikiwa kunyakua taji lao la tano nchini Gabon.

Mashabiki wa soka walishuhudia nyota mbalimbali wa soka wa Ligi Kuu England wakiachana na timu zao kwa ajili ya michuano hiyo.

Pamoja na nyota hao na wale wa ligi nyingine Ulaya, lakini kuna mambo mengi ya kukumbukwa kwenye historia ya michuano hiyo.

 

1994: Kuibuka kwa Zambia

Aprili 27 mwaka 1994, timu ya Taifa ya Zambia ilikuwa ikisafiri kwenda Senegal kwa ajili ya kucheza mechi ya kufuzu fainali za Kombe la Dunia kabla ya ndege yao kuanguka kwenye Bahari ya Atlantic, mita 500 kutoka mji mkuu wa Gabon, Libreville.

Abiria wote 25 na wafanyakazi wa ndege watatu walifariki.

Janga hilo lilitingisha sana nchi hiyo ya Zambia na dunia ya soka, ambapo ‘Chipolopolo’ (Copper Bullets) walikuwa wamekwishaifunga Italia kwenye michezo ya Olimpiki mwaka 1988 na ilikuwa ikielekea kwenye fainali yao ya kwanza ya  Kombe la Dunia, lakini walifariki kabla ya ndoto yao kutimia.

Mwaka uliofuata Zambia waliunda timu mpya ambayo ilifanikiwa kuingia fainali kwenye michuano ya Afcon 1994, ikakosa ubingwa kwa kufungwa mabao 2-1 na Nigeria.

 

2012: Herve Renard aipa Zambia taji

Zambia walishindwa kunyakua taji mwaka 1994, lakini walionja ladha ya ubingwa mwaka 2012. Wangeweza kunyakua taji hilo la Afcon mjini Libreville miaka 19 kama si ajali ya ndege.

Lakini chini ya kocha wa Ufaransa, Herve Renard, Zambia walikutana na Ivory Coast kwenye fainali.

Baada ya mchezo kuingia hatua ya matuta, zilipigwa penalti 18 na Copper Bullets wakawa mabingwa kwa kupata 8-7.

 

2015: Morocco yajitoa kuogopa ebola

Kutokana na kuongezeka kwa kasi ya ugonjwa wa ebola nchi za Afrika Magharibi, wenyeji Morocco walitaka michuano ya Afcon 2015 iahirishwe, wakiogopa kuandaa michuano hiyo kwa kuhofia virusi vya ugonjwa huo vitatapakaa nchini mwao.

Shirikisho la Soka Afrika (CAF) wakataa kuahirisha michuano hiyo, ikiwa imebakia miezi miwili kabla ya michuano hiyo kuanza Morocco walikataa kuandaa. Timu hiyo ilitolewa kwenye michuano hiyo na CAF kama adhabu.

Nchi nyingine tano zilikataa, kabla ya michuano hiyo kufanyika Equatorial Guinea na kushuhudia bingwa akipatikana kwa matuta kama mwaka 2012, ambapo Ivory Coast walishinda kwa matuta 9-8 dhidi ya Ghana.

2010: Basi la Togo lashambuliwa

Mwaka 2010, basi lililokuwa limebeba wachezaji wa timu ya Taifa ya Togo lilipokuwa likielekea kwenye michuano hiyo nchini Angola, lilishambuliwa kwa risasi na watu waliokuwa wamejificha sura zao kama ninja.

Watu tisa wakiwamo wachezaji, walijeruhiwa pamoja na mchezaji wa zamani wa Arsenal na Manchester City, Emmanuel Adebayor, alikuwa mmoja wao.

 

2006 & 2012: Drogba alituliza vita

Mshambuliaji wa Ivory Coast, Didier Drogba, hakuwa na nguvu kwenye klabu yake ya Chelsea, lakini nguvu zake kwenye soka aliweza kuzitumia hata kwenye masuala ya kutuliza vita ya wenyewe kwa wenyewe nchini kwao.

Wakati wa vita kati ya mwaka 2002 na 2007, Drogba alipiga magoti ‘live’ kwenye televisheni pamoja na timu yote mwaka 2005 kuomba wapiganaji wa pande zote mbili kuacha mapigano.

Baada ya kuwapo kwa amani, aliomba mechi ya kufuzu michuano ya Mataifa ya Afrika mwaka 2008 kati ya Ivory Coast na Madagascar ifanyike mji wa Bouake, kama alama ya kuwaleta pamoja watu wote wa Ivory Coast.

 

 

2002 & 2004: Jezi za Cameroon

Cameroon walibeba taji la Mataifa ya Afrika mwaka 2002 nchini Mali, waliifunga Senegal kwa penalti.

Ubingwa huo wa Indomitable Lions haukuwa wa kawaida kwenye michuano hiyo baada ya timu hiyo kutumia jezi za kata mikono.

Wakati staili hiyo ya jezi ikianza kuwa maarufu Afrika, Shirikisho la Soka la Kimataifa (Fifa) lilipiga marufuku Cameroon kuvaa jezi hizo kwenye fainali za Kombe la Dunia mwaka 2002, kutokana na kukosa sehemu ya kuweka nembo yao.

Lakini mwaka 2004, Cameroon walivaa tena jezi zao kwenye michuano ya Mataifa ya Afrika, Fifa walichukizwa tena na jambo hilo na kuwapiga fainali kwa kutumia jezi hiyo kwenye mchezo wa robo fainali dhidi ya Nigeria, ingawa waliruhusu kutumika wakati wa kujiandaa na mechi.

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania...

DEWJI: CHAMA NI SIMBA HADI 2022

Kiungo huyo raia wa Zambia, aliyetoa mchangomkubwakwaSimbakufikisharobo fainaliyaLigiyaMabingwaAfrikamsimuwa 2018/19, ikiwamo kutwaa ubingwa wa LigiKuuTanzaniaBarakwa misimumitatu mfululizo, awali ilidaiwa alikuwa yupo katika hatuayamwishoyakujiunganaYanga.

Sven aruka kihunzi

NA ASHA KIGUNDULA KOCHA Mkuu wa Simba, Sven Vandenbroeck, ameruka kihunzi na kuwaachia msala nyota wake, Clatous Chama na...

Sarpong ‘aua’ shabiki Simba

Na MWANDISHI WETU, MWANZA BAO la dakika ya 29 lililofungwa na Michael Sarpong wa Yanga juzi, limesababisha kifo cha...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -