Friday, October 23, 2020

MATUKIO YA MICHEZO YALIYOTIKISA AGOSTI 2016

Must Read

Fati aweka rekodi Barcelona

CATALUNYA, Hispania ANSU Fati ameweka rekodi ya mchezaji kinda wa kwanza kufunga mabao...

Lampard amshika mkono Silva

MANCHESTER, England KOCHA wa Chelsea, Frank Lampard, amesema atamtumia, Thiago Silva, katika mechi nyingi msimu huu licha ya...

Tuchel awatolea uvivu Mbappe, Neymar

PARIS, Ufaransa KOCHA wa PSG, Thomas Tuchel, amechukizwa na kiwango kibovu walichoonyesha mastaa wa timu hiyo, Kylian...

NA MWANDISHI WETU,

AGOSTI ilikuwa mwezi wa Olimpiki na kama taifa tulipeleka wawakilishi wetu, je, tuna cha kujivunia? BINGWA leo linakuletea matukio ya michezo yaliyotikisa Agosti 2016 hii ikiwa ni mwendelezo wa kujikumbusha matukio muhimu tunapokaribia kuuaga mwaka 2016 na kuukaribisha mwaka 2017.

Simba na Simba Day yao

Katika kusherehekea miaka 80 tangu kuanzishwa kwa Klabu ya Simba, timu hiyo ilicheza mchezo wa kimataifa wa kirafiki dhidi ya AFC Leopards ya Kenya kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam na kuibuka na ushindi wa mabao 4-0.

Ibrahim Ajib alifunga mabao mawili huku mengine yakipachikwa na wachezaji wapya, Mrundi Laudit Mavugo na Shizza Kichuya.

Mchezo huo ambao pia ulitumika kuwatambulisha wachezaji wapya ikiwamo na kocha wao mpya Mcameroon Joseph Omog na sehemu ya maandalizi kuelekea msimu mpya, ulihudhuriwa na mfanyabishara Mohammed ‘Mo’ Dewji, ambaye alitoa ofa ya kuinunua klabu hiyo kwa Sh bilioni 20.

Azam yabeba Ngao

Baada ya kukosa taji la Ngao ya Jamii kwa miaka mitatu mfululizo, mabingwa wa Afrika Mashariki na Kati, Azam FC, wamefanikiwa kulibeba kufuatia ushindi wa mabao 4-1 kwa mikwaju ya penalti dhidi ya Yanga ambao ni mabingwa wa Ligi Kuu Bara.

Mchezo huo ambao huashiria pazia la Ligi Kuu Bara msimu mpya kufunguliwa, ulichezwa Uwanja wa Taifa, jijini Dar es Salaam na hadi dakika 90 zinamalizika timu zote zilikuwa zimefungana 2-2.

Shujaa wa Azam FC kwenye hatua ya penalti alikuwa Aishi Manula aliyepangua penalti ya beki Ramadhan Hassan ‘Kessy’ huku nyingine ya Yanga ikikoswa na Haruna Niyonzima aliyegongesha mwamba wa juu na mpira kutoka nje wakati penalti za Azam FC zilifungwa na John Bocco, Himid Mao, Shomari Kapombe na Michael Bolou. Deogratius Munish ‘Dida’ ndiye aliyefunga penalti pekee kwa Yanga.

Serengeti Boys yaishangaza Afrika Kusini

Timu ya soka ya vijana chini ya umri wa miaka 17, Serengeti Boys, imeiondoa kwenye mashindano ya kufuzu Kombe la Vijana timu ya Afrika Kusini maarufu kama Amajimbos kwa jumla ya mabao 3-1.

Katika mchezo wa kwanza uliochezwa Uwanja wa Dobsonville ulioko Soweto, Afrika Kusini, ndiyo waliokuwa wa kwanza kupata bao kwa njia ya penalti iliyofungwa na Linamandlia Mchilizeli dakika ya 65 kabla ya Ally Msingi kuisawazishia Serengeti Boys dakika tano baadaye pia kwa penalti.

Serengeti Boys ilitumia vyema uwanja wake wa nyumbani katika mchezo wa marudiano licha ya kuwa pungufu na kufanikiwa kupata mabao mawili yaliyofungwa na Mohamed Abdallah dakika ya 34 na Shaban Zubeiry dakika ya 84.

Msimu mpya 2016/17 waanza

Jumla ya mabao nane yamefungua pazia la msimu mpya wa Ligi Kuu Bara 2016/17 uking’oa nanga katika viwanja mbalimbali nchini.

Mchezo ambao ulishuhudia idadi kubwa ya mabao ni ule uliochezwa Uwanja wa Taifa, jijini Dar es Salaam na Simba kuibuka na ushindi wa mabao 3-1 dhidi ya Ndanda FC.

Hamad Tajiri wa African Lyon aliingia kwenye kumbukumbu baada ya kuwa mchezaji wa kwanza msimu mpya wa ligi kuonyeshwa kadi nyekundu timu yake ikitoka sare ya bao 1-1 dhidi ya Azam kwenye Uwanja wa Chamazi.

Simbu ang’ara Olimpiki

Tanzania kwa mara ya kwanza ilishika nafasi za juu mbio za marathon katika mashindano ya Olimpiki yaliyofanyika Rio de Janeiro nchini Brazil, baada ya mwanariadha Alphonce Felix Simbu kumaliza nafasi ya tano.

Simbu alitumia muda wa saa mbili dakika 11 na sekunde 15 na kuibua shangwe kwa Watanzania waliokua wanafuatilia mashindano hayo, licha ya kushindwa kumaliza nafasi ambazo zingemwezesha kutwaa medali.

Mshindi kwenye mbio hizo alikuwa Mkenya Eliud Kipchoge akitumia muda wa 2:08:44 akifuatiwa na Feyisa Lilesa raia wa Ethiopia aliyetumia muda wa 2:09:54 huku nafasi ya tatu ikimwendea Mmarekani Galen Rupp dakika moja baadaye. Watanzania wengine waliomaliza mbio za marathon ni Saidi Juma Makula katika nafasi ya 43 na Fabiano Joseph Naasi nafasi ya 112.

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

Fati aweka rekodi Barcelona

CATALUNYA, Hispania ANSU Fati ameweka rekodi ya mchezaji kinda wa kwanza kufunga mabao...

Lampard amshika mkono Silva

MANCHESTER, England KOCHA wa Chelsea, Frank Lampard, amesema atamtumia, Thiago Silva, katika mechi nyingi msimu huu licha ya kuwa na umri wa miaka...

Tuchel awatolea uvivu Mbappe, Neymar

PARIS, Ufaransa KOCHA wa PSG, Thomas Tuchel, amechukizwa na kiwango kibovu walichoonyesha mastaa wa timu hiyo, Kylian Mbappe na Neymar, kwenye mechi...

IBRA:Kifaa kipya Konde Gang aliyetembea kwa mguu kumwinda Harmonize

NA BRIGHITER MASAKI UKITAJA vijana wanaofanya vizuri katika mziki wa bongo fleva, huwezi kukosa kumtaja msanii chipukizi anayefahamika zaidi...

Jay-Z: Mama aliingilia bifu langu na Nas

-Z: Mama aliingilia bifu langu na Nas New York, Marekani HAKUNA shabiki wa Hip hop asiyelifahamu...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -