Friday, December 4, 2020

MATUKIO YA MICHEZO YALIYOTIKISA FEBRUARI 2016

Must Read

HUJUMA NZITO YANGA

NA WINFRIDA MTOI UONGOZI wa Yanga upo katika harakati za kuhamishia mechi zao zilizobaki...

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika...

NA MWANDISHI WETU,

BAADA ya jana kutazama matukio muhimu ya michezo yaliyotokea Januari 2016, leo BINGWA linamulika matukio ya michezo yaliyotokea Februari 2016, hii ikiwa ni mwendelezo wa kujikumbusha matukio muhimu tunapokaribia kuuaga mwaka 2016 na kuukaribisha mwaka 2017.

Geita, Polisi Tabora ‘kicheko’

Timu ya soka ya Geita Gold na Polisi Tabora, zilipata matokeo ya kushangaza katika mchezo wa mwisho kutafuta timu ambayo itaungana na African Lyon na Ruvu Shooting kufuzu kucheza Ligi Kuu Bara msimu wa 2016/17.

Geita Gold katika mchezo wa mwisho iliifunga JKT Kanembwa 8-0 na kuongoza Kundi C, ambapo wapinzani wao wa karibu Polisi Tabora wakiishushia kipigo cha mabao 7-0 Oljoro JKT katika mchezo mwingine wa mwisho wa kundi hilo.

Kufuatia matokeo hayo ya mwisho ya kushtusha Kundi C Ligi Daraja la Kwanza, Rais wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Jamal Malinzi, alitangaza shirikisho hilo kuzuia kuitangaza Geita Gold washindi wa Kundi C hadi uchunguzi wa kinachodaiwa kupanga matokeo ukamilike.

Kikapu yapata kocha mzungu

Shirikisho la Mpira wa Kikapu Tanzania (TBF) limeingia mkataba wa miaka miwili na kocha raia wa Marekani, Mathew McCollister, kwa ajili ya kufundisha timu za taifa na pia kutoa ushauri kwa timu za vijana.

Uteuzi wa McCollister umerahisishwa na kocha wa zamani wa timu ya taifa ambaye pia ni raia wa Marekani, Al Sokaitis, ambaye alikuwa nchini mwaka 2012 kusaidia kuendeleza mchezo wa kikapu.

Katibu Mkuu BMT ang’olewa

Waziri mwenye dhamana ya michezo, Nape Nnauye, atangaza kufuta uteuzi wa Henry Lihaya kama Katibu Mkuu wa Baraza la Michezo Tanzania (BMT) kwa kile kilichoelezwa kushindwa kutimiza majukumu yake.

Uamuzi huo unakuja siku chache baada ya Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa, kufanya kikao na maofisa wa BMT pamoja na viongozi na wadau wa michezo.

Lihaya ameshikilia wadhifa huo kwa takribani miaka saba na wizara imesema muda huo unatosha na hakuna jipya analoweza kuleta kuendeleza michezo nchini.

Yanga, JKU safi Afrika

Timu za Yanga ya Ligi Kuu Bara na JKU ya Zanzibar, zafuzu raundi inayofuata ya michuano ya kimataifa ngazi ya klabu huku Mafunzo ya Zanzibar ikichezea kipigo.

Yanga iliwaondoa kwenye mashindano ya Klabu Bingwa Afrika, Cercle de Joachim ya Mauritius, kwa jumla ya mabao 3-0 ambapo katika mchezo wa kwanza, Yanga ilishinda 1-0 bao lililofungwa na Donald Ngoma huku Amisi Tambwe na Thaban Kamusoko wakifunga katika mchezo wa marudiano.

JKU nao walifuzu raundi inayofuata Kombe la Shirikisho bila hata kuingiza timu uwanjani baada ya Gaborone United ya Botswana kujiondoa huku Mafunzo ikiondolewa kwenye Klabu Bingwa Afrika baada ya kufungwa jumla ya mabao 4-0 na AS Vita Club ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.

Cheka amnyamazisha Mserbia

Bondia Mtanzania, Francis Cheka, atwaa mkanda wa Mabara wa WBF baada ya kumpiga kwa pointi bondia raia wa Serbia anayeishi Uingereza, Geard Ajetovic katika pambano lililofanyika viwanja vya Leaders jijini Dar es Salaam.

Katika pambano hilo uzito wa Super Middle la raundi 12 lililosimamiwa na Rais wa WBF, Goldberg Haward, huku mwamuzi akiwa Eddie Marshall kutoka Afrika Kusini, majaji wote watatu walimpa ushindi Cheka (115-112, 116-111, 115-112).

Hata hivyo, Ajetovic aliyeambatana na kocha wake, Aksu Ahhysaidar, alisema haamini kama amepigwa na Cheka na kwamba alistahili kushinda japo hawezi kupingana na uamuzi wa majaji.

Wakenya watawala Kili Marathon

Mbio za kilomita 42 Kilimanjaro Marathon zilizofanyika Moshi, zilishuhudia wanariadha kutoka Kenya wakitawala upande wa wanaume na wanawake.

Kirui Kiprotich alitumia muda wa saa mbili dakika 16 na sekunde 43 kuibuka mshindi upande wa wanaume, huku nafasi ya pili ikichukuliwa na Kenneth Ronoh (2:16.48) na Bernard Kimaiyo (2:16.52) akimaliza nafasi ya tatu.

Kwa upande wa wanawake, Alice Kibor aliibuka mshindi akitumia muda wa 2:38.03 huku akifuatiwa na Wakenya Elizabeth Chemweno (2:44.20) na Alice Serser (2:44.56).

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

HUJUMA NZITO YANGA

NA WINFRIDA MTOI UONGOZI wa Yanga upo katika harakati za kuhamishia mechi zao zilizobaki...

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul 'Ben Pol' ameshukuru mashabiki kwa...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania...

DEWJI: CHAMA NI SIMBA HADI 2022

Kiungo huyo raia wa Zambia, aliyetoa mchangomkubwakwaSimbakufikisharobo fainaliyaLigiyaMabingwaAfrikamsimuwa 2018/19, ikiwamo kutwaa ubingwa wa LigiKuuTanzaniaBarakwa misimumitatu mfululizo, awali ilidaiwa alikuwa yupo katika hatuayamwishoyakujiunganaYanga.

Sven aruka kihunzi

NA ASHA KIGUNDULA KOCHA Mkuu wa Simba, Sven Vandenbroeck, ameruka kihunzi na kuwaachia msala nyota wake, Clatous Chama na...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -