Friday, December 4, 2020

MATUKIO YALIYOMPA UJIKO AKRAMA

Must Read

HUJUMA NZITO YANGA

NA WINFRIDA MTOI UONGOZI wa Yanga upo katika harakati za kuhamishia mechi zao zilizobaki...

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika...

NA SALMA MPELI

MCHEZO wa marudiano wa Ligi Kuu Tanzania Bara kati ya Simba na Yanga, umemalizika bila kuwapo kwa vurugu zozote tofauti na ilivyozoeleka mara kwa mara.

Mwamuzi Methew Akrama amefanikiwa kupuliza kipenga cha mwisho cha mchezo huo wa Ligi Kuu Tanzania Bara, akitoka uwanjani bila lawama yoyote kutoka kwa pande zote mbili.

Hivyo huo unaweza ukawa ni moja ya mchezo wa mahasimu hao ambao mwamuzi ameumaliza bila ya kufanya makosa makubwa, kama ambavyo imekuwa ikitokea na kusababisha waamuzi mbalimbali kufungiwa.

Kuna matukio kadhaa ambayo angeshindwa kuyaamua vizuri basi Akrama angebeba lawama na kuvurunda mchezo huo.

Penalti

Uamuzi wa Akrama kutoa penalti dakika za mwanzo wa mchezo huo baada ya Novat Lufunga kumchezea vibaya Obrey Chirwa eneo la hatari, ulikuwa sahihi na haukuonekana kulalamikiwa na mashabiki wala wachezaji wa Simba.

Lufunga alishindwa kumiliki mpira na kuwahiwa na Chirwa ambaye aliingia na mpira huo kwenye eneo la hatari kabla ya kuangushwa na beki huyo wa Simba na hakukuwa na ubishi kwamba ilikuwa penalti ya wazi ambayo ilikwamishwa wavuni na Simon Msuva.

Kadi ya njano ya Dida

Baada ya bao la Msuva, mlinda mlango wa Yanga, Deogratius Munish ‘Dida’, alianza kupoteza muda na kudunda mpira mara mbili, jambo lililosababisha aonyeshwe kadi ya njano.

Baada ya kosa hilo na kuonyeshwa kadi ya njano, Simba walipewa mpira wa adhabu ambao walitakiwa kugongeana kwanza kabla mtu kupiga shuti golini. Shuti la Said Ndemla lilipaa juu ya lango.

Uamuzi wa kadi hiyo haukuwa na shaka, kwani ni kweli Dida alifanya kosa kwa kuudunda mpira zaidi ya mara mbili baada ya kuudaka na kupoteza muda, ambapo kwa kawaida kipa anatakiwa akae na mpira akiwa ameushika bila kuzidisha sekunde sita.

Kuangushwa kwa Mo

Tukio jingine ambalo lingeweza kumtia matatani Akrama, ni ile faulo ya Andrew Vicent ‘Dante’ kwa Mohamed Ibrahim ‘Mo’, ambapo walisukumana na kiungo huyo wa Simba kuzidiwa nguvu na kujiangusha ndani ya 18, pamoja na tukio zima lilifanyika nje ya eneo hilo.

Kadi nyekundu ya Bokungu

Dakika ya 55 beki wa Simba, Janvier Bokungu, alionyeshwa kadi nyekundu ya moja kwa moja, baada ya kumchezea vibaya Obrey Chirwa nje kidogo ya eneo la 18.

Moja ya vitu vinavyoharibu mechi hizo ni maamuzi ya kadi nyekundu na penalti, lakini maamuzi yake yalikuwa sahihi na ndio maana hakukuwa na fujo kwa mashabiki wala wachezaji.

Ajib kujiangusha

Kama si umakini wa Akrama basi mambo yangekuwa mengine, kwani kitendo cha Ibrahimu Ajib kujiangusha kwenye eneo la hatari la Yanga baada ya kuminyana na Dante, mwamuzi mwingine angetaka kutupia nafasi hiyo kufuta lawama kwa Simba baada ya kutoa penalti na kuwaonyesha kadi nyekundu.

Lakini haikuwa hivyo kwa Akrama, aliweza kuruhusu mchezo uendelee akiashiria kwamba, Ajib hakuchezewa vibaya na huo ndio ulikuwa ukweli, kwani mshambuliaji huyo wa Simba alijilegeza ili apewe penalti.

Huo ulikuwa mchezo wa pili kwa Akrama, baada ya ule wa Ligi Kuu Tanzania Bara uliopigwa Oktoba 3 mwaka 2012 na kumalizika kwa sare ya bao 1-1.

Katika mchezo huo, Akrama alimtoa Msuva kwa kadi nyekundu dakika ya 77 kwa kumrudishia faulo aliyekuwa beki wa Simba, Juma Nyosso, huku akimwonyesha kadi ya njano Haruna Moshi ‘Boban’, badala ya nyekundu kutokana na kumchezea vibaya Kelvin Yondani ambaye alipata majeraha yaliyomweka benchi kwa muda mrefu.

Kufuatia matukio hayo, Akrama alifungiwa kuchezesha ligi Oktoba 6 mwaka huo, huku msaidizi wake namba mbili Ephrony Ndissa wa Dar es Salaam akipewa onyo.

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

HUJUMA NZITO YANGA

NA WINFRIDA MTOI UONGOZI wa Yanga upo katika harakati za kuhamishia mechi zao zilizobaki...

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul 'Ben Pol' ameshukuru mashabiki kwa...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania...

DEWJI: CHAMA NI SIMBA HADI 2022

Kiungo huyo raia wa Zambia, aliyetoa mchangomkubwakwaSimbakufikisharobo fainaliyaLigiyaMabingwaAfrikamsimuwa 2018/19, ikiwamo kutwaa ubingwa wa LigiKuuTanzaniaBarakwa misimumitatu mfululizo, awali ilidaiwa alikuwa yupo katika hatuayamwishoyakujiunganaYanga.

Sven aruka kihunzi

NA ASHA KIGUNDULA KOCHA Mkuu wa Simba, Sven Vandenbroeck, ameruka kihunzi na kuwaachia msala nyota wake, Clatous Chama na...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -