Wednesday, January 20, 2021

MATUKIO YALIYOTIKISA MICHEZO MWAKA 2016

Must Read

Usiyoyajua sare ya Leicester, United

NI katika mechi ya Ligi Kuu ya England iliyomalizika kwa sare ya mabaon 2-2.-Man United wamemiliki mpira...

Eti Zidane anapangiwa kikosi!

IMEFICHUKA kuwa wachezaji waandamizi wa Real Madrid walikaa kikao na Zinedine Zidane kumwambia wachezaji anaopaswa kuwapanga na...

DIDA ASAINI IHEFU FC

Golikipa wa zamani wa Yanga na Simba, Deogratius Munishi ‘Dida’ amejiunga na Timu ya Ihefu inayoshiliki Ligi...

LONDON, England

TAYARI siku tano zimepita tangu kuanza kwa mwaka 2017.Hata hivyo, mwaka jana kulikuwa na mambo mengi yaliyojitokeza kwenye ulimwengu wa michezo.Lakini mambo haya nane yalikuwa gumzo kwa kipindi hicho cha miezi 12.

dhabu ya staa Maria Sharapova

Februari mwaka jana, staa wa mchezo wa tenisi, mwanadada Maria Sharapova, alijikuta kwenye majanga baada ya kufungiwa kwa kipindi kirefu na Shirikisho la Kimataifa la Mchezo huo (ITF).

Mrembo huyo alikumbana na adhabu hiyo ya kufungiwa miaka miwili baada ya kukiri kuwa alitumia dawa za kusisimua misuli wakati wa michuano ya Australia Open.

Saharapova alitumia dawa aina ya meldonium ambazo zimepigwa marufuku na Shrikia la Kimataifa la Kuzuia Utumizi wa Dawa za Kuongeza Nguvu.

Hata hivyo, adhabu ya miaka miwili ilipungua hadi miezi 15 baada ya Sharapova kukata rufaa na anatarajiwa kuanza kuonekana uwanjani Aprili 2017.

Leicester kuchukua ubingwa

Msimu uliopita wa Ligi Kuu England ulikuwa gumzo duniani kote kutokana na kile kilichotokea. Hakuna aliyetarajia kuiona Leicester ikitwaa ubingwa.

Katika msimu wa 2014-15, Leicester ilinusurika kushuka daraja, lakini msimu uliofuata mwaka jana, walichukua ubingwa.

Aibu ya England Euro 2016

Huenda mashabiki wa timu ya Taifa ya England wakabaki na kumbukumbu nzuri ya mwaka jana.

Timu yao hiyo iliondoshwa ‘vibonde’  Iceland kwenye michuano ya Euro 2016 katika hatua ya mtoano.

Kabla ya mchezo huo uliohitimisha safari yao, Iceland hawakuwa wakipewa nafasi kubwa ya kuibuka na ushindi kwani hiyo ilikuwa ni michuano yao ya kwanza mikubwa.

Wanamichezo Urusi na dawa za kulevya

Julai mwaka jana, ripoti ya Shirika la Kimataifa la Kuzuia Utumizi wa Dawa za Kulevya liliibua shutuma ya Urusi kuwa na mpango wa kuwezesha wanamichezo wake kutumia dawa hizo kwenye michuano mikubwa.

Baadhi ya wanamichezo wa nchi hiyo walibaniwa kushiriki mashindano ya Paralympic yaliyofanyika jijini Rio, Brazil. Lakini pia, wanamichezo wengi walivuliwa medali zao.

Mechi moja kumkimbiza Sam Allardyce

 

Ni miongoni mwa matukio ya kukumbukwa kwa mwaka 2016. Baada ya kuwa kwenye benchi la ufundi la England kwa siku 67, kocha Sam Allardyce alitimuliwa baada ya kufungwa mechi moja pekee.

Bosi huyo hakufukuzwa kwa sababu ya matokeo, bali tabia yake ya kujihusisha na vitendo vya rushwa iliyoibuliwa na mtandao wa Daily Telegraphy.

Rosberg kustaafu mbio za magari

Baada ya kushinda taji la Formula 1 kwa mara ya kwanza, mkali wa mbio za magari, Nico Rosberg, alitangaza kuachana na mchezo huo.

Dereva huyo wa timu ya Mercedes, alikuwa na mafanikio makubwa kwa mwaka 2016 hasa kutokana na ushirikiano wake na Lewis Hamilton.

“Nimemaliza, huu ni mwisho wa historia. Kinachofuata ni kuwa baba na mume na hicho ndicho ninachokiangalia kwa sasa,” alisema staa huyo alipokuwa  akitangaza uamuzi wake wa kujiweka kando na mchezo wa mbio za magari.

Ajali ya ndege ya Chapocoense

Ilikuwa ni mwishoni mwa Novemba ndipo ndege iliyokuwa imewabeba wachezaji na wafanyakazi wa klabu ya Chapocoense ya Brazil ilipoanguka.

Ndege hiyo ilianguka nchini Colombia na kuua watu 71 wakiwamo wachezaji 22.

Timu hiyo ilikuwa njiani kuelekea Colombia ambako ingecheza mchezo wao wa kwanza wa fainali ya michuano ya  Copa Sudamericana.

Hata hivyo, baadaye iliripotiwa kuwa timu hiyo imekabidhiwa kombe bila kucheza fainali, ikiwa ni sehemu ya kuwapooza machungu.

Mbali na kupewa kombe, pia klabu nne za ligi kuu nchini Brazil ziliahidi kuipa Chapecoense baadhi ya wachezaji wake.

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

Usiyoyajua sare ya Leicester, United

NI katika mechi ya Ligi Kuu ya England iliyomalizika kwa sare ya mabaon 2-2.-Man United wamemiliki mpira...

Eti Zidane anapangiwa kikosi!

IMEFICHUKA kuwa wachezaji waandamizi wa Real Madrid walikaa kikao na Zinedine Zidane kumwambia wachezaji anaopaswa kuwapanga na ndiyo maana timu hiyo imeshinda...

DIDA ASAINI IHEFU FC

Golikipa wa zamani wa Yanga na Simba, Deogratius Munishi ‘Dida’ amejiunga na Timu ya Ihefu inayoshiliki Ligi Kuu Tanzania Bara katika kipindi...

JDart Nation wapanga kutawala Africa

CHRISTOPHER MSEKENA MWANAMUZIKI na bosi wa JDart Nation, JDart, amesema miongoni mwa mipango yake kwa mwaka 2021 ni kuhakikisha...

HUJUMA NZITO YANGA

NA WINFRIDA MTOI UONGOZI wa Yanga upo katika harakati za kuhamishia mechi zao zilizobaki za Ligi Kuu Tanzania Bara...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -