Monday, November 30, 2020

MAVUGO, AJIB WAUNDIWA KAMATI

Must Read

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika...

DEWJI: CHAMA NI SIMBA HADI 2022

Kiungo huyo raia wa Zambia, aliyetoa mchangomkubwakwaSimbakufikisharobo fainaliyaLigiyaMabingwaAfrikamsimuwa 2018/19, ikiwamo kutwaa ubingwa wa LigiKuuTanzaniaBarakwa misimumitatu mfululizo, awali...

NA ZAITUNI KIBWANA

KAMA ulidhani Simba watakuwa wamelala isingizi wa pono wakati huu Ligi  Kuu Bara ikiwa inaelekea ukingoni, utakuwa umeachwa mbali, kwani Wekundu hao wa Msimbazi wanafanya mambo yao kimyakimya kana kwamba wanataka kummaliza mtani wao wa jadi pasipo purukushani.

Ishu ipo hivi, Simba wanatambua ugumu wa mechi zilizopo mbele yao, hasa zile za Kanda ya Ziwa, ambazo vigogo wa timu hiyo wameona si wakati mwafaka kwao kulala, hivyo kuamua kuandaa mipango thabiti ya kuhakikisha wanaibuka na pointi zote Kanda ya Ziwa.

Kutokana na ugumu wa michezo hiyo, nguvu zimeelekezwa kwa wachezaji, kwani kuanzia sasa watakuwa wakifuatiliwa kwa karibu zaidi pamoja na wale wanaowasiliana nao kwa simu mara kwa mara.

Kazi ya kwanza ni kutuma watu maalumu Kanda ya Ziwa ili kuhakikisha wanajua mbinu zote za timu wanazokwenda kupambana nazo.

Pia imewekwa nguvu ya fedha, kutokana na bonasi wanayopewa wachezaji wa kikosi hicho kila wanaposhuka dimbani ili kuwaongezea morali.

Hiyo ni mbali na Sh milioni 5 inayotolewa kila baada ya mechi, ambayo inachangwa na wadau mbalimbali wa timu hiyo.

Utaratibu huo unaonekana kuwapiga bao wapinzani wao, Yanga, ambao kwa sasa wapo kwenye misukosuko ya fedha hadi kusababisha wachezaji kutegemea mishahara yao ya kila  mwezi.

Pia Simba imekuwa na kamati maalumu ambayo imewahusisha wachezaji wa zamani ambayo imesaidia kurudisha hamasa kubwa ndani ya kikosi hicho, tofauti na wapinzani wao, Yanga, ambao mara nyingi hutumia benchi la ufundi pekee.

Yanayofanywa ndani ya Simba, hata kocha msaidizi wa timu hiyo, Jackson Mayanja, amekiri kuwa yamekuwa chachu ya kikosi chao kufanya vizuri kwenye michezo yake ya Ligi Kuu msimu huu.

“Mbali na ufundi wa uwanjani, lakini hili la hamasa ni jambo linalotusaidia sana, nina imani litatusaidia pia kwenye michezo iliyosalia,” alisema.

Simba ina kibarua kinene Kanda ya Ziwa itakapokabilana na timu za Toto Africans na Mbao FC (Mwanza) pamoja na Kagera Sugar ya Bukoba.

Mechi dhidi ya Toto inatajwa kama mtihani mgumu zaidi kwa Simba, huku Mbao FC na Kagera Sugar zikionekana  zisizotabirika.

Ngoma nyingine nzito kwa Simba itakuwa nyumbani jijini Dar es Salaam, itakapovaana na African Lyon, Stand United na Mwadui FC.

Lyon iliitungua Simba bao 1-0 katika pambano la mzunguko wa kwanza.

Simba inaongoza katika msimamo wa ligi hiyo, ikiwa na pointi 55 baada ya kucheza mechi 24, sawa na Yanga iliyoko nafasi ya pili ikiwa na pointi 53.

Previous articlePIGA HAOO
Next articleBOSSOU AWAPA UJUMBE MZITO YANGA
- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania...

DEWJI: CHAMA NI SIMBA HADI 2022

Kiungo huyo raia wa Zambia, aliyetoa mchangomkubwakwaSimbakufikisharobo fainaliyaLigiyaMabingwaAfrikamsimuwa 2018/19, ikiwamo kutwaa ubingwa wa LigiKuuTanzaniaBarakwa misimumitatu mfululizo, awali ilidaiwa alikuwa yupo katika hatuayamwishoyakujiunganaYanga.

Sven aruka kihunzi

NA ASHA KIGUNDULA KOCHA Mkuu wa Simba, Sven Vandenbroeck, ameruka kihunzi na kuwaachia msala nyota wake, Clatous Chama na...

Sarpong ‘aua’ shabiki Simba

Na MWANDISHI WETU, MWANZA BAO la dakika ya 29 lililofungwa na Michael Sarpong wa Yanga juzi, limesababisha kifo cha...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -